Je Cremation Ni Mbaya?!

Je Cremation Ni Mbaya?!

Kifupi turudi vitabu vya dini vilivyosema hizi gharama za misiba ya sifa tutaiepuka, siku hizi msibani budget mpaka ya mziki ipo dah sad sana.

Nashukuru wazazi wangu kunikuza katika imani ya kiislam na nikifa nizikwe kiislam no kulala kwenye friji, no majeneza, no muziki,no misafara ya magari In Sha Allah
 
Hii tabia ya kuchoma miili moto iendee huko huko walikozoea. Maana utajisikiaje mtoto wako uliempenda anateketezwa kwa moto?! Bora nimtupe aliwe hata na ndege kuliko kumteketeza kwa moto. Hii tabia ikija huku itaongeza uchungu na maumivu kwa wafiwa.
 
Kwakweli mimi swala la kunichoma na moto silitaki kama wamenichoka sana bora wanitupe tu kuliko kunichoma na moto...
What if mtu akifa anakuwa anasense maumivu (maana hakuna mtu aliyewahi kurudi kutoka kifo akwatwambia ukifa unakuwaje)

Mimi kunichoma hapa aiseh tutamaindiana na mtu nikifa akatoa wazo la kunichoma
Logic yako ni dhaifu sana, kwani ukioza si wadudu wanakukula...je unakuwa hauhisi maumivu? Inabidi tuchomwe tu...maeneo ya kuzikiia yanaisha sasa
 
  • Thanks
Reactions: Ctr
Mbona nikifa sijitambui so laia watakalo amua kunistili kwangu poa tu
 
Ungependelea Mwili wako upitie hali ipi siku ya kifo chako, Udongoni au kwenye moto mkali

Nimekuwa na huu mjadala na baadhi ya marafiki wangu wa karibu kwani tupo katika Mazingira ya hospitali na tunaona watu wakija kuchukua miili ya wapendwa wao kwa ajili ya mazishi

Ila kwa sasa Mazishi yameanza kuwa ya gharama kubwa na pesa nyingi zinatumika katika Procedure nzima ya burial ( Kama umeona mazishi ya siku hizi)

Baada ya kuona haya ilifika mahali tukahoji swala la Cremation,... Je ni kosa au vibaya kumchoma mtu mpaka kuwa jivu (disposing corpses by burning them to Ashes)

Cremation kwa kuangalia inapunguza unnecessary costs za msiba ukizingatia wengi sasa wamefanya mazishi kuwa njia ya kipato.

Je kisheria mtu ana haki ya kuchagua cremation kama njia ya burial ikitokea amefariki?!

Baada ya cremation wahusika wa marehemu uchukua jivu(ashes of the deceased); Wengine urushia lile jivu baharini, wengine utafuta chungu(pot or urn) na kuweka hii jivu kama njia ya kumbukumbu

Wengi wanaoachagua cremation over burial ni wale ambao wanachukia ile fact ya kuoza kwa mwili.

Labda Nijue kwa Wengine kama Swala la Cremation ni swala sahihi na je wewe ungependa mwili wako upitie huduma gani ukifa?!
Mimi nachagua cremation, kisha jivu langu walipukutishe tu hewani, nahisi nafsi yangu otakuwa huru zaidi napunga hata hewa. Kitendo cha kufukiwa chini peke yangu kisha naachwa hapo siwezi toka inaniba hisia mbaya, nahisi nitalia sana nikiomba msaada nitolewe ila hamna wa kunisaidia. Ni upweke wa milele.
Cremation kwa tanzania ikatokea mtu kachagua inawezekana?
 
Kabisa ni maamuzi yako ata ukitaka baadhi ya viungo vyako vitolewe
 
Ni wazi kabisa kuwa misiba ya kimagharibi ni gharama mno na inapoteza sana rasilimali,mara mbao sijui vyuma sijui zege yaani ujinga ujinga tu.Mimi nikifa bora tu nichomwe moto,kwanza inasaidia kuokoa maeneo,wenyewe mnaona sikuizi jinsi viwanja vya makaburi vinavyojaa.

Ila kuna wanasayansi wa Italia wamegundua mbinu nyingine ya kuzika maiti,unazikwa kwenye kitu chenye umbo la yai ukiwa umewekwa position ya mtoto kwenye tumbo la uzazi,halafu hapo juu unapandwa mti.hiko chombo kimetengenezwa kwa material ambazo zinaoza haraka.Kwa njia hii naona ntakua naendelea kuishi nikiwa kama mti,sababu mti utakula virutubisho vinavyo tokana na kuoza kwa mwili.

Hii itapendeza sana,kwani sasa makaburini kutageuka msituni na kusababisha utengenezwaji wa mvua.

Kwa undani zaidi soma Biodegradable burial pod turns your body into a tree - CNNView attachment 806217
Pia ndugu au jamaa zako wakiuona huo mti wanakua kama wamekuona wewe
 
Ungependelea Mwili wako upitie hali ipi siku ya kifo chako, Udongoni au kwenye moto mkali

Nimekuwa na huu mjadala na baadhi ya marafiki wangu wa karibu kwani tupo katika Mazingira ya hospitali na tunaona watu wakija kuchukua miili ya wapendwa wao kwa ajili ya mazishi

Ila kwa sasa Mazishi yameanza kuwa ya gharama kubwa na pesa nyingi zinatumika katika Procedure nzima ya burial ( Kama umeona mazishi ya siku hizi)

Baada ya kuona haya ilifika mahali tukahoji swala la Cremation,... Je ni kosa au vibaya kumchoma mtu mpaka kuwa jivu (disposing corpses by burning them to Ashes)

Cremation kwa kuangalia inapunguza unnecessary costs za msiba ukizingatia wengi sasa wamefanya mazishi kuwa njia ya kipato.

Je kisheria mtu ana haki ya kuchagua cremation kama njia ya burial ikitokea amefariki?!

Baada ya cremation wahusika wa marehemu uchukua jivu(ashes of the deceased); Wengine urushia lile jivu baharini, wengine utafuta chungu(pot or urn) na kuweka hii jivu kama njia ya kumbukumbu

Wengi wanaoachagua cremation over burial ni wale ambao wanachukia ile fact ya kuoza kwa mwili.

Labda Nijue kwa Wengine kama Swala la Cremation ni swala sahihi na je wewe ungependa mwili wako upitie huduma gani ukifa?!
 
Lakini mkuu sayansi inatutanabahisha mafuta na gas vinatokana na mabaki ya viumbe hai waliokufa miaka mingi iliyopita, tukichomana Moto itakuwaje dunia ijayo si watakosa wese ....
 
Ukija kwenye issue ya Cremation nahisi sio njia sahihi ya ku-dispose corpes, pia si agizo la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema wafu wachomwe Moto( maana biblia inasema mavumbi yatairudia nchi na roho itarudi Kwa Mungu aliyoitoa, sijaribu kupinga taratibu na Imani ya mtu yeyote.

Ukiangalia soil composition is compactible to body composition by 99%. Minerals,organic na matter zinazopatina kwenye udongo ndizo zinazopatikana kwny mwili wa binadamu.

Kwahiyo Kwa hitimisho, ardhi ndio sehemu mahususi ya kumuhifadhi mfu, kwakua anarudi kuwa udongo Kwa asilimia zaidi ya tisini. Mengine yote aliyoyafanya yataletwa hukumuni siku Mola wake akimfufua tena.
 
Mkuu Hili Pia Nilitaka Kulizungumzia

Kuliko kuacha Macho yaoze, Figo zioze, Mapafu yaoze mbona watu wasingekubali kwamba viungo ivi vitolewe sadaka kwa waliohitaji

Lakini kama unavyosema 'IMANI' zimetufunga pia tunaamini kwenye kuzikwa na kuoza na kila kitu

Wazo zuri sana Mkuu

Una uhakika gani kama huwa hawatoi baadhi ya viungo kwa maiti
 
Hata mwili wako ukichomwa haimaanishi ndo umekwepa adhabu ya moto wa jehanamu aka mauti ya pili, uchomwe uzikwe ardhini , adhabu ya siku ya mwisho iko pale pale
 
Kwa wale wasiojua cremation ninini ......ni kuchoma moto mwili wa mfu kulingana na tamaduni husika
Binafsi naipenda kwakuwa tunaipunguzia ardhi kuilisha uozo na uvundo laana na mabalaa

Kwa mtu eliyekutwa na kifo cha asilia (natural causes) cremation inaweza kuwa njia rahisi ya kuzika katika maeneo ambayo makaburi yana gharama kubwa. Ila katika mazingira ya kutatanisha, cremation huweza kuondoa ushahidi ambao ungepatikana baada miaka kupita. Ukifuatilia vipindi vya Foresinc Files, utaona kuwa kuna kesi kadhaa ambapo wahalifu hugunduliwa baada ya kufukua maiti na kuifanyia uchunguzi tena kufikia kun'gamua kuwa walilishwa sumu makusudi.
 
mimi wauchome tu wachimbe shimo waoteshee mgomba jivu liwe mbolea
 
Mimi binafsi nafikiri ni njia nzuri yakuyalinda mazingira,...
Cremation ni njia nzuri sana na inaokoa gharama na kupunguza matumizi mabaya ya ardhi
Unailinda ardhi ikusaidie nini ikiwa utakuwa umekufa
 
Kwa wale wasiojua cremation ninini ......ni kuchoma moto mwili wa mfu kulingana na tamaduni husika
Binafsi naipenda kwakuwa tunaipunguzia ardhi kuilisha uozo na uvundo laana na mabalaa
Hiyo kiroho, kisayansi bora kuzika ardhini
 
Back
Top Bottom