Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,386
Lipo kundi la vijana la propaganda mitandaonu lililotumwa maalum kubeza, kukejeli na kufubaza harakati zote za ukombozi wa Tanganyika zinazoongozwa na Gen Z
Hili ni kundi mchanganyiko lenye uelewa na maslahi tofauti kwenye hali tuliyo nayo
Wapo wafaidikaji wakuu na wenye maslahi ya moja kwa moja na wapo fukara wanaoambulia makombo. Ambao wao kwa ujira usiozidi million moja kwa mwezi wako tayari kufanya chochote kile hata kama kitadhalilisha utu wao
Ni wazi hatuwezi kufanana kwenye kila kitu, kuanzia imani mpaka itikadi.. Lakini kwenye kila kitu kuna mambo ya msingi ambayo hayazingatii imani wala itikadi.. Hayo yapo na yanajitegemea na mojawapo ni HAKI ya kuishi na UHURU wa kutoa maoni bila kuvunja katiba
Mfumo wenye makandokando mengi na tuhuma za kila aina unajitahidi kwa kila njia kujinasua na kujisafisha mbele ya watu na jumuiya za kimataifa
Hilo ni jambo la kawaida popote kwakuwa kuna kundi faidika kati yao na linajua wazi kwamba mambo yakienda mrama nao watayumba na kuwa sehemu ya uwajibikaji
Kwenye shida yoyote iwe kubwa ama ndogo jifunze kutulia.. Ukipaniki tuu.. Umejimaliza kwa bei poa kabisa, mbaya zaidi unaweza kusababisha madhara hata kwa wasiohusika
Kwenye medani za vita kila silaha ni muhimu kwa ajili ya ushindi, lakini haziwezi kutumika zote kwa wakati mmoja.. Kuna silaha za mkakati na kuna silaha kulingana na mazingira
Vijana waliotumwa mitandaoni kuwashambulia wote wanaotaka mambo yarekebishwe kwa manufaa ya taifa zima
Wengi hawajaandaliwa vema
Wengi no tiamajitiamaji
Wengi wana stress mbalimbali za maisha,kuanzia kipato mpaka ajira
Wengi wana uono na maono kimo cha mbilikimo kwenye hoja na tafakuri muhimu
Wengi hawana uwezo wa kujibu hoja bali hujibu viroja
Wengi ni wahitimu waliosoma lakini hawakuelimika.. Ni wahitimu janjajanja
Hawa ni tofauti kabisa na kundi la vijana wenzao wapigania haki kwa wore
Wamesoma na kuelimika
Wamefaulu kwa haki
Wana maono makubwa na mazuri
Hoja zao zina mashiko
Wanajitolea hawalipwi
Wanapambania kesho bora ya wote na si ya kikundi faidika cha watu wachache
Wana mbinu, wana mikakati na hoja zinazielezeka
Kama ukifanya tathmini ya siku na ya mwezi kundi hili la pili linajizolea point nyingi kila wakati! Na kila siku ipitayo wanasonga hatua moja mbele.. Maana wamejitambua na wanajielewa wanataka nini na kwa faida ya nani
.ndugu zao wa upande wa pili wao hawana mikakati, hawana hoja hawana akili.. Wao kazi yao ni vijembe, kejeli matusi uzushi uongo na uzandiki.. Na malipo yanapocheleweshwa utajua tuu
Kuna wakati wasilaumiwe Sana.. Maana wanatumikia tumbo. Na hakuna kitu kibaya kama njaa.. Aliyesema adui yako muombee njaa aliwaza jambo kubwa Sana..
Hawa hawajui ya kuwa kinachopiganiwa kina maslahi na faida kwao pia! Kazi ya ujira mwisho wake ni kutupwa.. Je mabadiliko tarajiwa yatakapotokea wataweka wali nyuso zao;?
View: https://www.facebook.com/share/v/1DimGudiwx/