Je kipi kinachomfanya mtu kujivunia kuwa wa kabila fulani??

proskaeur

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
1,571
4,925
Habarini za asubui.wana Jf, wakubwa zangu shikamooni wadogo habari zenu!!

Wakuu kwa upande wangu mimi sioni kama kuna haja ya mtu kujivunia kuwa kabila fulan tena mbele za watu ,kwa sababu nachokifikiria mimi ni kuwa kabila la mtu halimfanyi kuwa mtu fulani katika jamii ,, mfano halimuongezei CV kwenye kuomba kazi au kumpa priority yoyote katika eneo fulani

Pia kabila lina mtofautisha mtu na mtu kutokan na mila na desturi za kabila lake mfano kwenye mambo ya vyakula,, lakini kwa tuliopo mijini tumesahau kabisa desturi hizo tangu tumeondok vijijini kwetu na tukifika mjini tunasema tunajivunia kuwa wa kabila fulani wakati mila na desturi za makabila yetu hatuzienzi tumewaachia BIBI na BABU zetu uko vijijini!!!

Hvyo basi kwa mwenye uelewa na haya mambo naomba anieleweshe ni kipi mtu hasa hasa alieko mjini kujivunia kuwa wa kabila fulani??

mnakaribishwa kwa maoni!!!!
 
Shukrani kwa Mwalimu Nyerere alishatutoa huko zamani sana kwenye mambo ya eti kujivunia ukabila.Ukabila ni chanzo kikubwa cha ubaguzi.

Yatosha sana kujivunia kuwa mtanzania basi.
 
Binafs Nathan ni kutoelewa tu. .and kuamua kubakia primitive as we used to be but in reality we are all the same don't matter of were you come from if your stupid you will remain stupid kabila haliwezi kukufanya mjanja. ..lakini ukiamua kujichanganya na watu wengine badala ya kujitenga you will realise that you can learn from anyone around you and observe the knowledge that they have
 
Ungekuwa miongoni mwa hayo makabila makubwa ungeona radha ya kujivunia kuwa humo
 
sisi bwana shari tu tukiona kuna wafuasi nao wanatwangana baaaaassssss roho kunoga
 
Wengine hata hatujihesabii kama tuna makabila,maana hatufanyi wala kujua chochote chenye kuhusu makabila yetu.
 
Wapo wengi wenye tabia hizo hasa wale wanaojiita makabila makubwa na ndiyo yanayofanya upendeleo hata kwenye kazi ma maslahi mengine, wao wanatabia ya kubagua makabila mengine kama yetu. Hii tabia haina maana sana lkn hawaachi cjui itakwisha lini.
 
Ungekuwa miongoni mwa hayo makabila makubwa ungeona radha ya kujivunia kuwa humo
ingkua vizur mkuu ukaelezea atlist kwa kifupi kipi kilichomo kwenye hayo makabila makubwa kinachofany mtu kujivunia kuwa wa kabila husika ili na mim nielewe
 
mimi huwa sipendi tu ..
sifa wanazopachika makabila ..
mfano ukisikia mhehe -niangusage/wala mmbwa
mmakonde wala panya
wasukuma washamba
waluguru wafupi
wachaga wabahili

huwaga sipendi kabisa..
kujielewesha namna kabila fulani walivo hata kama hawana tabia hizo tena.
 
hayo mambo bado wanayo wale watu wasiojielewa mtu anayejielewa hawezi kudharau au kujiona bora kuliko mwingine kisa kabila na ukiona hivyo ujue huyo mtu kakosa lake binafsi so inabidi asimamie kabila fulani ili kujioonesha kana kwamba yeye ni bora kuliko mtu mwingine
 
Habarini za asubui.wana Jf, wakubwa zangu shikamooni wadogo habari zenu!!

Wakuu kwa upande wangu mimi sioni kama kuna haja ya mtu kujivunia kuwa kabila fulan tena mbele za watu ,kwa sababu nachokifikiria mimi ni kuwa kabila la mtu halimfanyi kuwa mtu fulani katika jamii ,, mfano halimuongezei CV kwenye kuomba kazi au kumpa priority yoyote katika eneo fulani

Pia kabila lina mtofautisha mtu na mtu kutokan na mila na desturi za kabila lake mfano kwenye mambo ya vyakula,, lakini kwa tuliopo mijini tumesahau kabisa desturi hizo tangu tumeondok vijijini kwetu na tukifika mjini tunasema tunajivunia kuwa wa kabila fulani wakati mila na desturi za makabila yetu hatuzienzi tumewaachia BIBI na BABU zetu uko vijijini!!!

Hvyo basi kwa mwenye uelewa na haya mambo naomba anieleweshe ni kipi mtu hasa hasa alieko mjini kujivunia kuwa wa kabila fulani??

mnakaribishwa kwa maoni!!!!
Unaanza anzaje kumlinganisha mchagga na mgogo
 
Mtu yeyote anayetanguliza au anayejitangaza kabila lake. Maanake huyo kuna kitu kimepungua katika wasifu wake so anatafuta kitu cha ku support. So hapo ataweka ukabila au dini. Ila kama angekamilika asingeweka kabisa hayo mambo ya kabila.
 
Back
Top Bottom