Je, Hayati Dr. Remmy aliunga mkono rushwa?

Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Mar 18, 2010
593
64
najua mmewahi kusikia sehemu ya wimbo maarufu wa Dr Remmy uitwao "Kifo" isemayo ".... kifo ungeonekana ungekuwa tajiri sana..... kifo tungekupa rushwa, kusudi tuishi milele...."

je, kwa hapo tunaweza kuhitimisha kuwa

1. mwanamuziki huyu aliunga mkono rushwa?

2. alikuwa muumini wa dhana za machieveli kwamba kwa kuwa rushwa huleta utajiri, basi, "the end justifies the means"?

RIP ramadhani mtoro ongala aka Dr Remmy
 
Mtu Mmoja, malembe malembe moninga na ngai. Huwezi kungoja hadi baada ya mazishi au arobaini ipite, aisee?
 
nimekusikia mkuu na kwa hiyo nakushukuru. sababu ya kulalamika kwangu inatokana na kujuana na marehemu tangu mwisho wa 70's.
 
najua mmewahi kusikia sehemu ya wimbo maarufu wa Dr Remmy uitwao "Kifo" isemayo ".... kifo ungeonekana ungekuwa tajiri sana..... kifo tungekupa rushwa, kusudi tuishi milele...."

je, kwa hapo tunaweza kuhitimisha kuwa

1. mwanamuziki huyu aliunga mkono rushwa?

2. alikuwa muumini wa dhana za machieveli kwamba kwa kuwa rushwa huleta utajiri, basi, "the end justifies the means"?

RIP ramadhani mtoro ongala aka Dr Remmy

Napenda sana nyimbo za remmy (ninazo kadhaa kwenye Ipod yangu). Ukisilikiza nyimbo zake utagundua Remmy alipenda sana kuwawakilisha "multiple themes" katika wimbo mmoja, kwenye huo wa kifo hapo alipogusia rushwa, alikuwa anaonyesha hali halisi ya jamii yetu ambapo Rushwa ilishakuwa imekubalika kwenye jamii kama kiungo cha kulainisha sehemu zote zisizopitika kwa uhalali (au haki), lakini påia Remmy anaonyesha kwa upande mwingine kuwa jamii itambue kuwa Rushwa sio kila kitu, siyo kila mara "Rupia" itaondoa udhia, kwa mfano kifo, hata uwe tajiri vipi, kuna siku tutakuzika tu.



Ni meseji nzuri kwa mafisadi, hata watuibie rasilimali zetu zote, hawataenda nazo kaburini, tutawazika (kama watakufa kabla yetu) na mali wataziacha hapa duniani. Remmy anatukumbusha tuishi maisha mema duniani kwani kuna siku tutafika mwisho.



RIP Dr. Remmy. Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Roho ya marehemu ipumzike kwa amani, Amen!



NB. Nafurahi zaidi kwakuwa Remmy amefariki huku akiwa amemkiri Yesu kristo kama bwana na Mwokozi wake, na kwakuwa Biblia inasema hakuna atakayemwona Baba bila kupitia kwa Mwana (Yesu), naamini kwa sasa Remmy amewekwa kuume kwa Baba akisubiri karamu takatifu na watakatifu wengine wa Mungu. Amen!
 
Kabla ya mauti kumkuta alimpa yesu maisha yake na historia yake ilikwisha badilika.r.i.p remmy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom