je,hii ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je,hii ni sahihi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by fabinyo, Aug 12, 2012.

 1. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Habari zenyu wadau,long time sijatupia uzi ila leo ninao,tusaidiane!!
  Kuna binti rafiki yangu,tumefahamiana kitambo sana hivyo awapo na lolote huwa ananishirikisha,tunaishi mji mmoja!!aliisha olewa kipindi cha nyuma ila mungu kwa mipango yake hakumpa nafasi binti huyu kufurahia ndoa yake takatafu waliyoifunga kikatoliki,baada ya kama miezi 3 ya ndoa Mungu alimchukua mumewe kipenzi katika ajali mbaya ya gari akiwa safarini Mbeya kikazi,bila shaka wote tunapata picha hali aliyokuwa nayo binti huyu,siwezi kuielezea!!Hawakuwa na mtoto.
  Okey,miaka mitatu sasa imepita,mungu amempa uwezo wa kuyashinda maumivu,majonzi na upweke na sasa anahitaji kuendelea na maisha tena,amepata kijana ambaye wamependana kwa dhati,wanapanga kufunga ndoa,ishu inakuja katika pete zake za awali,tatu ukijumlisha na ya marehemu mume wake na zote anazivaa katika kidole chake,of course ni pete nzuri kwani ile ya ingejimenti ni ya gold na imenakishiwa na tanzanite(4 carats) na zile mbili ni white gold(3 grms kwa kila moja)
  Sasa anawaza,
  Je wakati ukifika ampatie huyo bwana mpya pete zote hizo ile wasinunue zingine na hatimae pete hizo hizo zijirudie katika vidole vyake na ile moja amvalishe mumewe siku ya ndoa?au huyo bwana anunue zingine?na kama akinunua zingine hizo za awali azifanyie nini?
  Tusaidiane mawazo ili mjumbe mimi nipate cha kumshauri,asanteni:spy:
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mbona hii hata mtoto wa nursery anajua jibu?

  pete za zamani zinawekwa kwenye droo

  mchumba mpya alete pete mpya....

  pete za gold na vito ni assets kwa wadada

  zina mikebe yake kabisaa

  kuvaliwa sio lazima akijisikia anavaa yoyote
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  anataka awowe kwa pate za mme wa zamani???

  Jamani, wanamme mbona uvivu wa kutoa hela umekuwa mkubwa hivi! !
   
 4. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  duh,sawa wadau hapo juu,nimewapata
   
 5. YETOOO

  YETOOO Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alete pete mpya za zamani auze atengeneze kitu kingine hata kidani sio mbaya,asiwe na mawazo ya kuanza kumdekeza huyo mchumba mpya ni wajibu wake kununua pete
   
 6. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Napenda kutoa ushauri wa bure kwa huyo mwanaume. Ni kheri kuoa mwanamke aliyeachika baada ya kudundwa sana na mwanaume hadi akajuta, kuliko kuoa mwanamke aliyefiwa na mwanaume ambaye alikuwa bado anampenda sana. Hii ni kwa kuwa kila mara mwanamke aliyefiwa atakuwa anaendelea kuwa na majonzi na kumbukumbu za marehemu wake, na hivyo kila tatizo dogo, atakuwa anamkumbuka marehemu wake, na kudhani kuwa kama mungu asingemchukua, basi tatizo hilo lisingemkuta. Atajaa simanzi hata raha ya ndoa haitakuwepo. Achana na wafiwa.
   
 7. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Hali ngumu Kongosho, mambo mengine inabidi mtuvumilie. Sasa kama hatuna hela tusioe?
   
 8. B

  Bibi yaga Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hajui cha kufanya, anipe mimi hiyo ya mumewe nimtunzie kama ukumbusho!
   
 9. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Peleka mawazo yako ya kijinga, hili Ndo uliloombwa ushauri? We Unataka Huyu aolewe na nani? Aisee jamaa achukue mzigo fresh, ila awe kidume anunue Pete Zake Mwenyewe!


   
 10. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hizo za zamani aziyeyushe atengeneze mkufu au hata hereni then avae hizo za mchumba wake mpya.Maana kuziweka kwenye droo siafiki inatakiwa azitengenezee vitu ambavo vitaendelea kuwa kumbu kumbu kwake so long as anahisi kufanya hivo hakumkwazi yeye mwenyewe na mumewe mtarajiwa. Otherwise kama atajiskia vibaya basi awauzuie masonara na ela itakayopatikana aitumie kwa kitu kingine au hata aitoe sadaka ya shukrani maana biblia inasema tushukuru kwa kila jambo
   
 11. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkuu kwa kuwa huenda yalisha kukuta, ila samahani kwa kutonesha donda, ingawa ukweli unabaki palepale. Mungu akuhurumie.
   
 12. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ndio maana nikaleta hili suala jukwaani,kila mtu na mawazo yake!lakini mwisho wa siku tutajua wazo lipi ni zuri zaidi
   
 13. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mhhh,labda nawewe unataka kumpelekea mwenzio
   
 14. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mhhh,sithani
   
 15. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  Mwambie rafiki yako pete za ndoa na za uchumba zinatambulisha wewe ni mke au mchumba wa huyo aliyekuvalisha so hakuna jinsi wala sababu na actually sio fair kwa mchumba mpya kuona unaendelea kuvaa pete za mume wake aliyefariki unless hayuko tayari kuanza rasmi mahusiano mengine mapya!anaweza akatafuta njia nyingine ya kumuenzi huyo mume marehemu lakini awe makini sana asije akajikuta anampa insecurity the new one!otherwise kila la kher na ndoa mpya SHE HAS TO KEEP ON LIVING!
   
 16. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  it sound gud,thanx
   
Loading...