Je, huyu ni kahaba au mke?

Je, huyu ni kahaba au mke?

scatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,671
Reaction score
940
Wakuu habari ,

Kuna msichana nimeanzisha naye uhusiano kama yapata miezi minne imepita.Nimejaribu kumsoma lakini bado simuelewi. Mara ya kwanza aliniambia anakaa kwa wazazi tukaendelea na life mara zote tulikua tunakutana viwanja tu. Baada ya mwezi akaniambia amepata kazi hotelini mkoa mfulani nilifurahi nikamruhusu aende na nikampa na nauli ya kuendea huko.

Siku moja kulikua na mechi kubwa ya yanga na kwakuwa yeye nimshabiki wa Yanga jioni yake baada ya mechi yanga ilishinda ikibidi nimpigie simu kumpongeza, nilimtania nimekuona uwanjani alishituka sana na akaniambia yupo dar kazi ameacha.Tukatafutana tulipo onanana nimuuliza upo kwa nani sasa jibu lake anakaa na dada na kazi ameacha.

Tangu siku hiyo mpaka leo huyu mtu si muelewi ni wa mizinga kila siku haipiti siku bila kuniomba hela, simuelewi.

Naombeni ushauri
 
Sasa ushauri wa nn?jambo lakuamua sahihi unalijua ila hutaki kufanya.
 
Achana Nate kama anakuumiza akili.
 
Kwa nini kununua unachoweza pata bure kila saa, kila siku? 24/7/52? Mvutie ndani, ukiamka asubuhi unamwachia za mchana na jioni nawe ujitahidi kurudi mchana kula.
Amekuhakikishia kuwa anataka kuwa madame House. Umletee hapo nyumbani, nimeipenda hiyo kwani ameujua wajib wako na wajib wake.
 
Kama ulimpenda endelea kuwa naye karibu na kumchunguza kisha utafanya maamuzi mwenyewe,kama haeleweji na hataki umuelewe basi mwache.
 
Endelea kutafuta huyu wa kupoozea genye tu hana sifa za kuitwa mke na kama unacheza peku peku chukua tahadhari stahili kabla hujaatharika.

Natafuta mke
 
Mkuu nakupa usemi huu hakuna nyumba nzuri inayokosa mpangaji!
 
Kama ana tabia za kikahaba basi ujue ni kahaba
huwezi kukuta kuku ana tabia za bata...kwa vyovyote vile bata atakuwa na tabia za bata
na kuku atakua na tabia za kuku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom