TheCrazy Mchokozi
Senior Member
- Apr 7, 2017
- 181
- 252
- Thread starter
- #21
Nafikiri hapa umeleta nadharia nzuri ya burial...Ni wazi kabisa kuwa misiba ya kimagharibi ni gharama mno na inapoteza sana rasilimali,mara mbao sijui vyuma sijui zege yaani ujinga ujinga tu.Mimi nikifa bora tu nichomwe moto,kwanza inasaidia kuokoa maeneo,wenyewe mnaona sikuizi jinsi viwanja vya makaburi vinavyojaa.
Ila kuna wanasayansi wa Italia wamegundua mbinu nyingine ya kuzika maiti,unazikwa kwenye kitu chenye umbo la yai ukiwa umewekwa position ya mtoto kwenye tumbo la uzazi,halafu hapo juu unapandwa mti.hiko chombo kimetengenezwa kwa material ambazo zinaoza haraka.Kwa njia hii naona ntakua naendelea kuishi nikiwa kama mti,sababu mti utakula virutubisho vinavyo tokana na kuoza kwa mwili.
Hii itapendeza sana,kwani sasa makaburini kutageuka msituni na kusababisha utengenezwaji wa mvua.
Kwa undani zaidi soma Biodegradable burial pod turns your body into a tree - CNNView attachment 806217
Mazishi hayafai kuwa gharama na pia yanafaa kutunza Mazingira
Hao wa Italy kwa Mfano wanapunguza matumuzi mabaya ya miti kuchonga majeneza( Umuhimu wa Jeneza Ni Nini) na pia wanatunza mazingira
Mfano Kumzika mtu nyumbani na kutengeneza kaburi kwa zege na mapambo lukuki inaonekana kama tumemuenzi Ndugu yetu ila baadae eneo ili litakuwa gumu kufanya nalo biashara au kuwa pendeleo la watu kuishi
Kwa sasa nafikiri kuchomwa sio vibaya
