JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
wana jamvi,
..nadhani mnakumbuka kwamba Raisi aliagiza shule zote sasa zitumie kitabu cha aina moja kufundishia somo husika.
..nilidhani Raisi alipaswa kusisitiza kuhusu waalimu na watunga mitihani kuzingatia syllabuss.
..masuala ya vitabu nadhani kila mtu anachagua kitabu kile ambacho anaona kinamsaidia kuelewa vizuri somo husika.
..halafu hivi katika dunia ya leo tunapaswa kweli kutegemea source/kitabu moja/kimoja katika kujifunza?
..JE RAISI ALIKURUPUKA???
kusoma makala nzima bonyeza hapa.
..nadhani mnakumbuka kwamba Raisi aliagiza shule zote sasa zitumie kitabu cha aina moja kufundishia somo husika.
..nilidhani Raisi alipaswa kusisitiza kuhusu waalimu na watunga mitihani kuzingatia syllabuss.
..masuala ya vitabu nadhani kila mtu anachagua kitabu kile ambacho anaona kinamsaidia kuelewa vizuri somo husika.
..halafu hivi katika dunia ya leo tunapaswa kweli kutegemea source/kitabu moja/kimoja katika kujifunza?
..JE RAISI ALIKURUPUKA???
Paschally Mayega @ Tanzania Daima said:Rais wangu utaratibu wa kitabu zaidi ya kimoja vya kiada kwa somo moja ndio utaratibu unaofahamika zaidi katika mfumo wa elimu sehemu kubwa ya dunia. Katika semina elekezi iliyotangulia kabla ya kufunguliwa rasmi kwa Tamasha la Vitabu la Dunia kule Ujerumani, nilisikia faraja sana mjumbe wa APNET (African Publishers Network) alipoutolea mfano, utaratibu tunaoutumia Tanzania kuwa ni mfano unaopaswa kuigwa na mataifa mengine.
Katika mfumo wetu huu somo moja linakuwa na vitabu zaidi ya kimoja, kutoka kwa wachapishaji tofauti tofauti. Vitabu vyote vinakuwa vimepimwa ubora na mamlaka zile kuu mbili, BAKITA na EMAC na kupewa ithibati. Kinacholeta tija hapa ni pale wachapishaji tofauti tofauti wanapovipeleka vitabu vyao bora shuleni (sokoni) kuuza. Mwalimu anakuwa na uhuru wakuchagua kitabu kitakachomfaa zaidi kufundisha vizuri.
Kwa kuwa vyote vina ithibati, Mwalimu ataangalia mambo mengine ambayo yanaitwa nguvu ya soko. Ataangalia kwa mfano kati ya vitabu bora hivi kipi kina bei ya chini ili apate vitabu vingi zaidi kuwatosha wanafunzi wake kwa pesa aliyotengewa na hivyo kuwanufaisha wanafunzi wengi kwa kupunguza uwiano.
Ataangalia kwa mfano ni kitabu kipi kimeboreshwa zaidi kwa manufaa ya darasa lake au shule yake. Ataangalia kwa mfano ni kitabu kipi kimefafanua somo husika zaidi kwa uelewa wa wanafunzi wake. Akiwa na vya kulinganisha, atachagua kilicho bora zaidi.
Rais wangu katika mfumo wa vitabu vingi kila mchapishaji anakuwa katika hali ya ushindani kitabu chake kisije kikapitwa kwa ubora na kitabu cha mchapishaji mwenzake. Atafuatilia kwa karibu kwa lengo la kuongeza elimu iliyomo kufuatana na mabadiliko ya mara kwa mara ya mazingira na nyakati.
Huku ndiyo kutoa elimu bora, kitu ambacho kwa utaratibu wa kitabu kimoja mambo yote haya hayazingatiwi. Mchapishaji atabaki kuangalia faida yake tu na maslahi ya Waziri aliyemteua.
kusoma makala nzima bonyeza hapa.