Je hatuwezi badiri wimbo wa Taifa?

Je hatuwezi badiri wimbo wa Taifa?

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Naleta tena hoja hii hapa jukwaani, nimekuwa nikifuatilia mashindano yanayoendelea huko Misri Timu nyingi nyimbo zao zinapoimbwa hatusikii neno Africa mwanzoni bali ni nyimbo zinazochochea ari na shauku ya kupambania Mataifa yao.!

Kwanini wimbo wetu unaanza na kuibariki Afrika ? Badala ya Tanzania, kila mara tunajiweka sisi nafasi ya pili badala ya mwanzo je hili linawezaje jenga hali ya Uzalendo, ?
Yamkini hata Mungu huko aliko anatushangaa tunaomba abariki kwanza Africa kisha atubariki sisi na sio atubariki sisi kisha Africa! Zambia wana wimbo wenye tune kama yetu lakini sidhani kama wanaanza na Neno Africa bila shaka wanaanza na Zambia.

Wakati umefika wa kuendesha campain ya kubadiri wimbo wetu wa Taifa.
Nawasilisha..
 
Haaaaaahaaaaa kweli asee tunaiombea dua mijitu isiyotuhusu inaishia kutufunga tu!
 
Kama kuna mtu anaweza kuwa na uelewa wa jinsi ya kufikisha hii hoja bungeni anisaidie jinsi ya kuweza kuifikisha sina ukaribu na Mbunge wangu koka sabbu kwanza hata Bungeni sijawahi sikia akichangia chochote, je kwaweza kuwa na utaratibu mwingine wowote?..
Et wimbo una ubeti wakwanza na wapili!!!!
 
Tuache porojo,hatuna quality players, nchi yetu haina msingi wa soka,wachezaji wote waliopo Afcon hawazidi watano waliowawahi pitia academy,mpira siyo Siasa ni science
 
Naleta tena hoja hii hapa jukwaani, nimekuwa nikifuatilia mashindano yanayoendelea huko Misri Timu nyingi nyimbo zao zinapoimbwa hatusikii neno Africa mwanzoni bali ni nyimbo zinazochochea ari na shauku ya kupambania Mataifa yao.!

Kwanini wimbo wetu unaanza na kuibariki Afrika ? Badala ya Tanzania, kila mara tunajiweka sisi nafasi ya pili badala ya mwanzo je hili linawezaje jenga hali ya Uzalendo, ?
Yamkini hata Mungu huko aliko anatushangaa tunaomba abariki kwanza Africa kisha atubariki sisi na sio atubariki sisi kisha Africa! Zambia wana wimbo wenye tune kama yetu lakini sidhani kama wanaanza na Neno Africa bila shaka wanaanza na Zambia.

Wakati umefika wa kuendesha campain ya kubadiri wimbo wetu wa Taifa.
Nawasilisha..
Kiasili Tanzania sio nchi ya wabinafsi kwa kuzingatia misingi aliyotuachia haya Baba wa Taifa. Ukifuatilia kiasili kabla ya Berlin Conference ( 1884-1885) Africa ilikuwa ni moja na hakukuwa na mgawanyo wa Mipaka hii tuliyo nayo sasa hivi.
Hvy ss kama Taifa tunathamini umoja wetu wa asili kwa kuamini Africa ni moja, na hii mipaka ya nchi si kwa mapenzi yetu waafrica bali ni kwa maslahi ya tawala za kikoloni za wakati huo.
Hvy kuanza kwa kuitaja kwanza Africa katika wimbo wa Taifa tunaamini katika Umoja wetu kama Africa na Tanzania katika ubeti wa pili ni kwamba msingi wa utanzania wetu ni uafrica wetu.
Rejea katika katiba yetu bado inatamka sisi ni Taifa la kijamaa, kwahy sera ya Ujamaa inaamini zaidi katika maslahi ya Umoja wetu kwanza kabla ya maslahi binafsi.
 
Back
Top Bottom