Je, Diamond ni "ROLE MODEL"

Je Diamond ni ROLE MODEL?


  • Total voters
    5
  • Poll closed .

SunStrong

Member
Jan 24, 2011
56
3
Diamond.jpg ​

Kipindi cha nyuma nilikua nadhani kila "superstar" ni "role model" hasa nilipokua nafuatilia sana habari za watu mbalimbali maarufu duniani.
Tanzania ukitaja Super Star huwezi kumwacha Diamond,

ni mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa tena kwa muda mfupi, Big Up Bro!

Lakini mwenendo na tabia zake za kubadili wanawake, kibaya zaidi picha mbaya zinazo zagaa mitandaoni na ukijaribu kuangalia pozi unagundua kabisa ilikusudiwa kupigwa. Mi ndhani hii si sawa, vijana wengi sasa naona wanataka kuwa Maarufu ili wapate wapenzi wengi. Hili limenipa shida kuamini kama kweli Diamond ni "ROLE MODEL"
 
Tatizo umeshahukumu badala ya kuleta hoja ili watu watoe maoni yao! Kuna utofauti kati ya STAR na ROLE MODEL....sijui kwa uelewa wako unachukuliaje maneno hayo mawili! Mwisho wa siku nimegundua ww ni wale mnaofanya juhudi ya kumshusha huyu do go, hakuna hata picha moja ambayo ni mbaya...je unamfahamu KIM KARDASHIAN? kapiga picha uchi kabisa je si ndiyo utakufa kabisa! Na bado watoto wakimarekani wanamuona ni role model wao...ACHA CHUKI BINAFSI
 
Acha ubutu wa mawazo, kwa hiyo wamarekani wakifanya upuuzi wewe una_support tu coz ni wamarekani. Mimi diamond namkubali sana mungu anajua na ningepata nafasi ya kumshauri ningemshauri. Na hapa nasikiliza "song zake"
 
Huyu siku hizi anajichubua tofauti na domo aliyekua anakaa tandale usiniambie kung'aa Sean didy combs yupo vile vile
 
Si wanasema msanii ni kioo cha jamii!

Nani anasema hivyo? Kwa kanuni gani?

Na kama jamii yetu inaruhusu ufuska kiasi cha wabunge kama kina John Komba kufanya ufedhuli na watoto wadogo kina Lulu, huyu Domo akiakisi mwanga wa jamii hii na kuwa role model wa ufuska na umaaluni utamlaumu vipi?

It is wrong to expect Diamond to be a role model.

Just as it is wrong to look up to Diamond as a role model.

Whatever happenned to institutions such as the family, academia, faith etc?

Even the Americans, the ones we imported this celebrity worship culture from, do realize that artists and celebrities have no obligation to be role models.

In fact, expecting artists to be role model is curbing their artistic license and inspiration for creativity.

You guys are looking for role models in the wrong places.

Of course I know, that I'm a role model
But yo this rap life is real life sometimes it's full throttle
Right now I gotta think about me https://jamii.app/JFUserGuide the industry
You gets no love, except those who support me
What's the story, what happened when I went to L.A.?
Mixin shit up, no not there I got family
Nothin happened, mind your business yo step
You know we connect, JFK 2 LAX

Gangstarr, JFK 2 LAX
 
Nani anasema hivyo? Kwa kanuni gani?

Na kama jamaii yetu inaruhusu ufuska kiasi cha wabunge kama kina John Komba kufanya ufedhuli na watoto wadogo kina Lulu, huyu Domo akiakisi mwanga wa jamii hii na kuwa role model wa ufuska na umaaluni utamlaumu vipi?

Kwani wabunge ni wasanii? sijawahi kusikia kuwa mbunge ni kioo cha jamii.
 
Kwani wabunge ni wasanii? sijawahi kusikia kuwa mbunge ni kioo cha jamii.

Mbunge anatakiwa kuwa kioo cha jamii kuliko msanii.

Kwa sababu.

1. Mbunge kachaguliwa na jamii kuwekwa kwenye muhimili wa kuwatungia sheria
2. Mbunge anawakilisha jamii katika muhimili huo.

Msanii hajachaguliwa kupewa dhamana ya umma kama hiyo, na wala hawakilishi jamii kihivyo.

Sasa Diamond akiamua ku embrace the decadence of dadaism kwa sababu artistic inspirations zake ndivyo zinavyomuelekeza hivyo, utataka kumzuia asijinafasi anavyojisikia mwenyewe?

Kwa msingi gani? Role model? Alikuomba kuwa role model?

Kashindwa Jakaya Kikwete kuwa role model, mtu aliyezunguka nchi nzima kuomba kura za wananchi.Ukimtaka Diamond aliyefika hapo kwa kubangaiza bangaiza mwenyewe tu awe role model utakuwa umemfanyia haki?
 
Kuweni role models kwa wanenu na ndugu zenu.

Msitwishe wengine majukumu yenu.

Watu wanakariri sana.

Waiambiwa "Msanii ni kioo cha jamii" basi washajiridhisha awe role model.

Bila ya kujua wengine wanachotaka ni kumpata demu kama Zari the Bosslady, na Diamond akishawaonyesha mbwembwe za kuwa na Zari tayari kashakuwa role model wao.

Jamii is not monolithic. This idea of a monolithic more is a fiction.
 
Back
Top Bottom