Je, GEORGE KAHAMA na ANDY YOUNG wamegombana?.. Will IKULU Intervene?!

Yeah GT...high level data need time to learn and understand before contributing.Usisikitike instead give people time
 
Madela wa Madilu, very poetic! BUt excellent point you make! Mimi sikati tamaa hata kidogo! Naona JF imewezakufanya contribution kubwa sana na mtakuja kuona wote matunda yake in 10 years, when we reflect that the real political reforms in Tanzania started on a virtual forum. For your information many ex-Soviet bloc countries walikuwa na forums za wasomi and that is where the real opposition was born, sasa here we have a virtual forum but serves the same purpose!
JF imetufungua wengi macho, it has made us think, prod and push and question and it has served a noble cause!

hilo neno kaka, point kubwa tu waache watudharau hapahapa kuna mawaziri wa kesho, na wabunge wa leo na kesho, acha tuwaonyeshe kuwa tunafahamu wanayoyafanya, itawasaidia kuficha zaidi tusiyaone maana tukiyaona tunaumia na kukata tamaa ya kuijenga nchi wakati wengine wamelala wanasubiri tukimaliza kujenga wakalale.
mi hata kazi siwezi kufanya tena maana najiona mtumwa na tumikishwa na ndugu zangu wenyewe, kama mnania ya kuwarudisha wakoloni mtuambie...
Ehee Mungu kwanini umemchukua Nyerere ukatuachia mafisadi loooh
 
ninachofahamu GBP ni ya mwarabu mmoja anaitwa Badr yuko pale kurasini na ni trader wa mafuta,au miliki imebadilika?

makubwa usinikumbushe mtwara kuna mwekezaji mmoja eti mfaransa kanunua eneo kubwa jamani eneo la baharini eti ni muekezaji nasikia kuna misimba kwenye hilo eneo na anafuga migombe kwa ajili ya kuwalisha misimba hiyo. wanakijiji wanaliwa na misimba anasema wasiuawe na wazawa walikuwa wanajivuvia na kulisha vijimifugo vyao sikuhizi ukipatikana shaba. yani nimetembelea hilo eneo ni barabarani kabisa mi nataka kujua ni wazawa wnagapi wamefaidika na huyu muekezaji please mwenye data atupe maana nahisi tumekwisha.
 
Kimya cha wana JF kimenitisha, nilitegemea watu wangekuja na maoni mbali mbali kuhusu hili lakini assumption yangu ni kuwa:
either

Nimeenda too deep for your normal taste(yaani sijaipoliticise)

Au mnaogopa kutia neno kuhusu huyu GEORGE KAHAMA

either way i am not sure kama kuna uhumihi wa kuendelea kumwaga data za namna hii manaan nilikuwa na zingine kuhusu waingereza wanvyoitia Umasikini Tanzania kupitia DFID pale Dar lakini naona its not worth it
No Game Theory, watu wamekaa kimya sio hawataki kuchangia, bali they need ample time to grasp maana nondo yenyewe ni deep hivyo naamini wengi bado wanatakari huku wengine nikiwemo mimi tunaconnect the dots.
 
Deals za Balozi Stilth, Young na Bongo zilianzia Enzi za Mkapa. Stilth akiwa balozi wa Marekani ndiye mtu wa kwanza kusimamia ziara ya kiserikali ya rais wa Tanzania nchini Marekani. Wakati huo Stilth akiwa damudamu na Balozi Young wakati huo Balozi Young akiwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Morehouse Collage kilichopo Atlanta Georgia nchini Marekani. Akiwa Marekani, Stilth alimlobi Young kumpatia Mkapa degree ya Heshima toka Morehouse College. Mkapa akawa Dr.
Hii maana yake ni hatua ya kwanza ya kumnunua Mkapa ili asikwamishe deals.
Baada ya kumaliza kipindi chake cha ubalozi nchini mwaka 2000 kufuatia chama chake cha Democrat kubwagwa manyanga nchini kwake, ikamlazimu kufungasha virago na kurejea nyumbani, (kama anavyofungasha virago balozi wa sasa baada ya Republican kubwagwa), Balozi Stilth akaanzisha NGO yake iitwayo APARC yenye makao yake makuu Boston ambako yeye Stilth ndiko alipotoka na ndipo anapoishi.
Lengo la APARC pamoja na mambo mengine, ni kuutumia uwezo wa marais wastaafu wa Africa kutoa elimu kwa kizazi cha viongozi wa kesho kwa kutoa mihadhara mbalimbali katika vyuo vikuu vilivyoteuliwa.
Wakati nikiwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nilibahatika kuwamo katika listi ya wanafunzi 2O wa UDSM katika mkakati wa APARCH hivyo tulipelekwa nchi mbalimbali kusikiliza mihadhara ya marais wastaafu wa Afrika na mwisho wa masomo yetu watakao onekana wanafaa kuwa viongozi wa kesho, wengepatiwa scholarship za kufanya masters na Ph.D Boston University ya Chuo Kikuu cha Masachussets nchini Marekani.
Ni katika ziara hizo za kimasomo, nikaanza kuhoji mwenendo wa Mchungaji Stilth na hii APARC yake ambayo kwa namna moja ama nyingine, inafadhiliwa na serikali ya Marekani.
Kwanza niligundua timu ya wanafunzi waliochaguliwa katika mchakato wao, ni wale ma activist wenye leadeship potential, lengo la mwisho ni kuandaa viongozi wa kesho ambao watakuwa Americanized ili wakiukwaa uongozi, walinde maslahi ya wamarekani.
[NB. Ni wamarekani ndio wameilazimisha serikali kuchukua biodata kwa finger prints kwa
kila muombaji wa passport mpya huku tukifika Marekani lazima unapigwa tena picha na kuchukuliwa alama za vidole kujiridhisha wewe ndiye yule waliyenae, zikipishana, safari yako inaishia uwanja wa ndege. Sitashaa kitengo cha vitambulisho vya kitaifa kimewekwa mambo ya ndani na si ajabu wataalu washauri ni wamarekani. Waziri nae si mnajua tena, na hatakuwa ajabu kampuni iliyoshinda ni ya wamarekani nb, hii ni dhana tuu].
Naendelea na mada, nilipotafiti nchi wanachama wa APARC nikakuta ni nchi zilizokuwa na ama mwelekeo wa kikomunist kama Ghana, Zambia na Botswan ama mwelekeo wa kijamaa kama Tanzania, na nchi zilizotawaliwa na wareno kama ANgola na Mozambique.
Lengo likiwa kwanza kuwachukua marais hao wastaafu na kuwaweka kambini nchini Marekani hivyo kuwabrain wash kisawasawa ndipo baada ya hapo kuwazungusha nchi mbalimbali kutoa mihadhara ya uongozi. Zamu ya Mwinyi na Mkapa inakaribia.
Nakumbuka ziara yangu ya mwisho ni ile ambapo Dr. Migiro alitunukiwa nishani, nilipata fursa ya kumuuliza Balozi Stilth, ni vigezo gani wamevitumia kuzichagua nchi walizozichagua, alijibu kwa mkato, 'just randomly'. Nikadadisi zaidi kwanini wasingetujumuisha nchi zetu tatu za EAC ili sote tupate viongozi bora katika safari ya kuelekea shirikisho, alihitimisha kwa kusema, kwa vile selection was randon, Tanzania ndio the fortunate, and Kenya na Uganda was not so fortunate. Sasa ndio nimegundua why Tanzania. walishagundua udhaifu wa sheria zetu za ardhi kitu ambacho hakipo kenya wala uganda. the real deal ni madini ya Dhahabu ndio maana Afrika Kusini, Msumbiji, Botswana, Tanzania na Ghana!. Maswali yangu hayo kwa Stilth yalipelekea kuhitimisha hatma yangu na APARC na masters ya Boston ikaota mbawa!.
Kujifanya unatafuta sana ukweli, sometimes kunaponza na kupoteza opportunities. ningejikalia kimya, saa hizi, ningekuwa ninangara na masters ya BU.
Watu wenye kuona mbali kama Stilth waache tuu, ila pia sio siri, serikali yetu inafanywa ni ya mabwege mtozeni, ama mkono mrefu umerufushwa mpaka kwa Mzee wa Magogoni, na jinsi alivyo jeuri na kiburi, akishatia pamba masikioni huwa hasikii la mtu, si la muadhini wala la mnadi swala. Jee kilio hiki kitaangukia sikio la nani?.
 
Kimya cha wana JF kimenitisha, nilitegemea watu wangekuja na maoni mbali mbali kuhusu hili lakini assumption yangu ni kuwa:
either

Nimeenda too deep for your normal taste(yaani sijaipoliticise)

Au mnaogopa kutia neno kuhusu huyu GEORGE KAHAMA

either way i am not sure kama kuna uhumihi wa kuendelea kumwaga data za namna hii manaan nilikuwa na zingine kuhusu waingereza wanvyoitia Umasikini Tanzania kupitia DFID pale Dar lakini naona its not worth it

Anyway thanks MADILU kwa mchango wako

We GT vipi, huwa tuakushambulia kwa post za ajabu sometimes, this is very sensitive na nafikiri watu wanataka kuwa na uhakika zaidi hasa kupitia hizo link zako, nadhani ndio ukomavu huo, siju mnasemanje wenzangu.
 
Hakika haya mabo makubwa na anagusa kwa karibu sana uchumi wa nchi. Hakika Sirikali wanatakiwa wae makini sana kujiingiza katika sakata hili.

Kani kuna maslahi makubwa sana na US
 
Kimya cha wana JF kimenitisha, nilitegemea watu wangekuja na maoni mbali mbali kuhusu hili lakini assumption yangu ni kuwa:
either

Nimeenda too deep for your normal taste(yaani sijaipoliticise)

Au mnaogopa kutia neno kuhusu huyu GEORGE KAHAMA

either way i am not sure kama kuna uhumihi wa kuendelea kumwaga data za namna hii manaan nilikuwa na zingine kuhusu waingereza wanvyoitia Umasikini Tanzania kupitia DFID pale Dar lakini naona its not worth it

Anyway thanks MADILU kwa mchango wako

Mkuu, sio kuwa tunamwogopa yeyote kati ya hao uliowataja na ambao hujawataja. Ila binafsi mikono imekufa ganzi na ubongo umesizi. Nashindwa kuelewa tunaongozwa na viongozi wa aina gani jamani Tanzania ya leo. Ni jukumu letu sisi tunaopata hizi habari kuwa na mjadala wa kitaifa wa kulinusuru taifa letu linaangamia na kupotea. Tafadhali ili tuliweke kwenye jamii ya kitaifa na kimataifa uozo huu ufahamike na kila mtu mkubwa kwa mdogo. Nchi imeuzwa kilichobaki ni kupokea risiti za mauzo tu! Tutoe tamko moja la nguvu, haya mambo yashishie hapa jamvini tu.
 
Kimya cha wana JF kimenitisha, nilitegemea watu wangekuja na maoni mbali mbali kuhusu hili lakini assumption yangu ni kuwa:
either

Nimeenda too deep for your normal taste(yaani sijaipoliticise)

Au mnaogopa kutia neno kuhusu huyu GEORGE KAHAMA

either way i am not sure kama kuna uhumihi wa kuendelea kumwaga data za namna hii manaan nilikuwa na zingine kuhusu waingereza wanvyoitia Umasikini Tanzania kupitia DFID pale Dar lakini naona its not worth it

Anyway thanks MADILU kwa mchango wako
Kama ni kweli tunauzwa mchana kweupe,sasa huo ndio urafiki wetu na Marekani ulipojificha,tuokoe kilichobaki kabla ya kutokea ya DRC,Liberia na mwingineko.
 
George Kahama pamoja na akina Rupia ni moja kati ya ma UNTOUCHABLES bongo na wamekuwa immune for such a long time humu JF

Anyway kama mnavyojua kuwa yule bibie kwa jina la JILL amekuwa akiwaendesha puta maofisa wa Ikulu kutaka apewe special access to JK na kuna taarifa kuwa alifanikiwa kuipata namba ya JK ambayo hata mimi ninayo na mwanakijiji anayo vile vile hivyo siyo siri lakini JK amekuwa hataki kuwa involved moja kwa moja na mambo haya bila washauri wake kumwambia details zinaendaje.

Lakini kuna tatizo lingine ambalo limeibuka out of no where...

Mnavyojua akina KAHAMA walikuwa wako very prominent katika mining industry ya Bongo kwa kutumia influence yao na ndio walio wa-accomodate wale Wa-Canada in the 1990's

Kisha kuna kipindi wakawa wako close na hao GOODWORKS ambao kwa kweli credit anapea huyo Mchungaji Charles Stith.
LG18356.jpg


I have managed to connect the dots na kujua kwanini JILL amekuwa halali ma jisimu isio na wakati maalum

SABABU NI HUYU BWANA:

friedman.jpg

Ana itwa BRENT SCOWCROFT na ni:

hebu soma hapa: The Scowcroft Group, An International Business Advisory Firm


WEST POINT undergrad
COLUMBIA postgrad & PHD
MORMON
INTERNATIONAL RELATIONS SPECIALIST
NATIONAL SECURITY ADVOSOR to: current Bush and Ford,

Bila kusahau kazi yake nyingine alikuwa ni Chairman wa President's Foreign Intelligence Advisory Board ambayo katika mission statement yake inasema ni:


Kisha wanaendelea kusema:

source: http://www.whitehouse.gov/pfiab/

Personally nishawahi kumuona huyu mzee SCOWCROFT akizungumza katika duru za mambo ya Kimataifa lakini it never came to my mind kuwa atakuja kuwa prominent bongo kwani nilijua huyu ni mmoja kati ya wale ma architects wa vita kule Iraq.

In short jamaa ni beyond CIA na kampuni yake hii ambayo haina haja ya kupiga hodi kuingia IKULU ni manyoka watupu ambao wameletwa na mheshimiwa GEORGE KAHAMA na hilo ndilo tatizo kubwa linalomkosesha usingizi bwana ANDREW YOUNG ambaye alidhani anaweza kutumia charm na black brotherhood kupata access na kazi toka kwa JK. Sasa looks like CIA aka "THE COMPANY" are in town na access ya IKULU wanayo na sitoshngaa kama JK atakuwa hawapigii wao simu badala ya wao kumtafuta.

GEORGE KAHAMA kawaingiza Tanzania na washasaini mkataba kwa kutumia nafasi yake kama Advisor wa Tanzania Chamber of Energy &Minerals na vile vile kama member wa Tanzania National Business Council na post yake kama post of vice-president of the Tanzanian Royalty Exploration Corp ,

Kutokana na maelezo katika website yao, akina SCOWCROFT hawasemi mengi sana na inawezekana ikawa akina Kahama waliaambia wasifanye makosa kama akina GWI ambayo yameibua maswali mengi kuliko majibu.

Sasa hawa TANZANIA ROYALTY wamewanyima tenda akina Andy Young na wakaamua kuwapatia hawa akina SCOWCROFT GROUP ambayo ni ya mheshimiwa pichani hapo juu. Cha ajabu ni kuwa akina Andy Young walipata vijikazi kule Ghana kwa kumtumia Walter Kansteiner ambaye alikuwa ni Assistant Secretary for African Affairs and currently board member of Jean Raymond Boulle.

Sasa quick search yangu nimegundua kuwa hao Jean Raymond Boulle


Nikapata hili:

http://www.swtriallaw.com/att-werbner/jean-raymond-boulle.html

http://www.globeadvisor.com/servlet/ArticleNews/story/gam/20060508/RTAX08


POINTS OF INTEREST:

1) Hivi kama watu kama hawa wakishapata unprecedented access na ofisi yetu kubwa je sisi tutakuwa na la kusema wakitulazimisha mikataka mingine mibovu?

2) SCOWCROFT group kama kampuni haikatazwi lakini kutokana na nature ya kampuni yeyenyewe what makes you think our national security will not be compromised?

3) Ndio tunataka ma investors lakini at what price? And who will pay that price? Hivi Mheshimiwa MBUNGE kama GEORGE KAHAMA yuko tayari ku compromise our national security kwa sababu ya njaa yake what makes you think wafanyakazi wa chini watashindwa ku-leak mambo kwenye internet?

4) Role ya FOREIGN ni kui-advice serikali katika mambo haya japo TCCIA wanaweza wakawa hawana objection lakini hii inanifanya ni conclude yafuatayo:

a) RADHIA MSUYA ambaye ni mkuu wa kitengo cha NORTH AMERICA & EUROPE pale either alikuwa nawajua hawa lakini akaamua kukaa kimya au walipeleka assessment yake lakini wakaamua kumdharau

b) RASHID OTHMAN inawezekana alipeleka intelligence estimate ya hawa SCOWCROFT lakini IKULU waliamua ku overule kwa hiyo inawezekana hii ikawaondoa Usalama wa Taifa from this web

c) UBALOZI wetu DC someone is or is not doing his job properly na kama ulifanya then katika chain of command kuna walakini

d) BENARD MEMBE kama mtu niliyekuwa ninamtegemea angeweza kuweka hili wazi naye inaonekana amekuwa overruled na IKULU ambako in the wake of recent scandals kuanzia Jenereta la Richmond to Benki kuu wameprove kuwa ni ma incompetents na hawaji na majibu straight kwa walipa kodi na in other words they are out of touch with the reality on the ground.

5) Je nani anafanya vetting ya hizi kampuni zinazoingia Tanzania? Je KAHAMA kama mtu ambaye alikuwa serikalini kwa muda mrefu je anayo 'our national interest at heart' au kwake muhimu ni pesa tuu?

6) Tatizo siyo hizi kampuni bali ni web of secrecy ambazo zina-operate Tanzania and I have a belief kuwa hii inatokana na jinsi walivyo free kufanya walitakalo na serikali yetu inaonekana kuwa imejaa rushwa. Japo wanaona kuwa hawapati bad press internationally lakini this cannot last for long in my opinion

Last but not least washauri wa JK katika masuala ya UCHUMI ni wachemshaji wakubwa mno. Kila mtu anajua hakuna serious African American investor wa kuinvest Bongo kama wangekuwepo basi huyo MCHUNGAJI STITH angewaleta tangu mid 90's

Asante Mdau nadhani historia inajirudia.haya ndo mambo yaliyofanyika Angola wakati makampuni ya kijasusi yakichukua almasi ya Angola kwa migongo ya kina savimbi.sasa Tanzania tungoje tuone Ubeberu uliokubuhu.
 
Back
Top Bottom