je? Hii ni tamaa? Au Je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je? Hii ni tamaa? Au Je?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  likuwa 2009 nilipokuwa nyumbani Songea Ruvuma. Nilikuwa nimeenda kusuka kwa waMasai, sehemu ya kusukia ilikuwa nje tu. Tena barabarani kabisa au nisema kando ya barabara.

  Watu wakawa wanapita wa kila aina, bahati mbaya au nzuri akapita mwanadada mmoja ambaye ilionekana wamasai hao walikuwa wakimfahamu. Wakaanza kusema, he! Angalia mwanadada yule! Mmoja wao akawa anasema, miezi michache iliyopita alikuwa nusu kufa dada huyu, AMEATHIRIKA(VVU) na alikuwa amedhoofika sio mchezo. Lakini nasikia amepata dawa za kuongeza siku na sasa mwangalie alivyonawiri, mmmhh!

  Maongezi yakawa yanaendelea, lakini maongezi yenyewe yalikuwa yakiashiria tamaa ya kimwili walivyo wamasai wale kwa kummezea mate kimwana Yule. Muda wote nilikuwa kimya nikisikiliza maongezi yao. Mara wakawa wanaulizana wapi anaishi binti Yule, na lengo ilikuwa ni kutaka kumwendea na kujivinjari naye. Mwenzenu nikabaki mdomo wazi, mweh!!!
  Leo katika kuwaza kwangu ndipo mkasa huu au tukio hili likanipitia na ndio maana leo nimeona tutafakari pamoja. Je? Hii ni tamaa? Au Je? Ni kukosa kufikiri kwa makini? Maana wote walishajua kuwa ameathirika, sasa iweje wammezee mate ya kufanya naye tendo !!!?……
   
 2. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,503
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  yote yanawezekana may b alikuwa na ugonjwa mwingine
   
Loading...