Je hii ni haki kwa 'traffic police'?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu qna JF, mara nyingi nimekuwa nikijiuliza maswali mengi kuhusu utendaji kazi wa 'traffic police' wetu. Na kwa vile watu wengi hawajui sheria au kama wanajua hawajui namna ya kudai haki yao, hivyo hujikuta wakinyanyasika wanapokuwa wametenda kosa fulani au wakihisiwa wametenda kosa fulani.

Mfano, mara kadhaa nimekuwa nikiona 'traffic police' wakikamata gari (mfano dereva amepaki vibaya) basi 'traffic police' licha ya kumwambia dereva kuwa ametenda kosa na anapaswa aende kituoni, huanza kumwambia kufungua 'number plate' au yeye mwenyewe kufungua hiyo 'number plate' na kuondoka nayo. Je, hii imekaaje kisheria?

Pili siku moja niliona 'traffic police' akiendesha pikipiki bila helmet na alipofika sehemu fulani, aliona daladala ikipakia abiria kwenye route ambayo halikupangiwa. Basi yule 'traffic police', ambaye naye kavunja sheria za barabarani (kutovaa helmet) alimwamrisha yule dereva kutoa 'number plate' ili aichukue. Mimi nilibaki najiuliza maswali: Je, ingekuwa mimi ndiye dereva ningepaswa nifanye nini? Naomba ushauri ili hata ikitokea kwangu au kwa mtu mwingine niweze kumsaidia afanye nini.
 
Back
Top Bottom