Je, hakuna teknolojia ya kupima njia za wajawazito bila kuingiza mikono kwenye nyeti zao?.

mweatu

Member
Jul 13, 2015
16
47
Ndugu wataalamu wa afya na wanajamvi kwa ujumla, nianze kwa salaam.

Kama tunavyojua kuwa mama mjamzito akiwa katika hatua za mwisho kukaribia kujifungua, wataalam wa afya huwa wanapima njia ya uzazi ili kujua imefikisha cm ngapi. Njia ambayo imekuwa ikitumika kwa mujibu wa wife anavyonisimuliaga ni kuingiza mkono kwenye nyeti zao.

Binafsi najisikiaga vibaya na naiona njia hii kama inawakera wamama pia. Hivi kutokana na kukua kwa technolojia kila mahala, je, haijapatikana technolojia ya kupima njia bila kuingiza mikono?

Msaada wenu tafadhari
 
anayempima njia ndo anayemzalisha, shida iko wapi? kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko vidole vya muuguzi. hvyo hakuna sababu yoyote kukereka na kupimwa njia.
 
Madaktari/wauguzi wakasha zoea hiyo kuzalisha huona ni mambo ya kawaida sana na hata hawatilii maanani. Wanacho waza kwa wakati huo ni kumzalisha salama tu na hata picha ya namna mkeo alivyo hufutika mara tu anapo jifungua. Madaktari huendelea na shughuli zao
 
Asante mkuu kwa ushauri
 
Wajawazito wenyewe wanakereka sana na hii kitu.

(Nilisoma mahali maoni yao juu ya hili)

Tena hivi vitoto vya field sijui ndiyo intern kila muda vinatia viganja kwenye tupu kupima njia.

Hivi kule kwa wazee wa hijab hali ipoje?
 
Madaktari/wauguzi wakasha zoea hiyo kuzalisha huona ni mambo ya kawaida sana na hata hawatilii maanani. Wanacho waza kwa wakati huo ni kumzalisha salama tu na hata picha ya namna mkeo alivyo hufutika mara tu anapo jifungua. Madaktari huendelea na shughuli zao
Asante mkuu kwa ushauri
anayempima njia ndo anayemzalisha, shida iko wapi? kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko vidole vya muuguzi. hvyo hakuna sababu yoyote kukereka na kupimwa njia.
Ni sawa, ila kumbuka kutoka kwa mtoto Kuna msaada wa nguvu ya ziada ya homoni za uzazi ndiyo maana kichwa huweza kupita. Sasa unapomuingizia mkono bila kuwa homoni zimesaidia ni kero Fulani.
 
Ultrasound inapima,
Hata kama Ultrasound machine inaweza ikatumika kupima vitu vyote wakunga na madaktari wanavyopima kwa kutumia mikono yao, zitahitajika machine nyingi sana na wataalamu wengi katika mahospitali na vituo vya afya nchi nzima. Sasa hivi ni kina mama wajawazito wachache wanaopata huduma ya Ultrasound angalau mara moja katika kipindi chote cha ujauzito. Inahitajika angalau ultrsound mbili za kawaida. Uchungu unapoanza mjamzito anatakiwa kupimwa kwa mkono angalau kila masaa matatu, sasa huo uwezekano wa kutumia Ultrasound kama mbadala, utatoka wapi?
 
Aliyesema ultrasound ni mjuvi na yuko sawa
Inategemea ni mimba ya miezi mingapi?
kawaida inakuwa mwanzoni na katikati ya ujauzito, sio wakati wa kuzaa...

1664221811759.png

Madaktari/wauguzi wakasha zoea hiyo kuzalisha huona ni mambo ya kawaida sana na hata hawatilii maanani. Wanacho waza kwa wakati huo ni kumzalisha salama tu na hata picha ya namna mkeo alivyo hufutika mara tu anapo jifungua. Madaktari huendelea na shughuli zao
Mwambie huyo huwa tunasahau haraka sana
 
Back
Top Bottom