BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Ni zamu ya Kikwete
Baada ya Lowassa, Rostam...
na Irene Mark
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
BAADA ya wanamtandao wawili maarufu, Edward Lowassa na swahiba wake kisiasa, Rostam Aziz kutikiswa kisiasa, dalili za awali zimeanza kuonyesha kwamba, jina la Rais Jakaya Kikwete nalo limeanza kuwekwa chini ya mstari mwekundu.
Matukio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa, wiki hii imeanza kuchukua mkondo mbaya kwa Rais Kikwete ambaye kwa mara ya kwanza jina lake limeanza kuingizwa katika maeneo mabaya, ambayo rekodi zinaonyesha ndiyo waliyopita marafiki zake wawili, Lowassa na Rostam ambao hivi karibuni walikumbwa na gharika ya kisiasa wanayoendelea kukabiliana na athari zake.
Kwa mara ya kwanza, jina la Rais lilitajwa katika gazeti la kila wiki la MwanaHalisi ambalo katika habari yake kubwa lilionyesha dalili za kumhusisha Kikwete na ajira yenye mwelekeo wa kutia shaka ya mtoto wake mkubwa Ridhiwani ambaye anafanya kazi katika kampuni binafsi ya uwakili kama mwanasheria.
Siku chache tu baada ya kutajwa huko kwa rais waziwazi na kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani Desemba 21, mwaka 2005, katika sakata linalomhusisha mtoto wake huyo, dalili za mara moja zilianza kuonyesha kutikisika kwa mamlaka za dola.
Katika hali isiyotarajiwa, suala hilo la kutajwa kwa Rais Kikwete lilianza kuchukua mwelekeo unaoonyesha kuwa wenye lengo mahususi la kumpaka matope katika mwenendo unaokwenda sambamba na kuwapo kwa madai mengine ya kuwapo kwa jitihada mahususi za kumsafisha Lowassa ambaye hivi karibuni alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu baada ya jina lake kutajwa katika kashfa ya Richmond.
Hali hiyo ilisababisha kuitishwa mara moja kwa mkutano wa pamoja kati ya Jukwaa la Wahariri na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) uliofanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam na kutoa tamko kuhusu masuala hayo makubwa mawili; kuchafuliwa kwa Rais Kikwete na kusafishwa kwa Lowassa.
Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinaeleza kuwa, wamiliki na wahariri hao waliafikiana kimsingi kuwa, kazi ya wanahabari si kuchafua au kusafisha viongozi, bali kuandika habari za kweli, zilizotafitiwa na ambazo zinazitendea haki pande zote zinazotajwa katika habari husika.
Katika tamko lililotolewa kwa pamoja na Mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, vyombo vya habari vilikubaliana kimsingi kudumisha misingi na kanuni za uandishi wa habari wakati wanapotimiza wajibu wao.
Mkutano huo kwa namna ya pekee ulionyesha kupanda kwa joto la kisiasa hapa nchini, tangu jina la Rais Kikwete lilipoanza kutajwa katika masuala ambayo yanaonyesha mwelekeo wa wazi wa kuendelea na mashambulizi ya waziwazi ya kuchafuana miongoni mwa viongozi wakitumia baadhi ya vyombo vya habari lynch mob.
Siku moja tu baada ya angalizo hilo kutolewa na MOAT na Jukwaa la Wahariri, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe jana alivurumisha tuhuma nzito dhidi ya Rais Kikwete akieleza kushangazwa kwake na namna anavyoshughulikia wizi wa fedha katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) maarufu kwa jina la Kashfa ya EPA.
Mbowe aliyekuwa akihutubia kongamano la wanawake wa CHADEMA lililofanyika katika Ukumbi wa Urafiki jijini Dar es Salaam, jana, alisema kushindwa kwa rais kuyatumia ipasavayo madaraka yake ya kikatiba dhidi ya wezi hao ambao sasa inadaiwa kuwa wameanza kuzirejesha fedha hizo, kunamfanya yeye mwenyewe aonekane akiingia katika kashfa hiyo.
Alisema Rais Kikwete anahusika katika kashfa ya ufisadi kwa sababu ameshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi licha ya kuelezwa mara kadhaa kwamba anayo mamlaka ya kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria mafisadi waliotajwa kwenye taarifa ya kampuni ya ukaguzi ya Ernst & Young.
Alisema zipo juhudi za makusudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya nne chini ya utawala wa Rais Kikwete za kuwalinda na kuwatetea watuhumiwa wa ufisadi, hasa waliodhulumu fedha za EPA.
Zipo juhudi za makusudi za kuwalinda na kuwatetea mafisadi wa EPA tunalaani kauli ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo, kwamba fedha zilizoibwa EPA zimeanza kurudi huku kukiwa na siri katika kuwataja hadharani waliorudisha.
Huu ni uhuni, kwa wezi kurudisha fedha halafu wanaendelea kutamba mitaani. Hii inatulazimu kuamini kuwa Rais Kikwete anahusika. Tunataka hiyo timu ya rais iliyotumwa kuwachunguza hao mafisadi itutajie majina ya walioanza kurudisha fedha zetu na hatua gani za kisheria zilizochukuliwa dhidi yao.
Sheria inaruhusu kukamatwa kwa watu hao na kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi, tunasema ngoma hii ni nyepesi, najua tutakutana na serikali bungeni katika mkutano wa Aprili, wakitukwamisha tunaileta hoja yetu ya kutaka majina ya wanaorudisha fedha kwa wananchi, alisema Mbowe.
Katika hilo, alibainisha kwamba wabunge wa chama chake wamejizatiti katika kupigania maji safi na salama kwa kuwa fedha nyingi za wananchi zinaliwa na wachache kwa manufaa binafsi.
Alitoa mfano kuwa zaidi ya sh bilioni 133 za EPA zilizoibwa na watu wachache zingetosha kusambaza huduma za mabomba ya maji safi na salama kwa kila kijiji nchini.
Laiti hao mafisadi wangejua ni kiasi gani wanawatesa wanawake na watoto katika suala zima la maji safi na salama, Watanzania tungepiga hatua kubwa kimaendeleo, alisema Mbowe na kuongeza kuwa ni lazima serikali ieleze ukweli kuhusu ufisadi na kuwachukulia hatua stahiki watuhumiwa wote.
Akizungumza kuhusu umoja na mshikamo wa kitaifa, Mbowe aliwata wanawake wa CHADEMA kutowabagua wala kuwatenga wanawake wenye itikadi nyingine, badala yake washirikiane nao katika kuwabadili kiitikadi. Pia aliwashauri kutoingiza uzalendo wa kijinsia katika kutetea haki zao na kutokuwa tayari kufaidi matunda ya ufisadi.
Msiingize uzalendo wa kijinsia katika kutetea haki zenu hasa kwenye suala la ufisadi msiwe tayari hata kidogo kufaidi matunda ya ufisadi, taifa linaangamia kwa ajili ya wachache. Nawaomba tuichukue vita hii tuipeleke katika familia zetu.
Lazima tujue tu wasafi kwa kiwango gani kabla ya kuwahukumu wenzetu tukianzia kwenye familia tutaweza kupambana katika ngazi ya taifa, alisisitiza Mbowe.
Alisema, nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa, kuna mwanamke aliyeteseka. Aidha, kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa ni Tuelekeze rasilimali fedha katika usawa wa kijinsia.