Je, hali ingekuwaje kama Dr. Slaa ndiye angeteuliwa kupeperusha bendera ya UKAWA?

dr Slaa mikoa yenye wafuasi wengi wa cuf hasa ukanda wa pwani wote,mikoa ya ruvuma,njombe,iringa,rukwa,katavi,geita na simiyu angetupwa mbali sana na Magufuli....

kumbukumbu zangu zinaniambia Slaa hakufanya kampeni Tanga mwaka 2010 lakn kilichotokea kwa lowasa wote tunajua....
 
Tungethubutu kumsimamisha slaa tusingepata hata kura za CUF.
Tuwe wa kweli tu.

Na hapa ndipo palipokuwa na tatizo kubwa. Wanacuf siku zote wamekuwa hawamkubali Dk Slaa kwa sababu ya ukaribu wake na kanisa. na kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba CUF wangejitoa na kuungana na ACT. Na ACT walishasema Lipumba akigombea watamuunga mkono. Chhadema tungekuwa wenyewe na babu yetu Slaa. Hamasa isingekuwa kubwa kwa sababu Dr Slaa tayari anafahamika sana. Pia CCM walikuwa wamejiandaa kikamilifu kukmkabili Dr Slaa. Naomba nisisitize, hata tungemptisha Dr Slaa bado Lipumbavu angejitoa. CCM walishamweka mtu kati. Ndio maana mashabiki wao hapa jamii forum kina rutashobolwa walikuwa wanasema ukawa witavunjika kabla ya uchaguzi. msishaua hata Mbatia ccm walishamweka mtu kati. Pia ACT kingepata nguvu sana kwa sababu wabunge wengi wa chadema walikuwa wajiunge nao. Ishu ni kwamba ujio wa Lowasa n hamsa aliyokuja nayo vilivuruga mipango yote hiyo. Na hata wale waliokuwa wantaka kuhama chadema wakabadili mawazo. Project ya zitto ya wabunge 50 ikafa. Ndio maana mnaona Lipumba kajitoa baada ya yeye mwenyewe kumpokea Lowasa.

Kwa ujumla basi sioni ni kwa mvuto upi Dr Slaa angeweza kuleta hamsa kama iliyopo sasa. Kuna watu nawafahamu hawakuwahi kushabikia siasa lakini wamekuwa shabiki wa kufa mtu na watapiga kura kwa Lowasa. Kina maama wengi mwak huu watapiga kura kwa Lowasa kwa sababu wanampenda.

Tusisahau ukawa walikuwa na hofu hata ya kumtangaza mgombea wao kwa sababu ndani bado kulikuwa na mivutano. na Buguruni walikuwa wanasubiri tu Slaa atangazwe walianzishe! Kwa hiyo Lowasa alipokuja aliondoa zile tofauti na kuwaunganisha ukawa kuwa kitu kimoja.
 
DR ana mfadhaiko alafu Josephina amemzonga
anataka kujiunga na chama cha akina Mary, Siti na Anna ili amrithi Salma. Ndoto iliyoyeyushwa na ujio wa Rejina Chadema. Anachofanya kwa kutumwa na Sisiem ni jitihada za kupoteza na kuharibu Funguo ili Kufuli lisifunguke naye kama zuzu ameona ni
 
Habari zilizotapakaa jijini ni kwamba siku ya Jumamosi tarehe 28/9/2015 ndio UKAWA imepanga kuzindua kampeni zake kumtambulisha mgombea wake ambaye ni Dr. W. P. Slaa. Wiki moja kabla CCM ilikuwa imezindua kampeni zake kwenye uwanja huo huo ikimtambulisha mgombea wake Dr. J. P. Magufuli.

Hapana, nilikuwa naota tu ingawa hiyo ndoto imeniacha kwenye tafakari kubwa na nzito. Baada ya kufuatilia kampeni zilivyoendeshwa na zinakoelekea najiuliza je, hali ingekuwaje kama Dr. W. P. Slaa ndiye angeteuliwa na Chadema na kupitishwa na UKAWA (hapa sina hakika) kama mgombea Uraisi?

Nianze kwa kukiri kuwa hapo awali nilikuwa mpenzi mkubwa wa Dr. W. P. Slaa lakini kwa sasa nimemkubali E. N. Lowassa, je nilichukua uamuzi sahihi? Tofauti na wengi nilichukua uamuzi huo bila hata kusubiri nijue msimamo wa Dr. P. W. Slaa nikiwa na tumaini kuwa angeunga mkono uteuzi wa E. N. Lowassa.

Yaliyotokea yalitokea, Dr. Slaa alipojitokeza hakuunga mkono na badala yake aliamua kukaa kando na kutokujihusisha kabisa na siasa, uamuzi ambao nilikubaliana nao. Ghafla alijitokeza tena na safari hii alikuja na jipya kwa kusema kwamba hawezi, kukaa kimya, ameamua kuunga mkono upande wa pili.

Siku zote nimeamini adui wetu mkubwa kama taifa ni CCM na mimi ni katika wale wanaoamini kwa dhati kuwa CCM ni ile ile na haiwezi kusimamia mabadiliko. Hapa najaribu kujenga tu kajumba kangu angani...Lowassa na Slaa....nilikuwa naota tu.



Hii ndiyo Mbeya
Mkuu unauliza swali wakati majibu yamo humu humu JF. Kuna mada iloanzishwa humu kuwapima Dr.Slaa na Lowassa Je matokeo yake uliyaona?.. Leo hii wadanganyika kama kawaida yao wamebadilika, wale walomfuata Slaa wakati ule wamegeuka na kuwa wafuasi wa Lowassa kwa sababu hawaipendi CCM. Watu wameichoka CCM sana tu wala sii maajabu hata kidogo ila kuna uwezekano mkubwa Magufuli naye akavuta watu walompinga Lowassa akiwa CCM au UKAWA. Hivyo vyovyote vile, UKAWA ingevutia wananchi na pengine kufanya vizuri zaidi wakiwa na Slaa lakini tu kama Slaa angechaguliwa na vyama vyote shiriki. Hofu yangu kubwa ilikuwa Dr.Slaa kutopitishwa na CUF na hivyo kuanzisha mtafaruku mwingine baina yao.

Haya mnayoyaona ya TSUNAMI na sijui NYOMI ni matokeo ya UMASKINI wa wananchi wenyewe wanapojengewa tumaini. Hata Gwajima hujaza mihadhara yake yote, hii haina maana watu wataingia peponi..
 
Last edited by a moderator:
Huu ni UPUMBAVU wa wana ukawa wote, kuukubali UFISADI kuwa ni kitu cha kawaida sababu na wewe au 'kila mtu' ni fisadi.
Umri wako tafadhari!
Sio upumbavu wa wana CCM kukaa kimya wakati watu wachache wana fungasha pesa kwenye magunia ya chumvi ( esikroze )? Epa, Rada, Meremeta, Herikopter ya jeshi, ndege, pesa za wafadhili za HIV na Malaria? pesa toka world bank kwa matumizi ya ujenzi wa bara bara. Bado wataka niendelee kutaja..Ngalawa ya billion 8 pale kigamboni..CCM ndio wametufanya UUONE UFISADI ni kitu cha kawaida. Mimi nina miaka 75. Karibu.
 
Back
Top Bottom