Tatizo ni lipi haswa kwa huyu mwanamke?

juliusJr

Senior Member
Jul 14, 2016
180
61
Hello habarini wakuu.

Wasalaam

Ni mekua nashindwa kumwelewa uyu mtoto wa kike kwamba anahitaji nini hasa. Iko hivi wana JF ni takriban mwezi wa pili sasa nipo likizo dodoma baada ya mikasa ya COVID-19 kupamba moto mjini Dar sasa nina best angu mmoja nilisomaga nae advance hua anaishi huku Dom kwahiyo nilipata habari kwamba nae yupo Dom nijapanga niende nikamtembelee maana anaishi kwao bado. Basi nikapanga safari mpaka kwa huyo rafiki angu wa muda.

Bhasi kufika nilikutana na sura mpya pale walikuwepo wadada wawili wapya sijawahi kuwaona pale ila haikua kesi tukasilimiana nikauliza je mtu flani nimemkuta lakini mmoja wapo alikua mashalaah na alinivutia mno bhas uzuri kijana akawa pia amefika tukapiga story then tukaondoka na best angu. Ila sasa uwepo wa yule binti ulinivutia mno bhas ikawa haipiti siku sijaenda kwa yule rafiki angu nikajitaidi kujiweka karibu nae mpaka nikafanikiwa kupata namba yake japo haikua rahisi sana. Bhasi tukawa tunachati vizuri hata kabla sijamweleza lengo haswa ni lipi lakini the way alivokua ana act ninapochelewa kumjibu text as if tupo kwenye mahusiano kwahy ilo jambo lilinishangaza na nikajipa moyo jambo la kua na yeye halitakua gumu.

Hivo nikajikaza nikamueleza ila alinieleza history yake ya mahusiano kifupi na akadai kwamba nisimuumize kama wengine nikakubaliana nae na nikamuweka wazi tu kwamba baadhi ya vitu ambavo mimi sipendi especially pombe so akanikubalia na akasema yeye pia hanywi. Bhasi tukaingia kwenye mahusiano mimi na yeye ila mwanzoni ilinipa shida mno maana alikua na tabia ya kuongea na simu mno nyakati za usiku na kitu ambacho mimi sipendelei maana najua mchana kutwa anatingwa na kazi za nyumbani so usiku ni muda mzuri wa mimi kuzungumza nae ila sikutaka kumficha kwamba lile jambo silipendi nikamueleza tu ukweli kwa sababu nampenda na akadai atabadilika. Hivo tukaendelea tukawa tunakutana japo alikua anajiiba kwao.

Tukaendelea ivo ivo japo nikawa naskia tetesi kwamba ana mahusiano na watu wengine kama wawili hivi japo sikutilia maanani kivile ila nikamfata nikamuuliza ila akanibishia na akasema sio kweli ila niliridhika na majibu yake sasa kuna siku nikashika simu yake upepo wa kisuli suli ukanipeleka kwenye uwanja wa message nikakutana na charting zake na hao watu na hazikua nzuri za kufurahisha japo nikamuuliza pia baadhi ya maswali na akapaniki akasema mimi simuamini namuona malaya kiukweli kauli zile hazikunifurahisha ata kidogo.

Kumbe yote ayo tukipishana ana shosti wake anamwambia na ana mshauri baadhi ya mambo nikaja nikajua na ni baada ya kudukua tu simu yake pasipo yeye kujua. Bhasi nikasikia mengi mno anayomweleza rafiki ake tunapopishana mimi na yeye. Kuna siku nilimwambia naomba nikuweke status tu kama kumpima ila mwenzangu alinigomea bhas nikamzingua niweke mimi pia alikataa na akadai mahusiano ni yetu kwahiyo amna haja watu wengine kuyajua na ni mapema mno kufanya yote ayo nikajiuliza mno kwanini anakua msiri kiasi hiki na ataki watu ajue na nilivomuuliza yeye akasema ayo maisha yeye hajazoea yan daah nilichoka mno. Tukaendela na nikakubaliana na yeye japo nikimwambia jambo akikataa nakubali yanaisha na yeye akinambia jambo fulani hapendi bhas naacha yan inshort namskiliza.

Lakin yeye mambo yake ni yale yale sometimes anaweza kwambia anaenda sehemu fulani lakini ghafla akawa kimya na asikujibu kitu anpokua huko yan mpaka akirud ndo anakucheki na sababu kem kem kwamba hawezi kuchati anapokua sehemu fulani. Na jana tu tumepishana kisa tu maswala ya mazungumzo ya usiku maana nilimpigia ghafla akaanza sababu mara nipo kwenye kelele haniskii wakati nipo sehemu nzuri nikakata simu ile kumpigia tena anatumika nikasubiri mpaka akamaliza kumcheki akasema napenda mtafutia sababu za kugombana nae na kumuacha bhas nikamwambie yaishe nikawa natafakari asee nikakaa kama nusu saa ili nimpigie nimwambie yaishe asee nikakuta tena anatumika na trip hii ni kwa muda mrefu mno na baada ya kumaliza nikapiga na hakupokea na akanitumia message kwa kudai mimi nambana sana kama me simuamini nimuache na nimpe uhuru wake maana hapa tu sijamuoa lakina uhuru na simu yake je nikumuoa itakua.

Kwahiyo wadau em nielezeni nifanye nini nampenda kweli lakini mwenzangu haniskilizi kila ninalomweleza na pia ni mkali tunapopishana na wakati mwingine anatumia lugha kali mno japo nishamweleza yote na kiukweli nina mpango nioe mwakani kwa uwezo wa mwenyezi Mungu sasa jamani hii si changamoto wadau?
 
Kwani Dr christina Mauki umemshirikisha jambo lako pengine anaweza kukusaidia kukushauri
 
Kwani Dr christina Mauki umemshirikisha jambo lako pengine anaweza kukusaidia kukushauri
 
Kwani Dr christina Mauki umemshirikisha jambo lako pengine anaweza kukusaidia kukushauri
Daaah kiukweli huko sijafika kaka najua hata humu kuna watu labda wanapitia haya ninyaopitia mimi asee..... Maana mengine mpka nimeshinda kuyaandika mkuu
 
Umependa usipo pendeka! Endelea kujifunza kuhusu mapenzi maana bado unaonekana ni mgeni. Ukihitimu, utafahamu tu mwenyewe namna ya kutatua changamoto za aina hiyo.
 
Dahhhh kama mwanzo tu hivi umepitia yote hayo na bado unataka ushauri ? Acha kujipa mateso mkuu
Yan ndugu acha tu mwanamke hataki hata kuulizwa jambo sasa hivi aya mahusiano nikiingia nae kwenye ndo c tatizo nitakua najichimbia kaburi maan mzizi nimeshindwa kuukata mapema hivi anyway ni swala la muda tu kaka
 
Umependa usipo pendeka! Endelea kujifunza kuhusu mapenzi maana bado unaonekana ni mgeni. Ukihitimu, utafahamu tu mwenyewe namna ya kutatua changamoto za aina hiyo.
Mkuu daah sijui kama sioendwi lakini kiukweli uyu mwanamke ananipenda ila ana misimamo yake ya hovyo anataka kuishi kulingana na historia yake hataki kukubali wala kubadirika kwamba yupo kwenye mahusiano yan aishi kama ana mpenzi ndo shida maana me nataka kumuupgrade ila yeye ananionyesha vitu ambavo hata nashindwa kumuweka fungu gan
 
Mkuu daah sijui kama sioendwi lakini kiukweli uyu mwanamke ananipenda ila ana misimamo yake ya hovyo anataka kuishi kulingana na historia yake hataki kukubali wala kubadirika kwamba yupo kwenye mahusiano yan aishi kama ana mpenzi ndo shida maana me nataka kumuupgrade ila yeye ananionyesha vitu ambavo hata nashindwa kumuweka fungu gan

Sasa kama mnashindwana kwenye misimamo huoni tayari kuna tatizo hapo! Mwanaume usipokua na msimamo na ushawishi kwa mwanamke wako, ni dalili mbaya ya kuja kuwa 'mume bwege' siku za usoni.
 
Back
Top Bottom