Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,798
- 71,218
Ni utaratibu uliowekwa na Tume (NEC) kuwa vipeperushi vyote vinavyohusiana na uchaguzi lazima vikaguliwe na kupitishwa kabla ya matumizi.
Majuzi Tume imetoa karatasi ya mfano ya kupigia kura ikiwa na mpangilio wa majina yote ya wagombea yatakavyokuwa. Lakini CCM wameichukua na kuihariri na wanaitumia kuwaelekeza watu jinsi ya kupiga kura huku wakiwa wamekata picha na maelezo ya wagombea mwiba kwao.
James Mbatia alihukumiwa kusimamishwa kampeni kwa kosa hilo lakini jana amefutiwa adhabu hiyo, jee yalikuwa ni maandalizi kwa Magufuli kupewa nafasi ya kuvunja sheria hiyo ya kutumia kipeperushi bila kusajiliwa?
Mbona hawa Makamishna wa Tume wanajifedhehesha utadhani hakuna maisha mengine baada ya uchaguzi?
Kipeperushi hicho ni upotoshaji mkubwa sana, na kwa vile wafuasi wengi wa CCM ni maamuma sio rahisi kugundua.