Je, eda ya Samia kuzua mgogoro wa kikatiba?

Je, eda ya Samia kuzua mgogoro wa kikatiba?

Hapa tunazungumzia Sharia. Kweli eda ni kwa jobless siyo mtumishi wa serikali.
Basi kama IPO kisheria kila mfanyakazi wa serikali apewe eda siku 90.
Sheria inawahusu wafanyakazi walio chini ya sharia pia! Sharia is inferior to sheria.
 
07 September 2026

Mke Kukaa Eda Ya Kufiwa Na Mumewe​

View attachment 3666027

UFAFANUZI KWA MUJIBU WA KORAN
Sheikh Muhammad Mahdi-shushtari Mke Kukaa Eda yakufiwa Na Mumewe
Mwanamke mwenye kufiwa na mume kama hana mimba eda yake ni miezi minne (4) na siku kumi (10), na kama mwenye mimba eda yake mpaka azae, lakini iki wa amezaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi lazima akae eda hadi zipite, siku hizo.

Mwanamke mwenye eda ya kufiwa na mumewe, ni haramu kuvaa nguo za rangi; kujipamba kwa namna yo yote kwa mwili au kwa nguo kama kujitia manukato, kutia wanja machoni, mapodari, hina na kila jambo la kujipamba ni haramu kwake hata nguo nyeusi ikiwa ina nakshi au mkato wa kujipamba.

Eda huanzia siku ya kufa kwa mume ikiwa yupo hapo, na kama hayupo huanzia siku atakapopata habari hata kama kumepita muda mrefu sana. Katika muda huo wa eda hawezi kuposwa au kuolewa.

Uislamu unaamrisha unadhifu, basi wanaruhusiwa wanawake wenye eda kuoga kujisafisha na kuweka mwili safi, kukata kucha.

Anaruhusiwa kutoka nje kama ipo haja kama kununua mahitaji yake au kumwangalia jamaa au mgonjwa na kadhalika, asitoke nje paisipo na haja.

Tunaomba kwa Mola wetu atupe sote Twafiki ya kufuata maamrisho ya dini na kuepukana na yaliyoharamishwa au kufuata mambo ya Bida'a uzushi, usiona msingi.


MAONI YA MRENGO MWINGINE WA WANZUONI WA KIISLAMU KUHUSU EDA YA SAMIA HASSAN, NA MAJUKUMU NJE YA UISLAMU


View: https://m.youtube.com/watch?v=lRJqKloRX80
 
Sawa katiba inasemaje ikitokea au kama hamna kifungu ndio wakati sasa kwa haya mambo yametokea kuainisha kwenye katiba tarajiwa.

Maana eda ni siku 90, nchi haitokuwa na rais
Tanzania inaweza kutawaliwa na mwanaccm yeyote hata ambaye hajachaguliwa na wananchi.
 
Tanzania inaweza kutawaliwa na mwanaccm yeyote hata ambaye hajachaguliwa na wananchi.
Sio hilo tu unaweza kumpigia kura unayempenda ila ikatokea awaelewani wanaafukuzana kwa manufaa yao haijarishi na awazingatii kura za wananchi.
 
Sio hilo tu unaweza kumpigia kura unayempenda ila ikatokea awaelewani wanaafukuzana kwa manufaa yao haijarishi na awazingatii kura za wananchi.
Ukiwaona kwenye nyumba zaidi, wana sura kavu kama sio wao
 
Bila shaka huu ni mjadala wa kikatiba zaidi na wala sio mjadala wa kiitifaki. Je, katiba inatoa masharti gani na urefu gani kuhusu likizo za Rais? Je, katiba inasemaje juu ya eda ya Rais?

Lakini kwa nini Urais wakaimishwe watu wawili badala ya mmoja kama inavyotaka katiba kuwa huyo aliyekaimishwa kama naye hayupo basi atakaimu wa chini yake? Hii ya kuwakaimisha watu wawili kwa wakati mmoja inaelekezwa na matakwa ya kifungu gani cha katiba?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 8 Septemba 2026; Saa 5:40 jioni.

Waione mawakili: Helen Kijo-Bisimba, Boniface Anyisile Mwabukusi, Ado Shaibu, Paul Kisabo, Addo November Mwasongwe, Hilda Stuart, nkView attachment 3665939
Katiba ya Tanzania awamu ya Samia imepatwa kama mwezi na jua, serikali wanajigeuza geuza tu hawajui lipi ni lipi. Wahenga waliona mbali waliposema wanawake hawafai kuwa viongozi wa juu kabisa wanavuruga vichwa. Wapi katiba imesema cheo cha Rais kitakaimiwa na watu wawili kwa wakati mmoja! Hii nchi kwa awamu hii inaendeshwa na maafisa usalama tu ndio maana mvurugano kila kona.
 
07 September 2026
1788947037573.png

Mke Kukaa Eda Ya Kufiwa Na Mumewe​

More info :

UFAFANUZI KWA MUJIBU WA KORAN
Sheikh Muhammad Mahdi-shushtari Mke Kukaa Eda yakufiwa Na Mumewe
Mwanamke mwenye kufiwa na mume kama hana mimba eda yake ni miezi minne (4) na siku kumi (10), na kama mwenye mimba eda yake mpaka azae, lakini iki wa amezaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi lazima akae eda hadi zipite, siku hizo.

Mwanamke mwenye eda ya kufiwa na mumewe, ni haramu kuvaa nguo za rangi; kujipamba kwa namna yo yote kwa mwili au kwa nguo kama kujitia manukato, kutia wanja machoni, mapodari, hina na kila jambo la kujipamba ni haramu kwake hata nguo nyeusi ikiwa ina nakshi au mkato wa kujipamba.

Eda huanzia siku ya kufa kwa mume ikiwa yupo hapo, na kama hayupo huanzia siku atakapopata habari hata kama kumepita muda mrefu sana. Katika muda huo wa eda hawezi kuposwa au kuolewa.

Uislamu unaamrisha unadhifu, basi wanaruhusiwa wanawake wenye eda kuoga kujisafisha na kuweka mwili safi, kukata kucha.

Anaruhusiwa kutoka nje kama ipo haja kama kununua mahitaji yake au kumwangalia jamaa au mgonjwa na kadhalika, asitoke nje paisipo na haja.

Tunaomba kwa Mola wetu atupe sote Twafiki ya kufuata maamrisho ya dini na kuepukana na yaliyoharamishwa au kufuata mambo ya Bida'a uzushi, usiona msingi.


IKULU


View: https://m.youtube.com/watch?v=HJ3J3lOtmo8
 
Back
Top Bottom