Je, COVID19 ni maandalizi ya silaha za kibaolojia? Kama sivyo, je haziwezi kuja kutumika kama silaha ya maangamizi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Hebu tuwe na mjadala tofauti kidogo na huu ugonjwa wa corona maarufu kama COVID19.

Tuanze na tabiri mbali mbali.Kuna machapisho na makala yaliyotabiri huu ugonjwa hapo kabla na sasa imetokea kama utabiri ulivyotabiri

Je, hizi tabiri zilikuwa za kweli ama ni mipango ya muda mrefu ya wale waliotutangulia kufikiri? Kwa maoni yangu tabiri husika zilikuwa sahihi na si mipango ya wachache tunaowahisi kwakuwa wao ndio wahanga wakubwa kwenye hili.. Na kuna maono na nguvu ya ajabu kwenye huu utabiri

Aina za corona
Tunaambiwa kuna aina zisizopungua 20 za corona na karibia kila mtu ana aina mojawapo ya vimelea vya corona. Lakini corona AKA COVID19 ndio ndio mbaya sana na inayoisumbua dunia kwa sasa.. Kwenye utabiri iliitwa COVID19. Na ikatokea mwaka 2019. Je, hii ni coicedence ama ni tukio la kupangwa? Kama ni tukio la kupangwa. Je, ni nani kalipanga? Kwanini? Kwa maslahi gani? Kwanini 2019 na si mwaka mwingine wowote?

Mkanganyiko wa aina ya vimelea. Nimesoma kuna mojawapo ya makala inaelezea huu mkanganyiko kwamba je kimelea chake ni kirusi ama ni bacteria? Je, ni nini kinaeneza kwa njia ya hewa kati ya kirusi na bacteria? Je, ni nini kinaeneza kwa njia ya kushikana kati ya kirusi na bacteria?

Makala za siri zilizovuja
Ukweli ni upi kwamba kirusi/bacteria wa corona kilitengenezwa China kwa nia ya kuwaambukiza waandamanaji wa Kong Kong ili kudhuru ufahamu wao na wapoteane kwa kuugua? Na kwamba Mmarekani alistukia hiyo ishu na kumuomba mchina formula yake kwa matumizi yake ya baadae na mchina akagoma? Lakini mmarekani akatumia ulaghai kupitia majasusi wake na katika harakati za kupata kichupa chenye MBEGU Wachina wakastukia na kwenye kukigombea kikaanguka kikamwagika na kuleta hili janga.

Conspiracy ni nyingi kwenye hili lakini pia tunajua maslahi ya mmarekani pale Hong Kong na hujuma plus figisu anazofanya ili maandamano husika yalete matokeo tarajiwa.

Kutafuta mchawi
Tayari mataifa mawili yenye nguvu kubwa duniani mmarekani na mchina wameshanyoosheana vidole sana.. Kila mmoja akimtuhumu mwenzake kama chanzo na tayari hata kabla hali haijatulia mawakili wa Marekani wameshalimbilia mahakamani kumfungulia mchina shauri la madai ya uzembe na fidia ya dola trillion 20.

Ukweli ni upi kuhusu corona
Kuna vyanzo vinasema wanachougua watu sio corona bali ni kitu kingine kibaya kabisa ila ukweli unafichwa hasa na mchina na wanasema habari zinazoripotiwa ni tofauti kabisa na uhalisia.. Kwa mfano China inasemekana waliokufa ni mamilioni... Rejea mada ya laini million 21 zisizopatikana huko China baaada ya ugonjwa kupiga
Kwasasa ukweli ni vigumu kuujua na itachukua miaka na pengine hata karne pale wahusika watakapojitokeza hadharani na kuomba radhi.. Lakini bythen zitakuwa ni habari mfu

Sasa kitisho ni nini?
Kitisho kikubwa kilichopo mbele yetu sio corona ya sasa bali corona itakayorudi.. Corona inatayokuja kivingine.. Corona itakayobamiza Afrika. Kitisho kikubwa ni hapo mbeleni upgraded COVID19 iliyoboreshwa itakapotumika kama biological weapon. Kama silaha za maangamizi kwa adui.

Pale COVID19 iliyoboreshwa kama silaha ya kivita kwa bei ndogo salama na isiyo na hasara. Tumeshuhudia vifo vinavyofikia mia 800 kwa masaa 24 tuu huko Hispania na Italy. Hii ni idadi kubwa mno ya vifo kwa siku moja kwenye uwanja wa vita inayohitaji vifaa vingi vya kijeshi na hasara kubwa na gharama kubwa.

Kitisho na hofu kubwa ni pale corona iliyoboreshwa formula yake itakapodakwa na magaidi na vichaa wa hii dunia. Kwasasa watu wako busy maabara wakijaribu kutengeneza tiba na kinga ya COVID19. Ni katika mchakato huo bila kujua ama kwa kujua wanaumba kitu kingine kikubwa zaidi kibaya zaidi. Yaani wasumbufu hawatapigwa maroketi tena wala mabomu bali wataangushiwa tu kichupa kidogo chenye vimelea vya corona iliyoboreshwa na baada ya hapo itakuwa tu kuokota maiti.

Corona itarudi baada ya miaka 10. Hapa ndio ule utabiri wa bilionea Bill Gates utatimia. Utabiri wa kuangamiza waafrika million 10 kupitia huu ugonjwa. Na muda huo ukifika watakaokufa kwa wingi sana ni waafrika. Ambao pia ni rahisi mno kuwawekea quarantine wasitoke nje ya bara lao. Wakati huo wenzetu hawa wanaokufa leo kama kuku wa kideri watakuwa wameshajua chanjo na kinga na hawatakuwa tayari kuitoa Afrika na kama watakubali ni kwa masharti magumu mno.

Tuwacheke sasa. Lakini kilio chetu hakiko mbali. Tuziishi hizi nyakati lakini kiama kinakuja. Tukutane 2030



Jr
 
Tuwacheke sasa.. Lakini kilio chetu hakiko mbali... Tuziishi hizi nyakati lakini kiama kinakuja
Hapana mkuu mimi nakataa hili, nikitumia reference ya maandiko takatifu Hakuna ajuaye mwisho wa uhai wa binaadamu. Kiama kitakuja kama mwizi ajavyo labda kama unatafsiri kiama ni vifo vya watu wengi kwa muda mchache. Mwisho wa dunia hatutaweza kuuhisi kua ndio huu unakuja.

Lakini pia Hata iweje hakuna mtu anaweza kufuta uhai wa mwanadamu hapa duniani sana watu watakufa wengi unless aloye initiate uhai aamue kua ndio iwe mwisho wa uhai.

Mkuu hakuna haja ya kutishana sijui huu ni mwisho wa dunia wala nini Death is Fate..Kama fate yaki ndio muda huu utakufa tu hata kama sio kwa Corona. Btw tunaishi lwa imani siku zote kua tutaiona kesho na imani hiyo yatupatia neema ya kuifika kesho. Upande wangu nina imani na malaika wangu wanilindao. Hawajaacha kunilinda, nitakufa kama ndio muda wangu unefika.

Hakuna haja ya kuhofia na kutishana kua ndio mwisho wa maisha.
 
Asante Denvers kwa mchango lakini hakuna nilipozungumzia MWISHO wa dunia. Neno KIAMA nimemaanisha janga kubwa
Hapana mkuu mimi nakataa hili, nikitumia reference ya maandiko takatifu Hakuna ajuaye mwisho wa uhai wa binaadamu. Kiama kitakuja kama mwizi ajavyo labda kama unatafsiri kiama ni vifo vya watu wengi kwa muda mchache...Mwisho wa dunia hatutaweza kuuhisi kua ndio huu unakuja.

Lakini pia Hata iweje hakuna mtu anaweza kufuta uhai wa mwanadamu hapa duniani sana watu watakufa wengi unless aloye initiate uhai aamue kua ndio iwe mwisho wa uhai.

Mkuu hakuna haja ya kutishana sijui huu ni mwisho wa dunia wala nini Death is Fate..Kama fate yaki ndio muda huu utakufa tu hata kama sio kwa Corona. Btw tunaishi lwa imani siku zote kua tutaiona kesho na imani hiyo yatupatia neema ya kuifika kesho..Upande wangu nina imani na malaika wangu wanilindao. Hawajaacha kunilinda, nitakufa kama ndio muda wangu unefika.

Hakuna haja ya kuhofia na kutishana kua ndio mwisho wa maisha

Jr
 
deal done .....

Maneno yalisikika sehemu yakitamkwa kwenye kikao kimoja cha siri yakisema " Human extiction is easy if we consider bioweapon which alters hypoxic respiratory failure" Wakimanisha ""kukiteketeza kizazi cha mwanadamu ni rahisi kama tutacontrol uwezo wa kupumua.""

Kumekuwa na majaribio kadhaa kuhusu namna ya kufanya total(direct or indirect )human being extinction ambapo majaribio kadhaa yamefanyika katika nchi mbali mbali Uchina na Marekani mpaka kufikia hatua ya kufanya gene cloning au human cloning kwa ajili ya kufanya majaribio ya jinsi ya kuua mwanadamu kwa kutumia bilogical weapons ( mwanadamu sasa hivi anatumika kama trial ya madawa na bioweapon na sio wanyama kama hapo zamani).. wale jamaaa ni mwisho kabisaa

Je, ni kweli wale jamaaa ( people X) wanaweza tengeneza Selective antidote kwa ajili ya kufanya extinction ya kizazi flan halafu ikawa total life sparing kwa kizazi kingine?

Kwa mfano kama wanataka kuangamiza watu wote wenye kirusi X cha Ugonjwa flani kwa kutumia special antidote check below



Wanachokifanya ni kwamba, wanatengeneza aina flan ya kirusi, let's say kirusi X kisha wanakiachia kwenye jamii kinakaanga watu miaka 20 huku wakipotosha hakuna dawa yake ila kuna dawa za kukipoza tu then watu wanaangamia wengi kisha ukifika muda flani lest's say miaka 30 wanataka kubadili mfumo wa kubakiza aina flani ya race, age group au upigaji mwingine wa pesa though kwao pesa sio inshu coz mfumo wa pesa ndo waliubuni wao wenyewe kwa ajili ya kumotor service zote kwa mwanadamu .So kupitia kirusi X walichokiachia kwa miaka flani watatengeneza aina flan ya antidote ambayo inakuwa na aina mbili ya ufanyaji kazi.

1) Antidote itakuwa na fatal effects kwa mwenye kirusi X

2) Antidote itakuwa na life sparing mechanism kwa mtu ambaye hana kirusi X

What does it mean?

Kama wanataka kufanya total extinction ya watu wenye kirusi X watatoa hiyo antidote ambayo kwa kila mwenye kirusi hicho atakufa mara moja pindi apatapo hiyo antidote na kwa yule ambaye hana kirusi hatapata madhara yoyote ...

Lakini how do they generate and distribute hiyo antidote kwenye jamii ikiwa wanataka kufanya extinction ya jamiii ya kundi la watu flani?

Wanachokifaya ni kutengeneza new controllable kirusi ambacho kitakuwa na uwezo wa kuua watu wengi ndani ya muda mfupi ili kilete hofu kwenye jamii na kisha wao kutangaza kinga ya kirusi huyo mpya ambapo kila mtu atakimbilia chanjo hiyo mpya lakini ndani ya hiyo antidote watakuwa wameshaicoate( pandikiza) antidote yenye mechanism ya kuleta fatal effects kwa mwenye kirusi X

....umepata kitu hapa???

Kwa mfano wanataka kufanya total extinction ya watu wote wenye homa ya inni kwa kuwatengenezea special fatal antidote( Chanjo yenye kuleta madhara) ,watatengeneza kirusi mwingine mwenye madhara makubwa ndani ya muda mfupi kisha kutengeneza antidote yake ambayo kila mtu atakimbilia kuchoma lakini ndani ya antidote hiyo kutakuwa na added fatal antidote ambayo itakuwa lethal effects kwa yoyote mwenye homa ya Ini

Did you get something ??

Chukulia corona kama new antidote spread to the atmosphere but ni selective kwa watu wenye aina flani ya kirusi au ugonjwa flani au race au age group flan at the same time ikawa na life sparing mechanism kwa watu wa aina flani( Its just targeted kwa aina flani ya watu)

Tunajua homa ya ini ni aina flani ya kirusi wanaoshambulia na kufanya total hepatic parencyma changes kisha ini kufeli kabisa, but kuna aina nyingi sana za virusi na kila kirusi anaweza kuwa na effect ya organ moja tu. It's just an example, usibase sana na mfano wa homa ya ini.

Probably, corona is a type of fatal antidote kwa ajili ya kufanya extinction ya aina flani ya age group, gender ,race etc but its mechanism of fatality being hidden with highly prohibition laws.

Its a new game of making total replacement and total extinction ya aina flani ya jamii kwenye ulimwengu wa dunia ya tatu.

Ndo mana kuna mtu mmoja alisema hizi chanjo (Antidote) tunazokimbilia kupewa ipo siku zitaonesha madhara yake.

Questions to ask at your self....

1) Kwanini kirusi hiki kiwe selective kwa baadhi ya jamii hasa race, color and sometimes age group? why?

2) Does it mean kilianzia China then kikaenda italy kuonesha madhara makubwa kiasi kwamba kwingine bado hakijaja kwamba mode of spread kwa china ipo tofauti na Italy au Spain?

If at all ,mechanism ya kuspread ni ile ya hewa na njia ya kugusana kwanini Itally kimejikita zaidi ya nchi chache kama spain and sparing most of african race?

3) Does it mean black people are more civilized kwenye upande wa decontamination kuzidi wale jamaa weupe?

Kuna kitu hapa kinasukwa au kimelenga kufanya extinction ya aina flan ya race

Hawa jamaaa hawashindwi kutengeneza bioweapon yenye uwezo wa kuangamiza ukoo mmoja tu duniani unanaweza amini ukweli huo kwa asilimia flani.

CDC ambayo inacontrol maambukizi na magonjwa wapo kimya mpaka leo hawataki kutoa tamko lolote means kuna kitu kwenye hii kitu.

But Itally na Spain ndo zinatoa idadi kubwa ya watu wenye maamuzi kwenye mabalaza ya haki za kibinadamu na huenda they have been targeted so far with the new engeneered fatal antidote ambayo imepewa jina hilo la COVID -19 ambayo inapewa tafsiri kibao kuficha ukweli na uhalisia wa jinsi inavyoua ...does it mean hizo Ndo nchi zilizokuwa zinaongoza kutoa laws kandamizi kwa baadhi ya nchi zingine duniani)?

Question to think ....

Wenzetu kule mbele wana maabara ambazo zina mashine zinazobeba reagents zaidi ya 500 ambapo kila reagent inaweza tambua na kureact na kirusi au bacteria ambaye ashakuwa known kwa muda mrefu kisha kutoa majibu ya postive au negative pale pale manake nini, kama wakichukua sample ya blood yako wakaiweka kwenye mashine inadetect aina zote za infections za virus au bacteria ndani ya nusu saaa.

Ndo mama milipuko kama hii ya corona wanachukua sample ya mtu wa kwanza kisha kuiingiza kwenye mashine hizo kisha zina Ideantify kama ni mlipuko mpya wa bacteria Athransis ambaye aliwahi kuexist miaka hiyo au laaa kisha watu kupewa tahadhari.

But mashine hizo zinafichwa kwa siri sana kiasi kwamba ni ngumu kuwekwa wazi, but hakuna linaloshindikana hata siku moja ..

hizo blah blah eti wanajaribu kutengengeneza chanjo ni uongo wa hali ya juu kwa wanaojua mambo vizuri , they are trying kujiweka kwenye kundi la watu but themselves being with their own target.

My concern: Kama watatangaza antidote ya Corona basi its going to be one of the fatal antidote kwa kuja kufanya extinction ya watu wa aina flani na watakuja kufa kama nzige.

This game is being played by highly intelligent people ambao kujua mipango yao ni mpaka miaka 50 ndo utasikia habari za ajenda zilizotimilika miaka mingi iliyopita.

Be conscious with this movie ahead on us.
 
Mshana Jr,

Thread yako umehitimisha kinyonge sana. Ni kama vile waafrika hawakuumbwa na bongo za kufikiria. Wao kazi yao ni kusubiri wanaume wana Magharibi wakae maabara kutafuta dawa.

Waafrika tuamke sasa. Tuache kujikuta victims kwenye kila tukio.

Waafrika wanapenda kuji treat kama watoto yatima yaani wanaona wana haki ya kuonewa huruma na kila mtu na wala hawahangaiki kuboresha ustawi wa maisha yao.
 
Sio silaha ya kibaolojia na haziwezi kutumika kama silaha za maangamizi.

Wakati sisi tunaendelea kujadili utopolo wa aina hii wenzetu wako wanakesha maabara wakitafuta chanjo kwa ajili yao ila ikipatikana watatupatia na sisi waswahili pia kwa hisani yao kama msaada ili kuifanya dunia kuwa angalau sehemu salama na tulivu kwa biashara zao na maslahi mengine mapana zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kila Africans aliyejaribu kuamka watu weupe wanatupora na kisha wanapewa paradiso wanasahau nyumbani wametuecha kinyonge!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo na nyinyi waafrika mmewapa kipaumbele sana wanasiasa ndio maana watalaamu mbalimbali kama hapa Tanzania wanaingia kwenye siasa ili wapate pesa za bwerere.

Ni wakati muafaka sasa muwekeze kwenye rasimali watu kikamilifu.

Unafikiri kama wewe ni daktari bingwa ulitebobea halafu serikali inakuelea magumashi kwenye malipo utaendelea kufanya hiyo kazi ya kibwege?
 
Inasikitisha sana tulichobaki kukifanya kwa ustadi mkubwa ni kuchimba na kutengeneza absurd consiparicies theories.
Thread yako umehitimisha kinyonge sana. Ni kama vile waafrika hawakuumbwa na bongo za kufikiria. Wao kazi yao ni kusubiri wanaume wana Magharibi wakae maabara kutafuta dawa.

Waafrika tuamke sasa. Tuache kujikuta victims kwenye kila tukio.

Waafrika wanapenda kuji treat kama watoto yatima yaani wanaona wana haki ya kuonewa huruma na kila mtu na wala hawahangaiki kuboresha ustawi wa maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa technology ilivyo kwa sasa ni sahihi kusema hiki kirusi cha COVID19 ni kirusi cha maabara. Toka uanze huu ugonjwa nimeamini 100% kwamba ni kirusi cha maabara.

Kwa sababu tu ya njia kilivyoundwa. Kwanza kulenga kwake kuua watu wengi kwa njia za kushikana tu. Halafu kirusi kinaweza kukaa sehemu isiyo mwili wala damu kwa siku mbili. Mfano mtu ameshika sehemu ya sit za ndege mwenye kirusi,kinaweza kuishi hapo kwa siku mbili.

Na kufa kwake kinakufa nusu nusu,mtengenezaji hapo alikusudia kiimpate tu mwingine. Na humo kwenye usafiri wa ndege na mabasi ya umma kwa sehemu zilizoathirika zaidi kama china,Italy na Spain huko ndio wengi wameambukizwa.

2. Mimi nafikiria USA alikiunda ili kumpunguza speed mchina kiushindani. Hasa ktk uchumi. Maana mpaka sasa uchumi wa chini umepigwa na ukapigika. Japo uzuri wa Wachina, soon watarudi sawa,ksbb ya uchapakazi wao. Wanaushirikiano kama mchwa.

3. Kuhusu vifo China nina uhakika wamekufa mamilioni ya watu. Mengi yamefichwa. Na ujuavyo nchi ya China ina usiri mkubwa sana likaja swala ambalo hawataki kulitoa nje. Ni USA tu ndio wanaweza kujua takwimu halisi, KSSB wana majasusi wao humo ndani ya China.

4. Kwa technology inavyotamalaki ktk dunia ya sasa USA wanafikiria kuachana na vita vya kutumia mabunduki. Wanataka mtu mmoja tu anaweza akakaa ofisini kupigana na nchi nyingine umati wa jeshi lingine bila madhara yoyote. USA kwanza alianza vita vya kupigana nje ya mipaka yake,yaani anapigana na nchi wala hapakani nayo. Pili akaja na ndege zisizotumia rubani. Hiyo yote ni kujaribu tu kuwalinda raia wake na wanajeshi wake. Hapo ndio anajaribu kufikiria kuunda sasa siraha kama hizi. Nafikiri hata lile tetemeko la ardhi karibu na kinu cha nukrea mwisho mwa mwaka jana huko Iran sidhani kama lilikuwa la asili,japo vile vile kama ni USA alihusika nalo,bado linaweza kuwa siraha hatari pia kwenye majaribio.

5. Kinachoumiza sana kwenye hizi siraha za kibaolojia kama hii COVID19 ni namna kinavyoua hata wasiohusika na hayo mapigano,tofauti na vita vya siraha za kawaida mnapigana kwenye uwanja wa vita,raia wa kawaida hawaingizwi humo kwa makusudi. Ona watu 800 kwa siku. Wote hao ni wale wasiohusika kabisa. Au maadam tu umekuja duniani unahusika. Je Africa?

6. HIV (UKIMWI),nafikiri pia ulikuwa mwanzo wa uundaji wa hizi siraha za kibaolojia. Japo hii iliundwa rasimi kwa ajili ya Afilrica, kuwawinda waafrica kuwamaliza taratibu,ksbb wanajua tulivyo. Kwa hiyo wanacheza na akili zetu

7. Na bahati mbaya sana kwa bara la Africa huyo ndio atakuwa mhanga mkubwa wa hizi siraha mpya za kibaolojia. Tunabaki kumtegemea MUNGU. MUNGU atunusuru tena na tena kama alivyotunusuru siku zingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
That's Africa my friend... Sijaona chochote cha serious kuhusu huu ugonjwa.. Tunachofanya ni siasa na blah blah nyingi.. Just msome lifecoded kuna kitu kaandika hapo juu kina ufunuo fulani usiosemwa
Thread yako umehitimisha kinyonge sana. Ni kama vile waafrika hawakuumbwa na bongo za kufikiria. Wao kazi yao ni kusubiri wanaume wana Magharibi wakae maabara kutafuta dawa.

Waafrika tuamke sasa. Tuache kujikuta victims kwenye kila tukio.

Waafrika wanapenda kuji treat kama watoto yatima yaani wanaona wana haki ya kuonewa huruma na kila mtu na wala hawahangaiki kuboresha ustawi wa maisha yao.

Jr
 
.
tapatalk_1585241974245.jpeg


Jr
 
Back
Top Bottom