Game Theory,
nakubaliana sana na mchango wako ambao umeenda deep ktk kujaribu kuwaangalia hawa jamaa.
Kifupi nitasema kwamba Andrew Young anaweza kuwa tapeli kama madai ya wengi hasa ambao wanategemea saana huruma na kazi za kanisa wakati dunia ya leo misaada haiwezi kwenda hivyo.
Pamoja na mengi yaliyokwisha semwa mimi naamini kuwa ni watu wachache sana huko je wanao amini kuwa Uchumi wa nchi zetu utapatikana tu ikiwa kuna ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi za nje na sisi badala ya sisi kuwa watumwa ndani ya biashara hizo. Ni Andrew Young na Bill Clinton pekee kati ya hawa wageni wengi wamekuwa na msimamo huo na hasa kauli na mifano kama hii:-
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]"The Third World has paid more money back than they got and in a sense the interest that they've paid is more than the principal they borrowed. And it really is morally unjust," Young said.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]He and Clinton suggested that, once relieved from their heavy debt burden, developing countries should invest in public services such as roads, schools and hospitals. Clinton cited Honduras, where debt relief has enabled the government to increase the number of children's school years from six to nine, and Uganda, where primary school enrollment has doubled, as examples.[/SIZE][/FONT]
Sasa basi pamoja na kwamba Tanzania itajengwa na sisi wenyewe watanzania ni muhimu tukumbuke kuwa maendeleo ya nchi hayatoki ndani peke yake. Dunia ya leo huwezi kufanya kitu bila kushirikiana na serikali ama Taasisi za nje ambazo zinaweza kuku jerk ulipokwama. Hata tukitazama hao Tigers na Malyesia wameweza kufanikiwa kwa sababu ya uchaguzi mzuri wa partner wakaachana na kutegemea sana IMF na World bank. Kuuundwa kwa mfuko wa Asia ambao walitanguliza kwanza imani kuwa nchi hizo haziwezi kuendelea ikiwa zitazidi kujilimbikiza madeni na mikopo yenye riba kubwa, wakajenga chombo kinachowazesha nchi changa kujenga miundombinu, vitu muhimu kama mashule, hospital na barabara, changes ziliweza kuonekana mapema na leo hii hawashikiki tena.
Tanzania tunatakiwa kuchagua rafiki na kama nilivyokwisha sema hata siku moja bepari hawezi kuwa rafiki yako ila anaweza kuwa very friendly nasi kiasi kwamba tukafikiria ndiye mtu bora. Huyo Clinton ndoto za usawa wa kiuchumi hakuzianza jana toka akiwa shule alikuwa akikerwa sana na umaskini wa nchi zetu. Alipopata wadhifa, Clinton he managed kukuza uchumi wa Amerika na Dunia nzima sote tulikuwa tukipeta na hakika ndoto yake iliweza kuonekana dunia nzima pamoja na kwamba haikupendwa na mabepari wengi. Akazushiwa fitna na ndio tukauona mwisho wake, lakini matunda yalikwisha onekana kote.
Hata ukitazama September 11, ni ugonvi kati ya familia ya Bush na Ossama kiuchumi, Huko Iraq ni ugonvi kati ya Bush na Saadam kugombea mafuta. Afghanstan ni ugonvi wa Bush na taliban kuweka bomba la mafuta kwani 100% ya washiriki wa sept 11 walikuwa WaSaudia, how can Afghanstan did became a victim - Yote ilikuwa kazi ya CIA na huyo Bent Scowcroft ni mhusika mkubwa sana.
Nilijua toka mwanzo kuwa hapa kuna jambo na harufu ya mzungu kupindisha uwezo wa Sullivan foundation kwa kutumia jina la Andrew Young hali nia na malengo yao sio mabaya maadam sisi tuko macho na makini.
Kwa hiyo ni muhimu sana kwetu kuchunguza nani rafiki na nani adui yetu.