Je, kujitolea itumike kama kigezo cha kuajiriwa?

Je, kujitolea itumike kama kigezo cha kuajiriwa?

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2017
Posts
1,011
Reaction score
1,915
Je Kujitolea ni sahihi kutumika kama kigezo cha kuajili nchini?

Juzi kuna mjadala bungeni mh spika Tulia Akson alitoa Rai kwa wizara ya Afya na tamjsemi na utumishi wa umma kuangalia zaidi watu wanaojitolea na kuwapa kipaumbele katika nafasi za ajira pindi zinapotolea.

Je kama mwanajf unadhani ni sahihi ikiwa hakuna Sera nzuri katika watu wanaojitolea..Kuanzia malipo posho na mengineyo
 
Kujitolea Kuna faida mbili, Moja ni kumfanya mtaalamu husika kuwa active katika kada yake. Imagine mtu kamaliza chuo 2015 anasubiri ajira hajitolei kichwani atakua na kitu gani zaidi ataanza kuona Mambo mageni mengi. Lakini faida nyingine ni kujitengenezea CV, kipato Cha kujikimu na connection hili linawafanya wanaojitolea kuwa na CV nzuri tofauti na yule ambae hajitolei.

Kuhusu ajira. Kujitolea isitumike Kama kigezo Cha kuajiriwa. Kwasababu serikali ndio yenye kutegemewa kutoa ajira Kwa kundi kubwa la watu katika kada hizo mbili. Kwamiaka yote hiyo ambayo ajira zilisimama watu wangeishije?

Kuna waliooa na kuolewa na wanaopalangana na maisha. Je mtu huyo angeishije kwakujitolea nakupewa laki au wakati mwingine bila kupewa chochote? Kama ajira zipo zije na watu waajiriwe kutokana na vigezo vyakitaaluma.

Mimi najitolea tangu 2020 na chuo nimemaliza 2017 hivyo serikalini anaehusika na ajira namba yangu ya NIDA ni 1990062053............22 msinisahau maana nitazeekea home.

Nafurahi kama watatumia kigezo hiki angalau napata matumaini yakuajiriwa mwaka huu. Tayari wamechukua data zetu kwahiyo tunasubiri dirisha lifunguliwe tuombe.
 
Ubaya ni kwamba, hata hizo nafasi za kujitolea zinatolewa kwa kujuana. Kuna ambaye yuko nyumbani anatamani ajitolee ila anakosa wa kumshika mkono. Ukisema anayejitolea umuajiri na asiyejitolea umuache ni kumuonea. Watu waajiriwe kwa kufanya interview na kufaulu basi.
 
Waache iwe AJIRA HURIA kama ilivyo biahshara huria! Una vigezo pambania sio kubebwa!

Capitalism ndiyo inayotulea!
 
Back
Top Bottom