Je, JK akikupa post serikalini utakubali?

Je, JK akikupa post serikalini utakubali?

Wengi wanafiki tu.Wewe leo hii mfano uteuliwe ubunge,halafu upewe wizara utachomoa?Wengi wapiga kelele JF kwavile wako nje ya system,lakini wakikatiwa ulaji ndiyo hao watakuwa wakwanza kuifisadi nchi.

Wewe wasema. Kuna maisha nje ya ufisadi mazee.
 
wengi wetu tumekimbilia kujibu hii post bola tafakari mzuri, mtoa mada hajaiweka vizuri, wadhifa upi? maana hata ubunge ni wadhifa na CUF wameukubali.
mimi sioni tatizo ni nini hasa hapa
 
wengi wetu tumekimbilia kujibu hii post bola tafakari mzuri, mtoa mada hajaiweka vizuri, wadhifa upi? maana hata ubunge ni wadhifa na CUF wameukubali.
mimi sioni tatizo ni nini hasa hapa
Kasema wazi kabisa labda wewe ndio hukumsoma vizuri..
 
Ukiwa kama mwana JF ambaye unataka mabadiliko ya kweli kwa watanzania, leo hii JK anakuteua kushika wadhifa fulani serikalini au katika shirika la umma; je utakubali? Kama ndio au hapana, tupe sababu za msingi! Ulimwengu alikwisha wahi mkatalia Mkapa!!

mkuu kuiondoa CCM kwa kura imekuwa shida kubwa kwa jinsi walivyo hodhi kila kitu kuanzia tume hadi polisi. pengone sasa pia tuombe mabadiliko ya kweli toka kwa watendaji ktk nyadhifa za juu. hivyo ukiteuliwa ninafasi yako kuleta hayo mabadiliko ya kweli kwa kusimamia haki
 
mkuu nyadhifa ni dhana pana sana haiishii ktk uwaziri na mkuu wa mashirika.
anyway kwanini ukatae?
Duh mkuu wangu swali kaliuliza jamaa kinachotakiwa ni sisi kujibu na kutoa sababu..muhimu alosema mtoa mada ni ajira seriklaini au ktk mashirika ya Umma!
 
Swali lako ni very challenging sababu ku nadharia ni rahisi kudiscus lakini kihali halisi chance ya watanzania kuchomoa ni below 15%.

But theoretically binafsi mano JK akinipa nafasi ya uongozi kwenye Shirika la umma kama

ATCL- Nitamwambia strategic plan itakuwa kubinafissha shirika serikali iondokane na headache yake.
TRL- Nitaomba anihakikishie serikali itatoa ruzuku ya kulifua fua hili shirika la reli na kulifanya liwe mali ya umma .kwa zai ya %70. Kwa Vison yangu hili shirika ni uti wa mgongo wa uchumi.
NHC, NSSF, etc- strategic plan itakuwa kujenga japo nyumba 50 kila mwaka kwa mikoa mitano mikubwa (Mwanza -arusha-Mbeya etc)badala Focus itakuwa kustabilize maisha ya watu wa kati na kupendezesha miji. kwa kujenga nyumba za bei nafuu.

Sasa sijui kwa utamaduni wetu JK au rais anavyoteua viongozi yeye ndio anaweka rules au anayemteu ndo anamshauri Rais .Tujiulize kwenye haya mashirika ma CEO wanavyopewa kazi wanapewa maksii na kuwa evaluated kwa jinsi walitvyotekeleza maagizo au kwa jinsi walivyotoa ushauri

Ukitaka kujua state ya mashirika yetu ya umma jaribu kuangalia ogranisaion structure zao.
CEO - Anateuliwa na Rais lakini kazi zake za kila siku bosi wake wa karibu ni Bodi. Ingekuwa vizuri kama angekuwa anateuliwa baada ya kujieleza nini atafanya au angependa kufanya kwenye shirika.
Bodi shirika- Baadhi wanateuliwa na waziri wengine wanaingia kwa nafasi zao za kisiasa. Hawatakiwi kuwa na nguvu sana lakini jiulize vikao vya bodi kwa vina mshiko mkubwa. je ni rushwa CEO kuwakamata wazee???
Wajurugenzi wa idara kwenye shirika- Sijui kwa kweli kwenye mashirika yetu hawa wanateuliwa au kuchaguliwa vipi

Swali lingine
sasa jiulize ikulu/ Rais anakupa shirika ni yeye anakupa dondoo ili CEO aandee strategiic plan ya kuzitekeleza au Ikulu inakuwa imemaliza kila tu CEO kazi yake nikufuata maelekezo? Naona Its complicated, ambiguous with sphageed conflict of interest

kifupi its complicated kwa mfumo uliopo wa mashirika mengi ya umma.Theoretically inabidi ukatae lakini practically kwa kuwa tuna matumbo na malisho yaliypo hayatoshi inabidi ukubali tu.
 
if i will be a supervisor..

1.Nitakuwa mkali kwa wezi wote na sitawaonea haya hata kama ni wakongwe wa chama

2.Nitahakikisah mabadiliko makubwa ya sheria yanafanyika ili yaendana na kasi ya kuleta mabadiliko

3.Watu wote ambao hawana uwezo wa kuleta mabadiliko nitawang'oa,itakuwa siyo serikali ya kulipana fadhila..
Gembe

Hayo yote utayafanya kwa kipindi gani kabla hujatimuliwa, watakuwa wajinga wakuangalie tu wakati unawang'oa, thubutu........
 
Nitarudia kusema kwamba adui wa maendeleo yetu sio Kikwete hata kidogo. Na haifai kabisa kwa Mtanzania kufikiria kwamba hatakubali kulitumikia Taifa kwa sababu ni utawala wa Kikwete..Inachotakiwa wewe kufanya ni kulitumikia Taifa kadri ya uwezo wako na ikitokea sababu ya kiutawala inayokuzuia kufanya kazi acha, kwa sababu hili sio swala la siasa na majungu. Je, ina maana akiondoka yeye ndio watu tutakubali kufanya kazi serikalini au?

Kikwete mwenyewe is weak kwa sababu tunamtaka afanye sawa na fikra za matumaini yetu kwa maana nyingine ni mwenzetu ambaye kashindwa kutuletea maendeleo kutokana na mapungufu yake.. adui yako siku zote hana mapungufu na kama anayo hiyo itakuwa advantage kwako kummaliza..

Hivyo JK sio adui na hakika akikuchagua wewe ina maana ni mwanzo wa yeye kukubali na kukukabidhi wewe mamlaka ambayo yeye yamemshinda na anataka wewe unayepiga makelele hapa uyaweze. Accept the challenge na utuonyeshe what has to be done, ndio tutajua unayoyapigia kelele hapa kweli yana dawa yake..
 
Itabidi nifikirie mara mbilimbili kwa vile najua wazi siku nitakapokubali huo wadhifa ndio utakuwa mwisho wa kuwa na mawazo na fikira huru. Nitakuwa nimejinyima fulsa ya kutumia elimu na uwezo wangu bila ya kuingiliwa na mtu.

Najua kutokana na system yetu ilivyo ni vigumu sana kubadilishwa na mtu mmoja, kwa hali hiyo itabidi kushirikiana na waliopo na kwa kufanya hivyo tayari nitakuwa nimemezwa na system.

Ndiyo maana nimesema itabidi nifikirie sana kabla ya kukubali, kwa vile kama nitakubali na kuiheshimu dhamira yangu basi sintakaa madarakani kwa zaidi ya miezi miwili otherwise nitakuwa nimeisaliti dhamira yangu.
 
Kuna haja ya kutumia akili pana. Mimi ni mwananchi. Raisi kanipa kazi ya kutumikia wananchi. Nitaikubali bila hata remorse. Nitaifanya kwa uadilifu hata kama zipo forces without zinataka nipindishe. Nikiona sivyo nitamrudishia kazi yake. Simple and straight forward. Hii ishu kuwa watumishi wote serkalini ni mafisadi siyo sahihi. Wapo wachapa kazi wazuri tu.
 
Kuna haja ya kutumia akili pana. Mimi ni mwananchi. Raisi kanipa kazi ya kutumikia wananchi. Nitaikubali bila hata remorse. Nitaifanya kwa uadilifu hata kama zipo forces without zinataka nipindishe. Nikiona sivyo nitamrudishia kazi yake. Simple and straight forward. Hii ishu kuwa watumishi wote serkalini ni mafisadi siyo sahihi. Wapo wachapa kazi wazuri tu.
Kuchukua kazi ya kuteuliwa ni aina nyingine tu UFISADI as simple as that.
 
Watu wanampigia debe sasa JK ili wapate post. Sasa wewe hizo post utazipataje?
 
ganesh,
Mkuu wapo watu walioteuliwa na Rais kufanya kazi na wanazifanya tena kwa ufanisi pamoja na mungu makubwa kupikwa..Wapo makatibu wakuu wa wizara wanaozifanya kazi zao vizuri tu na kwa kupitia wao tumeweza kuona machafu kibao ya serikali na hasa mawaziri waliopita(wanasiasa)..Kwa hiyo ganish hata wewe unaweza kuteuliwa na ukaweza kushiriki kikamilifu pasipo kuwa fisadi na sii lazima uwe mwana CCM, sema tu ktk mfumo wetu wa KULANAO ndio kazi kuepukana.
 
Wengi wanafiki tu.Wewe leo hii mfano uteuliwe ubunge,halafu upewe wizara utachomoa?Wengi wapiga kelele JF kwavile wako nje ya system,lakini wakikatiwa ulaji ndiyo hao watakuwa wakwanza kuifisadi nchi.

P53 lingekuwa jambo la maana sana kama ungeongelea nafsi yako kwanza ingawa jibu lako tu laonyesha kuwa wewe ni mojawao. Ni vizuri ujue kuwa kuna watanzania wengi tu ambao wamekataa toka siku nyingi tu kuhusishwa kwa namna yoyote na huu utawala dhalimu. Kwangu mimi kwa mfano uteuzi wowote ule wa JK nitauona kama tusi na sitachukua hata dakika moja kuufikiria. Najua mtaguna, nyie mlio tayari hata kulala makaburini kulilia hizo nafasi lakini kaa ukijua kuwa wapo wenye msimamo tofauti na mimi ni mojawapo.
 
P53 lingekuwa jambo la maana sana kama ungeongelea nafsi yako kwanza ingawa jibu lako tu laonyesha kuwa wewe ni mojawao. Ni vizuri ujue kuwa kuna watanzania wengi tu ambao wamekataa toka siku nyingi tu kuhusishwa kwa namna yoyote na huu utawala dhalimu. Kwangu mimi kwa mfano uteuzi wowote ule wa JK nitauona kama tusi na sitachukua hata dakika moja kuufikiria. Najua mtaguna, nyie mlio tayari hata kulala makaburini kulilia hizo nafasi lakini kaa ukijua kuwa wapo wenye msimamo tofauti na mimi ni mojawapo.
Mkuu ya kweli haya?... Je akikuteuwa kuwa mshauri wake vipi bado utakataa na kwa nini?...
 
Nita ipokea. Ndugu zangu kuna mambo mengi hapa ya kuwafanyia wananchi, mfano ni Magufuli alipopewa uwaziri alifanya mazuri sana lakini alipata shida pale jambo linapohitaji busara ya Rais wa nchi, tazama Lyatonga Mrema nae alijitahidi lakini jambo linalohitaji busara ya Rais linakuwa gumu. Kama tutawekwa katika nafasi ndani ya CCM nakuwatumikia wananchi tusikatae kwani tutaweza kuwaonesha njia watanzania wenzetu waliozoea ukitaka huduma serikalini lazima uende umevaa nguo ya kijani tena siku hizi wametoa zenye nembo ya ccm au JK. mimi nitawahudumia bila kujali vazi.
 
Mtu yeyote akiteuliwa na rais kushika madaraka bila shaka atayakubali isipokuwa rais mwenyewe hawezi kumteua mtu yeyote asiyekuwa mwanachama wa CCM kushika madaraka ya uongozi ngazi ya juu ya uongozi wa serikali kutokana na mfumo wa Kijamaa tulokuwa nao..

Mkuu ilikuwa ni mfumo wa chama kimoja uliopelekea watu kuchaguliwa kutoka TANU ama CCM na si kwa sababu ya mfumo wa kijamaa. Mfumo wa Serikali ya TANU na CCM ungelikuwa ni wa kibepari watu wangelichaguliwa hivyohivyo kwa mtindo uleule wa rais kuteua mtu kutoka kwa chama chake.

Toka enzi ya Mwalimu kiongozi yeyote alilazimika kujiunga na chama kwanza ili kupewa wadhifa wa juu serikalini au mashika ya Umma..Hivyo ni swala la kuuliza - Je, rais anaweza kumteua mtu kushika wadhifa serikalini au shirika la Umma hali mtu huyo ni Mpinzani wa siasa za chama CCM?

Ndiyo, rais anaweza kuteua mpinzani. Rais wa aina ya Mwalimu angeliweza kabisa kuteua mtu kutoka upinzani iwapo mtu huyo atakuwa muadilifu, si mnafiki, mwenye kuweka Taifa mbele kuliko chama chake, mchapaka kazi na mwenye uwezo unaohitajika.
 
Back
Top Bottom