Nini maana ya taarifa za Intelligencia zinazosemwa na Jeshi la Police?

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,685
3,549
Wakubwa shikamooni, Naomba Leo niwe mjinga kiwango Cha lami ya kutoka Iringa kwenda dodoma.

Leo hii tunashuhudia kesi mbali mbali zikiwa zinahitimishwa mahakani na watuhumiwa kuachiwa huru bila kukutwa na hatia, na majaji au mahakimu wakisema ushahidi umeshindikana kuletwa au kujitosheleza.

Swali langu: Je kutokana na matamko ya makamanda wakiwa wanatoa report za kihalifu baada ya watuhumiwa kukamatwa, na kusema kutokana na taarifa za kiintelijensia tumemkamata mtuhumiwa Fulani na kosa Fulani na ushahidi wa kitu fulani, Police wanajua taarifa za kiintelijensia na maana ya neno Intelligencia au hawajui?

Kwa ugumu wangu wa kutoelewa Mambo na Mimi huwa nafikiri taarifa za kiintelijensia ni taarifa ambazo zimetafutwa na watu mahiri wenye akili nyingi sana na zikachambuliwa kwa jina mpaka kufikia hatua ya kwenda kukamatwa mna full information ambao haina Shaka kabisa na ukitiwa hatiani hutoboi.

Je, Kulingana na taarifa za kiintelijensia kutokuwa na ushahidi hapa ni Nani mjinga na anakula hela za watanzania bure?

Je, Jeshi la Police linakosa uhalali wa kutumia neno Intelligencia?

Je, Police Tanzania wanajua taarifa za kiintelijensia zikoje ama hawajui?

Je, Waandaji wa hizi taarifa ni watu wasiokuwa inteligence?

Je! Tunawandaa watu vizuri kwenye hizi kazi au kila Askari anafaa Linda's taarifa hizi?

Ugumu wangu najiuliza maswali ya kijinga huku Sina majibu sahihi naomba Mungu atusaidie kujua.

IMG_20210627_213111.jpg
 
Karibuni mnisaidie ndugu zangu nipo najiuliza hili jengo walijengaje
IMG_20210627_173219.jpg
 
Back
Top Bottom