Tumeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha, hakuna kama uumbaji wa Mungu.Sisi ni smart sana na kila sekunde ubongo unafanya hesabu ukiwa watembea usigongane na vitu ukate vipi kona vyote kwenye subconscious kiasi kwamba we don't even think or realize.
Binadamu ana input device za kila aina kuanzia macho kama camera, ngozi kama heat detector, na kwa ajili ya kuhisi mazingira, masikio kama sound input sawa na mic, na hisia nyingone ambazo hata hatuzielewi. Mfano kama kuna hatari nywele kusisimka, au kuna jambo baya limetokea unaanza kufeel something is not okay.
Ukija kwenye uhifadhi wa data, we fikiria unakumbukumbuku kiasi gani kwenye kichwa chako tena kwa format za video tupu.
Yani toka unajotambua unaweza kukumbuka tukio kuanzia mwanzo mpaka mwisho kama unatazama video.
Binadamu ni complicated na smart sana. Njoo kwenye mfumo wa uendeshaji mwili, jinsi mwili unavyotengeneza kinga, unavyochukua hatua kukulinda, yani huo usmart wa jali ya juu sana.
Sema tunayachukulia poa kwasababu yanatendeka bila hata kufuatilia.