Je, hii adhabu inanifaa?

Je, hii adhabu inanifaa?

Kila jambo na wakati wake kijana kuna wakati wa kutafuta maisha na wakati wa kuwa na familia lakini haina shida ajali kazini katika harakati za kupunguza nyege cha muhimu wewe usiende advance Bali uende chuo ili uwe unapata muda wa kutafuta Hela za wife na mtotooo kuwa na familia ni jukumu kubwa aiaeee

Hakika... Plan B ikishindikana itabidi nifanye ivyo...
 
MTOTO WA KWANzA TENA WA KIUME NA BADO UNAFANYA VITU VYA AJABU, YANI FORM 4 TU USHATIA MIMBA? MAMA YAKO YUKO SAHIHI, HATA MAGUFULI KASEMA HASOMESHI WAZAZI.
 
Hat ningekuwa mimi, nisingekusomesha. Siwezi kusomesha MZAZI. Ungekomalia shule na kuachana na mambo ya mademu
Raia Wa kawaida ukimuhukumu mtenda kosa aliyelijutia kosa lake wewe ndiyo unakosea zaidi
 
Fanya maamuzi ya kwenye pcha yatakufaaa,,, maana ulinogewa ukaacha focus yako,,,

Ila pole japo nyege ndo imekufanya hivo ungejua ungekua members wa CHAPUTA
 
Naona adhabu ya KUKATISHA MASOMO KISA MIMBA imefika ngazi ya familia
 
Si umesikia tamko la mkuu wa nchi basi usisumbue familia kunashughuli nyingi tu za kufanya achana na masomo wewe Lea familia yako
 
Mi ningekusomesha. Adhabu hiyo ni kubwa sababu mwisho wa siku mama yako inabidi ajue hakukomoi wewe tu,anajikomoa yeye akija kukuona miaka ya baadae umekuwa loser wakati alikuwa ana chance ya kukufanya uwe better. Kutia mtu mimba si mwisho wa maisha, huyo mtoto atazaliwa na atakuwa then what?
I wouldn't dare do that to my son. He will still go to school.
 
Dogo ingia kitaa anza kusaka hela
ujue wewe una mtoto tayari, unawaza kusoma una acha akulelee nan?

piga kaz ingiza pesa, utakuja kusoma ukiweka sawa familia yako. yaan mama yako nadhani yuko sahihi tu.
halaf pia kusoma siyo kufanikiwa, tafuta namna uingie kitaa upige kazi, ushakuwa mtu mzima sasa siyo unawaza kusomeshwa.
now waza baada ya miaka mi3 mwanao atahitaj kuanza shule itabid wewe ndio umsomeshe.
pambana na hali yako
 
Pole kwa matatizo yaliyo kukuta japo ni ya kujitakia, kwenye thread yako unasema mmezaliwa watoto watatu (3), wa kike wawili na mmoja (wewe) wa kiume na kwa sasa una umri wa miaka 22 na Baba yenu alishatangulia mbele ya haki tangu ukiwa Form III. Tatizo kubwa nililoligundua kwako wewe umeshindwa kujikubali na sasa unatafuta huruma (Sympathy) kupitia watu mbali mbali badala ya kutumiza wajibu wako (Japo umekubali kosa).

Kwa umri ulionao ulitakiwa kutambua kuwa mama yako ni mjane na ujifunze kuhusu changamoto zinazowakabili wajane. Wewe kama mtoto pekee wa kiume ulitakiwa umsaidie mama yako kutatua changamoto na kero mbalimbali za kimaisha huku ukijikita vema katika masomo yako na kuachana na starehe za muda mfupi (Maana mshika mbili moja humponyoka).

Badala yake wewe ndiyo umeenda kuyazua kwa kuendekeza starehe za muda mfupi na kuzidi kumsababishia stress mama yako, halafu unasema eti ndilo kosa lako la kwanza (Siyo kweli). Unatwambia kuwa hapo nyumbani kwenu kumtuza huyo mkeo sijui mzazi mwezio hakuna shida wakati wewe hutoi chochote huoni kama huo mzigo wote ameubeba mama yako?

Kwa ufupi mama yako ANAKUPENDA kama mwanae (Amekusamee ndiyo maana amekubali kumpokea mkamwana na kumuhudumia) lakini anawaza vingi, na tatizo wewe ulilijua siku nyingi na kukaa kimya zimebaki siku chache ndo unasema. Hiyo fedha unayodai ulipiwe ada ndiyo hiyo ya kumtunza mwenzako na kulea hiyo mimba hatimae mtoto. KWA UFUPI WEWE NI BABA MTARAJIWA unatakiwa upambane nanma ya kustawisha familia yako siyo kukimbilia shule halafu msala unamuachia mama yako.

Ushauri wangu ni kuwa Hao Baba zako wadogo na shangazi (japo hukuwataja) kama kweli wana nia njema ya wewe kusoma waombe wachangishane fedha ya ada wewe urudi shule kuendelea na masomo na mama yako abakie na jukumu la kukulelea familia yako tu. (Maneno yao matupu bila vitendo hayasaidii). Kwa upande mwingine huo ni ukomavu UKIAMBIWA KUWA UYAONE NI PAMOJA NA HAYO. Matatizo ni sehemu ya maisha jikubali na USIKATE TAMAA. Wajibika Mama aishi.
Mkuu umemshaur vizur sana.. Hongera kwa maneno yako ya busara... Iwe funzo kwa hawa vijana wetu wanaoendekeza mapenzi
 
Back
Top Bottom