Je, inawezekana kuongeza urefu wa mwili?

Simeone

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
672
623
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 20, ni mfupi nataka niongeze urefu wa mwili. Je, inawezekana!?

Msaada tafadhali.
 
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 20, ni mfupi nataka niongeze urefu wa mwili je, inawezekana!?
Msaada tafadhali.
Jua kabisa umri, uzito na kimo vinatakiwa viendane ili mwili uwe na balance na afya kikizidi kimoja kati hivyo ujue utapata shida Kiafya
 
😂😂😂 Imeisha hiyo mkuu. Labda ufuge nywele tu. Tiba pekee ni kujikubali tu mkuu ulivyo. Mengine ni kumuachia Mungu ufupi si kilema.

Kila mtu ana ubora kwa upande wake boresha kwenye kile kizuri ulichojaaliwa. Utakuwa na kitu mbadala cha kuoffer.

Mfano watu wafupi huwa hawatumainiki jijenge kuwa mtu wa kutumaika. Epuka kuwa mtu wa hasira hasira.

NB: Me nataka kupungua urefu wakuu.
 
Hahah mkuu haiwezekani. Kuna kipindi cha ukuaji nilikuwa natamani kuwa na kimo sawa na washkaji zangu ila ikawa ngumu. Zama za ubitozi zile kula Tshirt na bati mixa chini raba kali.

Niliwaza sana bila suluhu maana nilikuwa naona wenzangu wakigonga trouser zinanyooka bila kukunja miguuni hadi kunatana na kiatu ila mie mpaka nikunje kidogo!

That was a pain in the ass 🤣🤣🤣!!! Mwisho wa siku nilijikubali tu nilipogundua nawazidi akili na confidence so mie ndio nikawa ndio mtu wa kwanza wanaemtazama when it comes to serious issues! Pia nilikuwa mchangamfu na comedian sana. So watu wengi wananikubaligi.
 
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 20, ni mfupi nataka niongeze urefu wa mwili. Je, inawezekana!?
Msaada tafadhali.
Kipindi unambiwa ulale ukue ww hutaki upo busy na tv, haya tayari umepiga 20 mda wa kuota unakimbizwa umeisha saivi unaota mapenzi tu.

Pole sana subilia kunenepa tu,
 
Wakuu basi tu kama haiwezekani!

Profile picture yangu inayoonekana hapo ndo picha yangu.
 
Kipindi unambiwa ulale ukue ww hutaki upo busy na tv, haya tayari umepiga 20 mda wa kuota unakimbizwa umeisha saivi unaota mapenzi tuu.

Pole sana subilia kunenepa tu,
Mkuu kwahiyo sitaongezeka hata kidogo!?
 
Back
Top Bottom