Je, ilikuwa ni karamu ya risasi?

Je, ilikuwa ni karamu ya risasi?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,882
Reaction score
828,450
Kwamba zilikuwepo silaha mpya na wapigaji waliopewa kuzijaribu kwenye miili ya watu? Je ulikuwa ufundi, umahiri ama mashindano ya kulenga shabaha?

Je ilikuwa ni kamari ya kubashiri nani ataketekeza roho nyingi kwa wakati mmoja? Ama je kulikuwa na silaha zinzokaribia kuisha muda wake wa matumizi hivyo inabidi zitumike haraka kabla ya muda wake kutimia ili zisilete hasara?

Maana roho nyingi zisizo na hatia ziliteketea nje ya maandamano .. Ilikuwa kama mchezo wa kuwinda.. Watu waliviziwa mitaani na majumbani, vichochoroni na hata kwenye veranda za majumba
Ilikuwa ni killing spree..

Karamu ya risasi.. Na kwakweli hazikubagua maana hakuna kundi ambalo halina kilio mpaka sasa.. Zile risasi hazikumuacha yeyote salama..

Wale wapigaji sijui walipewa nini huko.. Maana walichojua ni kulenga na kufyatua.. Na shabaha zao zilikuwa zimenyooka mno.. Majeruhi kidogo vifo vingi😭

Kuna damu bado hazijakauka
Vidonda vingi bado vinavuja damu vingine usaha.. Kuna majereha yameanza kutoa harufu..

Kuna miili imeanza kutoa uvundo mkali
Ardhi ya Tanganyika imenajisiwa.. Damu inanuka kila kona..!
b8cac8d9-caf1-434f-9517-b2e9f800ad00.jpeg
 
Hapa alikuwa anatafutwa mmasai mmoja tu, dogo ana bahati sana mda wake haukuwa umefika. Three bullets aimed at one person, it was a mission to kill, kill innocent civilians, pedestrians, kids na hata miti maniner!!
20251108_111800.jpg
20251108_111835.jpg
20251108_111736.jpg
 
Kwamba zilikuwepo silaha mpya na wapigaji waliopewa kuzijaribu kwenye miili ya watu? Je ulikuwa ufundi, umahiri ama mashindano ya kulenga shabaha?

Je ilikuwa ni kamari ya kubashiri nani ataketekeza roho nyingi kwa wakati mmoja? Ama je kulikuwa na silaha zinzokaribia kuisha muda wake wa matumizi hivyo inabidi zitumike haraka kabla ya muda wake kutimia ili zisilete hasara?

Maana roho nyingi zisizo na hatia ziliteketea nje ya maandamano .. Ilikuwa kama mchezo wa kuwinda.. Watu waliviziwa mitaani na majumbani, vichochoroni na hata kwenye veranda za majumba
Ilikuwa ni killing spree..

Karamu ya risasi.. Na kwakweli hazikubagua maana hakuna kundi ambalo halina kilio mpaka sasa.. Zile risasi hazikumuacha yeyote salama..

Wale wapigaji sijui walipewa nini huko.. Maana walichojua ni kulenga na kufyatua.. Na shabaha zao zilikuwa zimenyooka mno.. Majeruhi kidogo vifo vingi😭

Kuna damu bado hazijakauka
Vidonda vingi bado vinavuja damu vingine usaha.. Kuna majereha yameanza kutoa harufu..

Kuna miili imeanza kutoa uvundo mkali
Ardhi ya Tanganyika imenajisiwa.. Damu inanuka kila kona..!View attachment 3498956
Mkuu, siyo wewe peke yako unajiuliza haya maswali. Mimi mpaka sasa nilikuwa siamini kuwa kuna watu wanaweza kuwa makatili namna hii. Kosa walilofanya wananchi (siwalaumu kwani hakuna aliyetarajia) ni kudhani kuwa hawa wauaji walikuwa mitaani kulinda usalama. Wananchi wangekuwa na clue ya nini ''askari'' wauaji wanafanya, basi wangewazingira, wawanyang'anye silaha na kuzitumia kujilinda. Wangekufa wachache lakini wangeua wauaji wote. Wajuzi wanasema ukitaka kupambana na mtu mwenye bunduki, kosa kubwa ni kukimbia na kumpa mgongo. Huwa wanasema unatakiwa ku-charge kwa haraka sana na ukifanikiwa kuishika silaha basi umepona. Hawa wauaji walikuwa wanatembea kwenye vikundi vya watu wachache ambao wananchi kwa umoja wao wangeweza kabisa kuwanyanganya bunduki na kujilinda.
 
Maeneo ya Kigogo...
Kuna nyumba Ina matundu 7 ya risasi....
Bahati nzuri hakuna madhara...
Jirani ndio Kuna madhara ya mtu kuvunjika bega...yupo Muhimbili...
Na ndugu wanahangaika atoke (maana walitonywa na wasamasia wema kwamba wakipata nafuu ni magereza Moja kwa Moja )maana majeruhi wengi wanaweza kufunguliwa kesi ya Uhaini ila walikuwa ndani ya nyumba
 
Yote haya yanetokea ili raia wa nchi jirani ya Zanzibar aendelee kuitawala Tanganyika, hakika CCM wametuuza Watanganyika utumwani Zanzibar . Hivi kweli CCM walikosa Mtanganyika mwanaume mwenye sifa ya kuwa Rais wa Tanganyika hadi watoe kafaraya damu za Watanganyika zaidi ya 10,000 ili Mzanzibari awe Rais wa Tanganyika ? Na mzee Kikwete damu hizi zitamlilia sana yeye na uzao wake wote vizazi hadi vizazi .
 
Zile risasi balaa, utoboaji ule wa kuta sio mchezo. Unashindwa kuelewa kwa nini utumia silaha nzito vile?
 
Back
Top Bottom