Nakapanya
JF-Expert Member
- May 22, 2012
- 2,096
- 709
Kupitia taarifa ya habari ya ITV leo usiku,nimesikia mwenyekiti wa wazazi Tanzania Bw.Abdala Bulembo akiwahimiza wananchi wilayani Mbozi kupinga baadhi ya vifungu vilivyomo katika rasimu ya katiba.
Moja ya vitu alivyosema ni kuhusu serikali tatu kwamba itavunja muungano na kuwapa faida wenye maslahi na kuvunjika kwa muungano.
Lililonishtua zaidi ni kuhusu wakuu wa wilaya,mikoa,madiwani na serikali za mitaa.Anasema rasimu imefuta wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,serikal za mitaa na pia imefuta madiwani hivyo waipine kwani itazuia maendeleo ya nchi.
Sasa hoja yangu ipo hivi,rasimu inayjadiliwa hapa ni ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,hivo masuala ya wakuu wa mikoa,wilaya na madiwani na hata serikali za mitaa vitawekwa kwenye katiba za NCHI WASHIRIKA (Tanzania Bara na Zanzibar).
Sasa leo hii kiongozi wa juu kabisa wa chama anaposimama kwenye jukwaa kuwahutubia wananchi huku akiongea upotoshaji ni kadhia kubwa sana na inaonekana viongozi wengi hawajui wanachokiongea kuhusu rasimu hii hali inayopelekea upotoshaji mkubwa kwa wananchi.
Wanajamvi tulijadili hili ili hata kama mimi niliyoyaandika hapo ni upotofu ili tuzuie kupotosha jamii.
Nawasilisha.