Je, hali ingekuwaje kama Dr. Slaa ndiye angeteuliwa kupeperusha bendera ya UKAWA?

Mag3

Ungekuwa na busara ungesha ifuta thread yako. Mpaka leo hujui Dokta kakuza upinzani katika nchi hii.

Unaweza kufanya baya moja likafuta mema yoote.Nimeamini historia ni muhimu ktk uongozi.Mtu mwenye historia ya Usaliti,ataendeleza usaliti popote tena kwenye wakati mnapokuwa na uhitaji mkubwa.(Kanisa,Kamili,Fisiem na sasa M4C Original).
 
Last edited by a moderator:
DR ana mfadhaiko alafu Akanana kamemzonga kanataka kujiunga na chama cha akina Mary, Siti na Anna ili amrithi Salma. Ndoto iliyoyeyushwa na ujio wa Rejina Chadema. Anachofanya kwa kutumwa na Sisiem ni jitihada za kupoteza na kuharibu Funguo ili Kufuli lisifunguke naye kama zuzu ameona ni heri wakose wote!
 
Ninapofikiria matusi ya viongozi na makada wa CCM kwa E.N. Lowassa halafu nakumbuka matusi ya akina Lusinde, Mwigulu, Nape na UVCCM kwa ujumla wake kwa Dr. Slaa kabla hajaungana nao. Nachelea kusema safari hii kama Dr Slaa ndiye angekuwa mgombea hayo matusi bila shaka yangefikia kiwango kisichoelezeka wala kueleweza. Hata humu JF matusi aliyokuwa anarushiwa na watu kama FaizaFoxy, Ritz, Ruttashobolwa na wengineo yalivuka mpaka, hapa chini nawawekea tu baadhi ya matusi aliyowahi kutupiwa Dr. Slaa na FaizaFoxy humu JF;

FaizaFoxy said:
Mnaobwabwaja ni nyinyi na Slaa wenu, si mpaka awe na kazi ya kuweza kufanya maamuzi. Maamuzi yake ni kukopa fedha za walipa kodi zinazokwenda chadema kama ruzuku na kumjengea hawara.

Wizi, wizi,...
FaizaFoxy said:
Babu hachaguliwi kwa kuwa ni mzinifu, au biblia yako inakuruhusu kuzini?

Hayo ya huko ulipopataja hakuna anaekuja kutoka huko kupiga kura Tanzania.
FaizaFoxy said:
Wacha porojo, tuko Tanzania hapa hatuko Afghanistan wala Peru.

Babu Slaa hata tukiweka mgombea wetu awe jiwe basi tutashinda. Nani ampe kura babu asiye na maadili?
FaizaFoxy said:
Utamchaguwa wewe, sisi hatumchaguwi. Hilo ni wazi. 90% ya wapiga kura Waislam hawatathubutu kumchaguwa, hilo kumbuka.

Hatuwezi kuchaguwa mtu asiye na maadili hata kidogo, awe padri asiwe padri. Unamuona nyoka kaingia kwenye tundu halafu unapeleka mkono? mawee!
FaizaFoxy said:
Wewe wacha porojo, padri mzinzi Waislaam hatumpi kura. Hilo ni wazi na ukweli.
FaizaFoxy said:
Huyo babu Slaa wa josefina , kazi yake ni kudandia mada za watu, hazijuwi kichwa wala miguu, yeye akisikia anadandia.

Kwisha kazi yake, akalee kijukuu alichobambikiwa na josefina.
Huyo ni FaizaFoxy tu, bado wengine! Sasa fikirieni kama Dr. Slaa angekuwa ndiye mgombea, mbona ingekuwa kazi! Na hapa chini msikilizeni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM aka Kibajaji aka Mh. Lusinde;


 
Last edited by a moderator:
Tungeishia kusukuma gari lake mpaka hotini huku tukiimba rais rais rais ila kwa Edo hii ni mpaka Ikulu.
 
DR ana mfadhaiko alafu Akanana kamemzonga kanataka kujiunga na chama cha akina Mary, Siti na Anna ili amrithi Salma. Ndoto iliyoyeyushwa na ujio wa Rejina Chadema. Anachofanya kwa kutumwa na Sisiem ni jitihada za kupoteza na kuharibu Funguo ili Kufuli lisifunguke naye kama zuzu ameona ni heri wakose wote!
Mahaba yako kwa Lowassa yasikufanye ujenge dharau kwa wengine, kila zama na kitabu chake, Bila Dr.Slaa kukijenga hadi kuvunja ungo huenda hata mshenga Gwajima asingeleta barua ya posa.
 
UKAWA walifanya uamuzi sahihi kumteua Lowasa badala ya Dr. Slaa. Kwanza CCM wangefanikiwa kuwagawa kirahisi kupitia Lipumba ambaye aliandaliwa kujitoa mara baada ya kumtangaza mgombea wa UKAWA. Kumbuka baada ya kuteuliwa Lowasa hata Lipumba kujitoa bado impact haikuonekana kwa kuwa Lowasa ana wafuasi wengi kushinda mgombea yeyote hapa TZ. Magamba walipogundua mbinu yao kwa Lipumba imefeli ndipo walikomaa na mchumba wa Dr. mihogo na baadaye kumtia kimiani Dr. mihogo hadi kaingia mkenge lakini pia impact haijaonekana hivyo "vijisenti" walivyomhonga Dr. mihogo na tripu ya markekani havijasaidia kitu.
 
Slaa angekuwa kila siku analalamika kwenye majukwaa badala ya kunadi sera zake.....mara ungesikia vijana wa ccm wanawapiga vijana wetu, mara kura zimekamatwa mpakani.....pili, ungekuta tulisha vunja sheria za NEC kwa kuzidisha mda wa kampeni maana babu ni king'ang'anizi...
 
Ukweli ni kwamba sisiemu wamecheza karata yao safi, WAMESIMAMISHA JEMBE HASWA, hakuna mgombea wa upinzani wa sasa ambaye angemuweza, HUO NDO UKWELI.
Kama ukawa wangemteua Dr. Slaa kuwa mgombea wao, binafsi naona kwamba wangekuwa na wigo mpana wa hoja dhidi ya sisiemu, UFISADI likiwamo ambalo ni pana sana na linagusa sana wananchi. Pia wangekuwa na mtu ambaye ni mjenga hoja na mtetezi wa hoja zake kwa ufasaha, vile vile future ya chama cha chadema na ukawa kwa ujumla ungekuwa salama. Hata kama ukawa wangeshindwa, ambayo ni obvious, ila bado wangekuwa na image ktk jamii. Sasa hivi UKAWA na hasa chadema watake wasitake, hii karata waliyoicheza ni ya kufa au kupona, endapo watashinda, VIZURI, ila kama watashindwa, watarudi kuwa chama cha kawaida kabisa kisicho na mvuto kwa wengi, Lowassa baada ya kushindwa anaenda kustaafu siasa.
Slaa au hata Lipumba, walikuwa ni safe choices for the future being of ukawa. Wanasema, the highest risk yields the highest return, but if it's clear that the risk taken is a dead end, why risking?
 
Watakuja watu na kusema Dr. Slaa mzuri kuliko Lowassa. Na sababu watasema Lowassa fisadi. Hapa Tz ni kiongozi yupi ambaye hajawahi kupiga deal. Mimi mwenyewe ni Fisadi mdogo sembuse wakina JK .
Huu ni UPUMBAVU wa wana ukawa wote, kuukubali UFISADI kuwa ni kitu cha kawaida sababu na wewe au 'kila mtu' ni fisadi.
Umri wako tafadhari!
 
... nadhani sifa/historia ya kwamba aliwahi kuwa 'upadri' ingemnyima kura nyingi tu

Ukweli ni kwamba, JPM is invincible, TUTAKE. TUSITAKE! Hamna mwanasiasa wa sasa ambaye angesimamishwa na JPM alafu akawa na nafasi ya kushinda, HAMNA, sio ukawa wala sisiemu. Hivyo ishu ya upadre ingepunguza kura ila kumbuka hapa Tz hata ukimzidi mwenzio kura moja, we ndo rais.
 
Mkuu Maistro labda mimi nitakuwa nimeelewa tofauti hii Thread ya jamaa. Unikosoe hapa. Awali alikuwa anampenda DR. Lakini kutokana na kitendo kilichotokea cha kumkana Lowassa ile hali ya mapenzi kwa Dr. imepotea. Kingine ni ile haya ya undumi la kuwili. Unaongea hiki baada ya dk chache unaongea lingine. Na sidhani kama kuna mahala MAG3 ameonyesha kupiga kuhusiana na juhudi za DR. kukuza Upinzani. Unikosoe mkuu..!!
kuna watu wamekufa kutetea upinzani.sembuse
slaa
 
Kweli leo Mg3 wamekuwa watu wakutueleza Dr Slaa hatoshi.Lakini mie naamini kilichomkuta Slaa ni muendelezo wa Karma na hakika na wengine watafuata.
 
Tungethubutu kumsimamisha slaa tusingepata hata kura za CUF.
Tuwe wa kweli tu.

Hizo kura za CUF faida yake labda ktk ruzuku ya chadema kama chama cha upinzani kilichopata kura nyingi. Urais, JPM ni chaguo la Mungu, watu walitaka KUJIWEKA, narudia watu walitaka KUJIWEKA, nadhani wanielewa, na kuna wengine walitaka KUWEKA watu wao, ila Mungu akapangua na kuwashangaza hata hao wenyewe, alichukua fomu kimya kimya, akatafuta wadhamini kimya kimya na Mungu akampitisha kimya kimya.
 
>lakini kwa sasa nimemkubali E. N. Lowassa, je nilichukua uamuzi sahihi?<

Of course umechukua uamuzi sahihi. Hii ni kwasababau wewe unajua kuwa kuiondoa rushwa nchini sio kuikemea bali kupata Katiba yenye maana na unajua kuwa there is no way kama Magufuli atatupa Katiba nyengine zaidi ya hii iliyopendekezwa na CCM ambayo inalinda status quo ya CCM tu!
Kwahivyoa Kaka ulichukua uamuzi sahihi kumuunga mkono Lowassa.
Lowassa alikuwa hiyo sisiemu walioikataa hiyo katiba ya wananchi, ana miezi 2 na ushee toka ajiunge chadema, na mpaka sasa lowasa hajaongea cha maana kuhusu kuitetea katiba hiyo.
 
Nyie mnaesema Dr.slaa msaliti hivi mshajiuliza huo usaliti amemfanyia nani hasa? Acheni kushabikia maslahi binafsi ya wanasiasa yaliyopewa jina la matwakwa ya wananchi.
 
Back
Top Bottom