Je hili ni tatizo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je hili ni tatizo....

Discussion in 'JF Doctor' started by mkerwaji, Oct 4, 2012.

 1. mkerwaji

  mkerwaji Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Habari ndugu zangu wa jf....

  mimi nina swali kuhusu afya yangu....nikiwa kitato cha tano na cha sita miaka kumi iliyopita nilikuwa mwembamba sana kutokana na maisha ya shule lakini nilikuwa na kilo 80,...na baadae nikaenda chuo kikuu nikaishi miaka mitatu na kumaliza na kilo 90, na tangu mwaka 2006 mpaka leo navyoandika mail hii nina kilo 100,.....
  Lakini hazinipi shida yoyote,....nakimbia, nafanya kazi zangu vizuri tu na juzi nimetoka kupanda safu za milima uduzungwa kama kilometa tano na kushuka bila wasiwasi ...mpka mpira hacheza...lakini wananishauri eti nipunguze kilo zifikie atleast 80 kwa urefu wangu wa cm 180, je mnanishauri kupungua?....na nifanyaje ili nipungue manake nakula kawaida sana, chakula kidogo, na mazoezi nahudhuria....lakini pia kwa mimi sioni tatizo lolote mwilini....

  Naomba ushauri wenu......
   
 2. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Pole, ni hatari sana, we unaweza usiione hiyo hatari ni kwa sababu haiji kwa pamoja kwa siku, madhara yake utayaona baadaye kidogo kuanzia sasa. Kwa urefu wako wa cm 180, uzito wako wa juu kabisa unaopaswa kuwa nao ni kg 75, hii 75 ndiyo maximum yako na wala hutakiwi kuufikia, ili upumuwe vizuri na ujihakikishie miaka mingi mbele hakikisha unacheza kwenye 65 na 70.

  kazi ni kwako.
  jaribu kuongeza unywaji wako wa maji, bonyeza hapa: Jitibu kwa kutumia maji | maajabuyamaji.net
   
Loading...