Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Habari zilizotapakaa jijini ni kwamba siku ya Jumamosi tarehe 28/9/2015 ndio UKAWA imepanga kuzindua kampeni zake kumtambulisha mgombea wake ambaye ni Dr. W. P. Slaa. Wiki moja kabla CCM ilikuwa imezindua kampeni zake kwenye uwanja huo huo ikimtambulisha mgombea wake Dr. J. P. Magufuli.
Hapana, nilikuwa naota tu ingawa hiyo ndoto imeniacha kwenye tafakari kubwa na nzito. Baada ya kufuatilia kampeni zilivyoendeshwa na zinakoelekea najiuliza je, hali ingekuwaje kama Dr. W. P. Slaa ndiye angeteuliwa na Chadema na kupitishwa na UKAWA (hapa sina hakika) kama mgombea Uraisi?
Nianze kwa kukiri kuwa hapo awali nilikuwa mpenzi mkubwa wa Dr. W. P. Slaa lakini kwa sasa nimemkubali E. N. Lowassa, je nilichukua uamuzi sahihi? Tofauti na wengi nilichukua uamuzi huo bila hata kusubiri nijue msimamo wa Dr. P. W. Slaa nikiwa na tumaini kuwa angeunga mkono uteuzi wa E. N. Lowassa.
Yaliyotokea yalitokea, Dr. Slaa alipojitokeza hakuunga mkono na badala yake aliamua kukaa kando na kutokujihusisha kabisa na siasa, uamuzi ambao nilikubaliana nao. Ghafla alijitokeza tena na safari hii alikuja na jipya kwa kusema kwamba hawezi, kukaa kimya, ameamua kuunga mkono upande wa pili.
Siku zote nimeamini adui wetu mkubwa kama taifa ni CCM na mimi ni katika wale wanaoamini kwa dhati kuwa CCM ni ile ile na haiwezi kusimamia mabadiliko. Hapa najaribu kujenga tu kajumba kangu angani...Lowassa na Slaa....nilikuwa naota tu.
Hii ndiyo Mbeya

Last edited by a moderator: