JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,327
- 9,328
Je, gari yako inatetemeka engine ikiwa ya baridi?
Je, engine ya gari yako inamisi inapokuwa ya baridi?
Je, gari yako ukiwasha inazima yenyewe mpaka uwashe mara kadhaa au uwashe na kupiga resi mara kadhaa ndio itulie isizime?
Kwanza kabisa kama ukiwasha gari unakimbilia kupiga resi basi unategeneza tatizo lingine kubwa na muda ukifika zitakutoka hela nyingi. Kwanza ukiachana na kukumalizia mafuta, kupiga resi baada tu ya kuwasha gari inaweza kupelekea spark plug kuwa fouled (yaani spark plug zako zinakuwa covered na mafuta, Oil au carbon na hivyo kuzifanya zishindwe kufanya kazi katika ubora wake)
Sasa turudi kwenye maada. Kama gari yako inatememeka, kumisi au kuzima kila ukiwasha mpaka uwashe mara kadhaa basi kwa sehemu kubwa matatizo huwa yanakuwa kwenye sehemu mbili au tatu kulingana na aina ya gari. Sehemu hizo ni:-
1. Intanke Air Temperature (IAT) sensor
Hii sensor ina njia mbili za kufa, Inawez kufa ikawa inapelekea signal kwamba hewa inayoingia kwenye engine ni ya moto(hot signal) au signal ya cold signal. Kama ikipeleka signal ya hot basi gari lako lazima tu likusumbue kuwaka kwa sababu mafuta yatakuwa yanaenda machache na engine ni ya baridi hivyo hayatawaka vizuri. Baadhi ya watu atasema alisolve hili tatizo kwa kubadili MAF sensor ila kama connector ya hiyo MAF sensor ina pin 5 basi ndani ya hiyo maf sensor kuna IAT sensor pia na hakuna namna unaweza kuzitenganisha
2. Engine Temperature sensor(ECT) sensor
Hii sensor ina tabia zinazofanana na za hiyo IAT sensor hapo juu kwa asilimia 100. Utofauti ni kwamba hii yenyewe inapima joto la coolant. Kwa hiyo nayo kama muda wote inapeleka signal ya hot basi lazima gari litasumbua kuwaka au litawaka kwa kumisi na kuvibrate. Ni vizuri mtu akawa makini, usije ukaona tatizo ukakimbilia kwa fundi ukamuambia akubadilishie sensor hii, baadhi ya gari zinakuwa na sensor za aina hii mpaka 3, zingine kwenye rejeta na zingine kwenye engine, hivyo unaweza kubadili na tatizo lisiishe kumbe umebadili sensor nzima.
3. Exhaust Gases Recirculation(EGR) Valve
Kama hii valve ikijaa carbon au solenoid yake ikiwa mbovu basi inaweza kupelekea valve hii kubaki wazi wakati gari inawaka wakati ilitakiwa kuwa imefungwa. Sasa mafuta yanakuwa yanawaka kwa shida halafu kuna exhaust gases zinarudi tena kuja kuchomwa, hapo lazima gari liwake kwa shida. Pia gari nyingi hazina EGR valve labda kwenye SUV na baadhi tu ya sedan/saloon.
Kama kuna kitu ambacho nitakuwa nmekisahau nitakiongeza.
MWISHO.