Je, Hayati Dr. Remmy aliunga mkono rushwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Hayati Dr. Remmy aliunga mkono rushwa?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mtu Mmoja, Dec 14, 2010.

 1. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  najua mmewahi kusikia sehemu ya wimbo maarufu wa Dr Remmy uitwao "Kifo" isemayo ".... kifo ungeonekana ungekuwa tajiri sana..... kifo tungekupa rushwa, kusudi tuishi milele...."

  je, kwa hapo tunaweza kuhitimisha kuwa

  1. mwanamuziki huyu aliunga mkono rushwa?

  2. alikuwa muumini wa dhana za machieveli kwamba kwa kuwa rushwa huleta utajiri, basi, "the end justifies the means"?

  RIP ramadhani mtoro ongala aka Dr Remmy
   
 2. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Mtu Mmoja, malembe malembe moninga na ngai. Huwezi kungoja hadi baada ya mazishi au arobaini ipite, aisee?
   
 3. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  haya ngoja ningoje hiyo arobaini. thanks
   
 4. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  nimekusikia mkuu na kwa hiyo nakushukuru. sababu ya kulalamika kwangu inatokana na kujuana na marehemu tangu mwisho wa 70's.
   
 5. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Napenda sana nyimbo za remmy (ninazo kadhaa kwenye Ipod yangu). Ukisilikiza nyimbo zake utagundua Remmy alipenda sana kuwawakilisha "multiple themes" katika wimbo mmoja, kwenye huo wa kifo hapo alipogusia rushwa, alikuwa anaonyesha hali halisi ya jamii yetu ambapo Rushwa ilishakuwa imekubalika kwenye jamii kama kiungo cha kulainisha sehemu zote zisizopitika kwa uhalali (au haki), lakini påia Remmy anaonyesha kwa upande mwingine kuwa jamii itambue kuwa Rushwa sio kila kitu, siyo kila mara "Rupia" itaondoa udhia, kwa mfano kifo, hata uwe tajiri vipi, kuna siku tutakuzika tu.  Ni meseji nzuri kwa mafisadi, hata watuibie rasilimali zetu zote, hawataenda nazo kaburini, tutawazika (kama watakufa kabla yetu) na mali wataziacha hapa duniani. Remmy anatukumbusha tuishi maisha mema duniani kwani kuna siku tutafika mwisho.  RIP Dr. Remmy. Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Roho ya marehemu ipumzike kwa amani, Amen!  NB. Nafurahi zaidi kwakuwa Remmy amefariki huku akiwa amemkiri Yesu kristo kama bwana na Mwokozi wake, na kwakuwa Biblia inasema hakuna atakayemwona Baba bila kupitia kwa Mwana (Yesu), naamini kwa sasa Remmy amewekwa kuume kwa Baba akisubiri karamu takatifu na watakatifu wengine wa Mungu. Amen!
   
 6. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kabla ya mauti kumkuta alimpa yesu maisha yake na historia yake ilikwisha badilika.r.i.p remmy
   
Loading...