Je, George Floyd ni mtume?

Je, George Floyd ni mtume?

chabuso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
6,379
Reaction score
5,887
Habari za mitandaoni Dunia nzima Ni kuhusu kifo cha Mmarekani Mweusi George Floyd.

Katika dini ya Kiislam Mitume iko mingi wengine wanajulikana na wengine hawajulikani. Kuna Mitume Kama 123 ambayo inajulikana, kuna Mitume inaliyopewa vitabu na isiyopewa vitabu.

Mitume inafanya kazi ya Mungu katika jamii iliyomzunguka au hata kuleta mabadiliko Dunia nzima. Yesu aka Issa aka Jesus kabadilisha Dunia, Muhamad kabadilisha Dunia, kuna akina Musa, Sulemani nk ambao wamebadilisha jamii zao.

Uonevu kwa watu weusi unaofanywa na Polisi katika nchi ya Marekani haujaanza leo. Kifo cha George Floyd kimeleta mtazamo mwengine katika vitendo vya uonevu vinavyofanywa na Polisi kwa watu weusi.

Hivi sasa dunia nzima, nchi za Ulaya, Marekani, Australia nk watu wanaandamna mbele ya balozi za Marekani kupinga unyanyasaji wa Polisi kwa watu weusi.

Katika Jimbo la California Polisi leo wameungana na waandamanaji kupinga vitendo vya unyanyasaji wa watu weusi. Cha kushangaza, wengi wa waandamanaji ni watu weupe; cha kushangaza zaidi, nchi za Kiafrika ambazo ni chimbuko la watu weusi hamna hata nchi moja watu wameandamana kupinga uonevu huo.

Donald Trump leo kalazimika kupelekwa kwenye handaki chini ya White House kwa usalama wake baada ya waandamanaji kuandamana mbele ya White House.

Jeshi limeingia mitaani kuungana na Polisi, kafuu ya kukataaa watu wasitoke majumbani mwao imewekwa nchi Marekani. Haijawahi kutokea, Marekani kama vile kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Je, George Floyd ni Mtume asiejulikana alietumwa na Mungu kuibadilisha mitazamo ya watu kuhusu mtu Mweusi nchini Marekani?
 
Je George Floyd Ni Mtume asiejulikana alietumwa na Mungu kuibadilisha mtazamo ya watu kuhusu mtu Mweusi nchini Marekani?

G. Floyd, Mtume wa Mungu aliyetolewa "kafara na Mungu" ili kubadilisha mtazamo wa watu (weupe) kuhusu mtu mweusi nchini Marekani?

Hii haiingii akilini hata kidogo, kama yeye ni kafara kutoka kwa Mungu, je wale askari waliomuua hawana makosa?
 
Ila kusema ukweli ubaguzi unaofanyika huko majuu umenifanya niichukie hii tittle ya kujiita 'diaspora'. Bora tu kunyuti huku huku 'nyumbani' Africa, madiaspora mnisamehe.
 
Let USA burn and gringos learn their lesson......

Where is KKK now??
 
Ungekuwa unamjua Rodney King sijui kama ungeandika Haya maana nae alipigwa na mapolisi wanne vibaya sana na kumsababishia ubongo kuharibika na kuvunjwa mbavu na meno

Pia hukumu ilikuwa not guilty kwa wote
Vurugu na maandamano hii ni cha mtoto sasa sijui na huyo tumuitaje
 
George Floyd ni sampuli ya ubaguzi ulioonekana wazi wazi, wapo wengi kuna mwingine alinyongwa kwa kutumia rungu kwa mtindo uleule " I can't breath".
 
G. Floyd, Mtume wa Mungu aliyetolewa "kafara na Mungu" ili kubadilisha mtazamo wa watu (weupe) kuhusu mtu mweusi nchini Marekani?

Hii haiingii akilini hata kidogo, kama yeye ni kafara kutoka kwa Mungu, je wale askari waliomuua hawana makosa?
Kwani hadithi ya Yesu ilikuwaje?kwani Yesu hakutolewa kafara na MUNGU,Mungu anaweza kufanya chochote

Hivi sasa media hazizungumzi tena kuhusu Corona,watu wanaandamna bila kujali Covid19

Dunia imebadilika George Floyd kabadilisha Dunia kuliko Corona..

George Flyod ni Mtume,.. Mtume mwingine alikuwa Bob Marley yeye alikuja na Style nyengine..

"Burning and looting tonight, burning all pollution tonight,burning all illusion tonight"

Hayo ni maneno ya Bob Marley hayo ndio yanayotokea..

G. Floyd, Mtume wa Mungu aliyetolewa "kafara na Mungu" ili kubadilisha mtazamo wa watu (weupe) kuhusu mtu mweusi nchini Marekani?

Hii haiingii akilini hata kidogo, kama yeye ni kafara kutoka kwa Mungu, je wale askari waliomuua hawana makosa?
 
George Floyd ni sampuli ya ubaguzi ulioonekana wazi wazi, wapo wengi kuna mwingine alinyongwa kwa kutumia rungu kwa mtindo uleule " I can't breath".
Kweli Mkuu, huyo jamaa alikuwa anaitwa Rodney King, lakini mpasuko haukuwa Kama hivi, George Ni habari nyengine amemfanya Trump aingie kwenye Handaki
 
Kweli Mkuu, huyo jamaa alikuwa anaitwa Rodney King, lakini mpasuko haukuwa Kama hivi, George Ni habari nyengine amemfanya Trump aingie kwenye Handaki
Nimewakubali sana waandamanaji,wameusukuma ujumbe wao kwa nguvu sana.
 
Vitu vingine bwana watu sijui mkoje,unauliza na umesha jijibu humo humo, kweni kuandamana ndio kigezo cha mtu awe mtume? hizo ni ghadhabu tu za watu juu ya uonevu na ni hali ya kawaida na isiyo mpa mtu utume wowote. Yaani sijui hata nikuelezeje by the way unaelewa ila tu na wewe umeamua kutafuta michango ya watu kwa mada ndogo
 
Ungekuwa unamjua Rodney King sijui kama ungeandika Haya maana nae alipigwa na mapolisi wanne vibaya sana na kumsababishia ubongo kuharibika na kuvunjwa mbavu na meno Pia
Na hukumu ilikuwa not guilty kwa wote
Vurugu na maandamano hii ni cha mtoto sasa sijui na huyo tumuitaje
Rodney King hakuleta mpasuka Kama wa George, George kawafanya Polisi wapige magoti,

National gurd wamepelekwa mitaani sio Jimbo moja

Watu weusi wameshirikiana na weupe,vurugu za Rodeny king, weupe walipigana na weusi Sasa hivi ni tafauti

Kikubwa zaidi Raisi wa Taifa kubwa kaingia handakini kwa kuogopa raia wake
 
Kwa sasa dini imekaa ipasavyo mioyoni mwa wanadamu, kutokea mtu from no where na gafla umuite mtume ni kugombana na hao ambao dini imekaa mioyoni.

Wanasahau misaafu ni historia.
Difficult nowdays.
 
Back
Top Bottom