God knows
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 276
- 173
Mwanzoni mwa mwezi wa Sita, 2014 niliingia kwenye website ya zoomtanzania.com
Katika tembea tembea zangu, nikakutana na tangazo hili la internship kutoka African Barick Gold. Lilikuwa linasomeka kama hivi:

Kwa sababu nilikuwa katika mchakato wa kutafuta nafasi za field, nilituma barua ya maombi. Baada ya wiki kama 2, nilipokea e-mail ifuatayo:

Baada ya kupata email hiyo, leo nimepokea ujumbe ufuatao kwenye simu yangu kutoka kwenye namba ya Mr. Bryson Kagenzi:
+255759352328: Ndugu, naendelea kufanya selection ktk nafasi za internship & field practice/ABG.so far zimebaki nafasi 9 tu, tusaidiane kitu, unitumie laki 1.5 then mm ntakupitisha ktk hizi nafasi, nakushauri usiache maana kw baadae wanalenga kutoa mikataba y kurudi kufanya kazi, after graduading unasemaje?
Nilipousoma ujumbe huo, sikuujibu.
Nikajaribu kutuma hela kwa kupitia M-pesa ili niangalie usajili, nikakuta hiyo namba imesajiliwa kwa jina hilo hilo la Bryson Kagenzi.
Baada ya hapo nikajaribu kupiga simu kwa kutumia namba nyingine, maongezi yakawa hivi:
Mimi: Hello, naongea na Bryson!?
Yeye: (Akashtuka kama vile hamfahamu huyo mtu)!!
Mimi: Naongea na Bryson Kagenzi?
Yeye: Basi utakuwa ume-wrong number. Mimi sio bryson!
Mimi: Asubuhi njema. Nitakuwa kweli nime-wrong number.
Baada ya muda mfupi, ghafla ujumbe kama huo hapo juu ukaingia kwenye namba hiyo nyingine.
Nahisi nataka kuibiwa. Najua sio mimi tu, kuna wengine pia watakuwa wameshatuma hela.
Wana Science & Tech Forum, naomba mnisaidie kuthibitisha uhakika wa hizi taarifa.