Pole kwa matatizo yaliyo kukuta japo ni ya kujitakia, kwenye thread yako unasema mmezaliwa watoto watatu (3), wa kike wawili na mmoja (wewe) wa kiume na kwa sasa una umri wa miaka 22 na Baba yenu alishatangulia mbele ya haki tangu ukiwa Form III. Tatizo kubwa nililoligundua kwako wewe umeshindwa kujikubali na sasa unatafuta huruma (Sympathy) kupitia watu mbali mbali badala ya kutumiza wajibu wako (Japo umekubali kosa).
Kwa umri ulionao ulitakiwa kutambua kuwa mama yako ni mjane na ujifunze kuhusu changamoto zinazowakabili wajane. Wewe kama mtoto pekee wa kiume ulitakiwa umsaidie mama yako kutatua changamoto na kero mbalimbali za kimaisha huku ukijikita vema katika masomo yako na kuachana na starehe za muda mfupi (Maana mshika mbili moja humponyoka).
Badala yake wewe ndiyo umeenda kuyazua kwa kuendekeza starehe za muda mfupi na kuzidi kumsababishia stress mama yako, halafu unasema eti ndilo kosa lako la kwanza (Siyo kweli). Unatwambia kuwa hapo nyumbani kwenu kumtuza huyo mkeo sijui mzazi mwezio hakuna shida wakati wewe hutoi chochote huoni kama huo mzigo wote ameubeba mama yako?
Kwa ufupi mama yako ANAKUPENDA kama mwanae (Amekusamee ndiyo maana amekubali kumpokea mkamwana na kumuhudumia) lakini anawaza vingi, na tatizo wewe ulilijua siku nyingi na kukaa kimya zimebaki siku chache ndo unasema. Hiyo fedha unayodai ulipiwe ada ndiyo hiyo ya kumtunza mwenzako na kulea hiyo mimba hatimae mtoto. KWA UFUPI WEWE NI BABA MTARAJIWA unatakiwa upambane nanma ya kustawisha familia yako siyo kukimbilia shule halafu msala unamuachia mama yako.
Ushauri wangu ni kuwa Hao Baba zako wadogo na shangazi (japo hukuwataja) kama kweli wana nia njema ya wewe kusoma waombe wachangishane fedha ya ada wewe urudi shule kuendelea na masomo na mama yako abakie na jukumu la kukulelea familia yako tu. (Maneno yao matupu bila vitendo hayasaidii). Kwa upande mwingine huo ni ukomavu UKIAMBIWA KUWA UYAONE NI PAMOJA NA HAYO. Matatizo ni sehemu ya maisha jikubali na USIKATE TAMAA. Wajibika Mama aishi.