Je hawa Mbwa hawapatikani Tz? Kwanini Germany Shepherd ndio maarufu ukiacha hawa wa kwetu?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
14,952
Reaction score
34,958
Wakuu,
Kwanini hizi aina nyingine za Mbwa hatuoni zikitangazwa sana hapa Tanzaniaa zaidi ya German Shepherd
Je upatikanaji wake ni mgumu au ndio watanzania wamekariri tu?
1.Golden Retriever
2.Labrador Retriever
3.Husky

Sifa zao
1.Ni salama na rafiki kuishi na familia hasa watoto.
2.Wana uelewa wa juu na rahisi kufundishika
3.Ni wapole na wanapenda kuwa karibu na watu(social dogs)
4.Wanafaa kwa ulinzi wa wastani

Najua kuna aina nyingi za Mbwa lakini nimeamua kuweka hawa maana naona wana Sifa zinazokaribiana sana.

Naomba ufafanuzi wataalamu
Asante.

Untitled_design-40.jpg

Golden Retriever 1
images (2).jpeg

Golden Retriever 2
images (1).jpeg

Labrador 1
images.jpeg
Labrador 2
9cade9c3-7a1e-4644-8694-fcdd7a2b20db___.webp

Husky dog
Husky-Dog.webp

JAA_3538-2.jpg

German_Shepherd_-_DSC_0346_(10096362833).jpg

Germany Shepherd
 
Wanapatikana ndio lakini kwa ugumu kidogo na wengine mpaka ukafwate Kenya. GSD amekuwa na mapokeo makubwa kwa wafuga Mbwa na kwakuwa huwa anatumika hata kwenye majeshi yetu, lakini kuna ambao hata umewataja hapo nao ni wazuri sana na kuna baadhi ya vitu wana mpita GSD.
GSD amekuwa na mapokeo makubwa tu kwa wafugaji kuliko kuangalia aina ya Mbwa na malengo ya kuwafugia.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri, kumbe shida unaweza ikwa ni upatikanaji wake tu,Hivi GS ukiwaacha huru na watoto wanakua salama kweli?
 
Kwa mfano kuna huyu Mbwa anaitwa st bernard ni mzuri sana kwa uelewa wake lakini umbo lake ni likubwa na halina mvuto kama GSD , na niwachache sana hapa nchini kwakuwa wengi wamempokea zaidi GSD, tena wana penda GSD awe Show line hawapendi walking line, wakati ukiwachunguza wana utendaji tofauti kutokana na maumbile yao.
 
Hawana shida kabisa ni marafiki sana na wanadamu, lakini pia huwa inategemeana na wewe mfugaji utakavyo muhifadhi na kumtunza Mbwa wako, mfano watu wengi wanazania Mbwa akiwa anabweka sana akiwa bandani ni ukali kumbe hapana nao huwa wanapata stress za kufungiwa mno, kwahiyo ni njia gani utazitumia kumtoa ktk hali hiyo itakutegemea wewe mfugaji kwa jisni utakavyo mfuga na kumwongoza. Kanuni kuu ya Mbwa ni kumtii kiongozi wake.
 
Ngoja nitafute nimuone, Nadhani pia Watanzania wanafunga Mbwa bila malengo ndio maana mtu anafunga Mbwa badae wanashambulia familia yake au yeye mwenyewe, wakati unaweza kufuga mbwa ambae yupo friendly lakini anakua alert dog kwamba anaweza kukustua kama kuna wezi au watu wasiofahamika
 
😀😀Asante hapo nimekupata
 
Watanzania wengi wafuga mbwa huwa ni wapuuzi sana, unakuta Mbwa anafungiwa bandani siku mzima au yuko na mnyororo/kamba shingoni anafungiwa mahali kila siku mchana wote halafu anafunguliwa usiku tu.
 
Ngoja nitafute nimuone, Nadhani pia Watanzania wanafunga Mbwa bila malengo ndio maana mtu anafunga Mbwa badae wanashambulia familia yake au yeye mwenyewe, wakati unaweza kufuga mbwa ambae yupo friendly lakini anakua alert dog kwamba anaweza kukustua kama kuna wezi au watu wasiofahamika
Karibu sana nitakusaidi hitaji lako juu ya ufugaji wa Mbwa, upatikanaji wa mbegu bora,wakufunzi wa mbwa, vet bora wa Mbwa na vyakula na vifaa vya Mbwa.
 
Watanzania wengi wafuga mbuwa huwa ni wapuuzi sana, unakuta Mbwa anafungiwa bandani siku mzima au yuko na mnyororo/kamba shingoni anafungiwa mahali kila siku mchana wote halafu anafunguliwa usiku tu.
Ni kweli ulisemalo kikbwa sasa ni kueleimishana pole pole kwa hekima na busara ili wote tufikie malengo yetu na ufugaji bora na kuwa na Mbwa bora.
 
Ukiwa mfugaji wa mbwa kibiashara utaelewa kwanini wafugaji hawaentertain aina nyingine za mbwa zaidi ya German Shepherd, Rottweiler, Boer Boel (and) Maltese (pia) kwa uchache Belgian Malinois na Doberman Pinscher.

BTW iko hivyo kwa sababu, an intelligent seller keep what the market demand.
 
Sio breed zote, kuna Zingine ni hatari sana
Ni kweli Mbwa wote ni wakali ila kila Mbwa ana miongozo yake ya jinsi ya kumfuga na kumfundisha, nasisitiza sana Mbwa ni wanyama kwahiyo wanategemeana sana na wewe unataka kumfuga vipi, hata Rottweler unaweza kumtengua akili toka mwanzo akawa zuzu au unaweza mtengeneza vibaya asisikilize hata anae mfuga, na hapo ndipo inakuja hadisi ya kuwa hawa huwa hawafai kuwa karibu na wanadamu.
 
Watanzania wengi wafuga mbuwa huwa ni wapuuzi sana, unakuta Mbwa anafungiwa bandani siku mzima au yuko na mnyororo/kamba shingoni anafungiwa mahali kila siku mchana wote halafu anafunguliwa usiku tu.
🤣🤣, halafu akimfungilia yeye mwenyewe anakimbilia ndani, nishaona watu kibao eti anatembea na Mbwa wake barabarani na mnyororo cha kushangaza Mbwa ndio anamvuta mbele, yaani Mbwa anakula ndio leader wakati Mbwa anatakiwa akufuate wewe au muwe sambamba na ukitoa amri anakutii, ukisema simama anasimamia.
 
Back
Top Bottom