Kaka kuna kitu kimoja muhimu sana watu wanakisahau wanapochagua simu nacho ni SAR
SAR ni kiasi cha miaonzi ambacho mwili wa binadamu una-absorb. kila unapoongea na simu ujue kichwa chako kinakuwa kinazungukwa na hii mionzi. kuna kiasi cha mionzi kinakuwa ni salama kwa binadamu na kuna kiasi kikizidi kinaweza kuleta madhara.
Wenzetu wa marekani wana FCC kwa ajili ya kupima simu, Ulaya wana EU na baadhi ya nchi kama india wanatumia FCC pia.
Hawa FCC na EU wanazipima hizi simu kama zina mionzi mibaya na ni salama kutumika kwa binadamu then zikifaulu ndio zinaruhusiwa kupita madukani. Ila sisi Tanzania hakuna chombo cha ukaguzi na tunanunua simu ambazo hazijawahi kupimwa kabisa na tunakuwa kwenye risk na hii michina. 7
Ukichunguza watu wengi wanaokuja kudump simu africa huwa simu hizo haziuzwi ulaya na marekani wanaogopa kuzipeleka sababu simu zinakuwa hazina viwango. hili ni jambo kubwa la kuliangalia kwenye afya yako.
Matatizo mengine ya clone zinakuwa pia sio reliable, unaweza kuiformat simu ikabadilika kabisaa, touchwiz ikatoka, boot animation ikabadilika, au hata isiwake tena. pia wana tabia ya kudanganya specs run cpu z ili kuona specs halisi za simu.