Je, HESLB imepunguza mikopo kwa wanaoendelea?

Je, HESLB imepunguza mikopo kwa wanaoendelea?

DVC

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2019
Posts
219
Reaction score
215
Habari wakubwa,

Kuna suala linasemekana linaendelea vyuoni hivi sasa. Ada au mkopo kwa wanafunzi umepunguzwa kwa kiwango fulani. Mfano, kama ulikuwa na 100% basi utakuta 70% au chini ya hapo.

Swali ni je, hili swala mbona kama hawa wakubwa wamefanya kimya kimya bila ya public notes? Au labda hili suala halina haja ya wahusika kuambiwa kabla?

Wajuzi embu tupeni uelewa.

Jioni njema!
 
Duuuuu! kama hii ni kweli ni hatari. Ila ile hela ni tamu asee,
ndiyo upewe yote sasa.

aloooo! Baada ya kumaliza nikapigika kitaa nilijutia sana ule mzigo.
 
mnasaidiwa na bado mnataka kuwapangia! na bado mtagoma kulipa hizo pesa.
 
Aaron Arsenal, Usibishe mkuu, waulize walioko vyuoni huko mtaani kwako, hata DARUSO Waziri wao Mikopo katoa tamko
 
mnasaidiwa na bado mnataka kuwapangia.! na bado ntagoma kulipa hizo pesa.
Ule sio msaada mkuu, ndio maana unasaini mkataba wa kurejesha sasa kama fedha inarudi na riba, kwanini unaona watu wanasaidiwa? Fika chuo uone hali ilivyo.
 
Leta uthibitisho

Siasa za majitaka waachie upinzani
Pitia hiyo

Screenshot_20191106-071547.jpeg
 
Aaron Arsenal,
Acha ubishi mkuu zaidi ya 80% ya wanufaika ambao ni continuous wamepunguziwa pesa za ada pamoja na zile za matumizi...binafsi mdogo wangu pia ni mhanga wa kadhia hii. yeye alikuwa analipiwa 1.5m per year ila wameipunguza hadi laki 9 bila kutoa taarifa.
 
mnasaidiwa na bado mnataka kuwapangia.! na bado ntagoma kulipa hizo pesa.
Umeishia darasa la ngapi wewe jamaa?😂😂😂 kwa mtu ambaye amepitia maisha ya University hawezi kuwa akili kama hizo zako. Mkopo sio msaada bali ni mkataba kati mkopeshwaji na taasisi inayokopesha. Mabadiliko yoyote lazima yahusishe pande zote mbili kwa sababu kufanya kinyume na hapo ni kwenda kinyume na mkataba.

Be updated young man.
 
Aisee n kweli ila awajafanya haki sasa iyo ela mtu anatoa wap.
 
Ni kweli wamepunguza bila taarifa
 
Umeishia darasa la ngapi wewe jamaa?[emoji23][emoji23][emoji23] kwa mtu ambaye amepitia maisha ya University hawezi kuwa akili kama hizo zako. Mkopo sio msaada bali ni mkataba kati mkopeshwaji na taasisi inayokopesha. Mabadiliko yoyote lazima yahusishe pande zote mbili kwa sababu kufanya kinyume na hapo ni kwenda kinyume na mkataba.

Be updated young man.
Huyo ndio yule wa la saba B.
 
Habari wakubwa,

Kuna suala linasemekana linaendelea vyuoni hivi sasa. Ada au mkopo kwa wanafunzi umepunguzwa kwa kiwango fulani. Mfano, kama ulikuwa na 100% basi utakuta 70% au chini ya hapo.

Swali ni je, hili swala mbona kama hawa wakubwa wamefanya kimya kimya bila ya public notes? Au labda hili suala halina haja ya wahusika kuambiwa kabla?

Wajuzi embu tupeni uelewa.

Jioni njema!
Hawa wanazingua Mimi wameniondolea books and stationery
 
[QUOTEvi Mmoja, post: 33394181, member: 557355"]
Alikuwa chuo gani ?
[/QUOTE]
vyou karibia vyote kuna jamaa yangu yupo DUCE pia kanambia hvyo
 
Back
Top Bottom