Je, hizi fedha anazotoa Mhe. Rais zinatoka kwenye fungu gani?

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Leo nimeshuhudia kupitia luninga Mhe. Waziri Mkuu akihabarisha umma wa Watanzania kuwa Mhe. Rais ameridhia kutoa Tshs.300 billioni kwaajili ya ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali pale Dodoma ikiwa ni pamoja na Ikulu.

Sasa swali langu:- Bunge lina utaratibu wa kujadili bajeti na kuipitisha ili fedha hizi zitumike kama zilivyopangwa.Je hizi fedha anazotoa Mhe. Rais zinatoka kwenye fungu gani?.

Je zimepitishwa katika bajeti ya 2021/22?.

Nawasilisha.
 
Katiba yetu ni mbovu. Unakumbuka yule mungu-mtu aliyekufa kwa korona? Aliwahi kununua ndege bila hata kushauriana na mkewe. Aliamua mwenyewe na nafsi yake tu.
 
Ikiwa zinatumika kwa maendeleo ya kaya yetu haina jinsi acha itumike

Haina haja kugombania fito ilihali nyumba yakwetu sote
 
Back
Top Bottom