Je hiki walichofanya CCM ni sahihi ?

Je hiki walichofanya CCM ni sahihi ?

Sales man

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2025
Posts
570
Reaction score
845
Hii ni sahihi?. Kuwavisha wanaCCM mavazi haya ili kupumbaza wananchi?
FB_IMG_17587250020926050.jpg
 
inategemea mkuu inaweka kua kweli au isiwe kweli

maana huwa tunaona viongozi wa dini wakiwa na ccm
 
Wenzako wako kwenye kampeni wewe unawapigia kelele.
Wana uchaguzi hao
 
Ccm hawana kosa hapo,
Wananchi wanaokubali kurubuniwa ndo matahira .
 
Hao masista wa ndolo ndanda wengi ni walewale kichwani,Turtizing huwezi kuwakuta hapo
 
Hii ni sahihi?. Kuwavisha wanaCCM mavazi haya ili kupumbaza wananchi?
View attachment 3478415
Hiyo taasisi iwapo inahitaji kutajirika wa wadai fidia baada ya kuwafungulia kesi kwenya mahakama ya kimataifa,na fidia yenyewe nawashauri wawe wanalipwa kila mwaka kwa miaka 1000.Wataacha mambo ya mchongo mchongo kuhadaa umma.
 
Hao masista wanafanya nini hapo mbona kama hii ishakua shida tena
 
Kwanini kanisa limeshikwa masikio sana na hii serikali. Natamani kwahaya yanayofanyika kanisa litutangazie kuwa waumini wake haeatashiriki kupiga kura mwaka huu.
 
Lengo na kilichofanyika ni vitu viwili tofauti.

Wito ulitolewa ghafla na haukuwa na madhara kwa maana waliitwa kwa lengo jingine kabisa lakini walivyofika wakaganizganga ngwa na sport light ya maana kuwa #Mama amefurahia sana uwepo wao kama wanawake wenzake ,kabla hawajahoji zaidi wakaambiwa waorodheshe majina maana kutakuwa na heshima ya viremba wakati hayo yanaendelea watu wa itifaki wakatimiza lengo la msingi , tafadhali tujiandae kupokea Mama ,kufumba na kufumbua wakajikuta tayari wanavitu mikononi na wapiga picture from no where wakiendelea na zoezi lao ,mwisho wa siku kilichofuata ni ITV.

Masister wa watu walikuwa well principled lakini wahuni ndiyo wakawaingiza kwenye 18 bila wao kujua .

Wanakuja kustuka game ishaisha kitaaambo.

Mama anajua kuwa hapendwi na hata zunguka yake ishatoka kwenye lengo la kutafuta kura , akifanyacho kwasasa nikutafuta matukio ya ushahidi kuwa aliungwa mkono na watu wa makundi yote , msisahau nawenyewe wanakuwaga na ugeni wao ambao wengi wao hawanaga muda wa kutisha wa kuyafuatilia ya mitandaoni so anajua wakiwa Ikulu na akifanikiwa kumuonyesha tu matukio katika picture then game over .

Anyway ......
ila CCM Mungu anawaona .
 
Inawezekana waka masista kweli mbona kanisa katoliki mpk sasa hawajasema kwamba siyo masista wao
Walikuwa ni masister kweli na wala siyo uwongo ,ila wamechezewa kinyamazongo na wahuni , yaani walichoitiwa ni tofauti na lengo la wahusika.

Kimsingi wao (Masister) tukio la wao kupigwa picture wakiwa wameshikilia vile makaratasi kwao hawakuwa wamelichukulia kwa uzito kiviiile bila kujua kwa CCM hilo ndilo lililokuwa lengo lao la msingi.
 
Hizi kampeni za ccm za mwaka huu ni kampeni hasa!, na hasa kwa mgombea urais wao. Kama kule kwenye vyama shikizi wanasapoti kampeni zao kufanya abrakadabra ionekane vile vyama vya kipuuzi navyo vina vibe kwenye kampeni why ccm yenyewe isijifanyie abrakadabra kwenye kampeni zake? Mikutano inajaa pomoni nyomi feki la kimagumashi ili tu ionekane wananchi wanaipenda ccm kwa moyo wote. Ni propaganda tupu kwa kwenda mbele, mambo ni mengi ya kuundwaundwa yanafanyika kuhadaa wananchi
 
Back
Top Bottom