Je, chama kikongwe kitatumia dodoki gani ili kisafishike kitakasike?

Je, chama kikongwe kitatumia dodoki gani ili kisafishike kitakasike?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,974
Reaction score
871,040
Je, mchafu anachafuka tena? Hapana!
Je, mchafu anachafuliwa tena? Jibu pia ni hapana.

Kutoka jina jema kabisa la chama cha wanaolima na wanaofanya kazi, kuendea majina mengine kama
Chama cha walafi
Chama cha chukua chako mapema
Chama cha majambazi mpaka chama cha mauaji/wauaji... Kuna kutakasika tena hapo!?

Achana na ile slogan ya Wagalatia kwamba ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu kama damu yeye (aliye juu) atazisafisha ziwe nyeupe kama theluji... Hili ni la kiroho zaidi, ni la kiiimani zaidi na ni la kininafsi zaidi.. Lina kitubio. Je chama cha mauaji kinaweza kutubu na kikatubika? Jibu ni hapana!
Uchafu ninini?

Uchafu ni kuweka kitu kisichostahili mahali husika. Kuna uchafu wa kimwili/kimazingira na kuna uchafu wa kiroho/ wa kiimani.. Haya ni makundi mawili makubwa ya uchafu.. Lakini vilevile kuna aina anuwai za uchafu
Uchafu unaweza kuwa ugonjwa.. Ugonjwa unaweza kutibika ama usitibike... Je uchafu wa chama pendwa unatiba!? Unatibika? Jibu pia ni hapana!

Kuna uchafu unaosafishika na kuna uchafu usiosafishika. Hata kwa kutumia kemikali kali kabisa.. Je uchafu wa chama tajwa unasafishika? Jibu ni lilile HAPANA.

Cheza na vyote lakini usicheze na hivi vitu viwili
Ardhi
Uumbaji

Hivi ni tunu za kimbingu alizotunukiwa mwanadamu... Fanya vyote lakini usiinajisi ardhi kwa kuimwagia damu isiyo na hatia.. Huu uchafu hausafishiki... Hii dhambi haina msamaha wa kimwili wala wa kiroho.

Usicheze na uumbaji kwakuwa hauna mbadala wala vipuri.. Kama kuna kitu kinapaswa
Kulindwa kwa nguvu zote basi ni uumbaji
Kuogopwa sana basi ni uumbaji
Kuheshimiwa sana basi ni uumbaji

Jina baya la CHAMA CHA MAUAJI limetokana na kutokuheshimu UUMBAJI wala KUULINDA wala KUUOGOPA!
Uumbaji haudhihakiwi kwa namna yoyote ile!

Chama kimefika ukomo wa dhuluma, ghiliba, mateso, wizi na kubwa kuliko yote. Mauaji... Hili doa halifutiki...!... Na kadiri kinavyoua ndivyo ladiri kinavyozidi kuharibu na kujichimbia kaburi kubwa.

Baadhi ya 'serial killers' walianza kwa kuua mashahidi ili wapone na kesi za mauaji zinazowakabili.. Lakini kila walivyoteketeza roho moja waliacha nyayo za ushahidi na kujikuta wanazidi kuua ili kupoteza ushahidi mpya!

Chama kimechafuka, kimenajisika na kinanuka damu za watu wasio na hatia. Hakuna dodoki wala kemikali iwayo yote inaweza kukisafisha, kukitakasa na kurudi kwenye asili yake!

Kuna muda najiuliza kuna raha gani ya kukalia kiti cha mamlaka ilihali kinanuka damu za watu? Je haiwezekani kutawala pasipo kuua mtu au watu ambao wanakupinga?..Hizi damu zinazomwagika hizi ipo siku zitanena juu ardhi kama ile ya habili iliyomwagwa. Mbona kuna nchi voongozi wao wanaishi na wakosoaji wao wa kisiasa pasipo kuuana?
 
Je mchafu anachafuka tena? Hapana!
Je mchafu anachafuliwa tena? Jibu pia ni hapana....

Kutoka jina jema kabisa la chama cha wanaolima na wanaofanya kazi, kuendea majina mengine kama
Chama cha walafi
Chama cha chukua chako mapema
Chama cha majambazi mpaka chama cha mauaji/wauaji... Kuna kutakasika tena hapo!?

Achana na ile slogan ya Wagalatia kwamba ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu kama damu yeye (aliye juu) atazisafisha ziwe nyeupe kama theluji... Hili ni la kiroho zaidi, ni la kiiimani zaidi na ni la kininafsi zaidi.. Lina kitubio... Je chama cha mauaji kinaweza kutubu na kikatubika? Jibu ni hapana!
Uchafu ninini?
Uchafu ni kuweka kitu kisichostahili mahali husika. Kuna uchafu wa kimwili/kimazingira na kuna uchafu wa kiroho/ wa kiimani.. Haya ni makundi mawili makubwa ya uchafu.. Lakini vilevile kuna aina anuwai za uchafu
Uchafu unaweza kuwa ugonjwa.. Ugonjwa unaweza kutibika ama usitibike... Je uchafu wa chama pendwa unatiba!? Unatibika? Jibu pia ni hapana!
Kuna uchafu unaosafishika na kuna uchafu usiosafishika. Hata kwa kutumia kemikali kali kabisa.. Je uchafu wa chama tajwa unasafishika? Jibu ni lilile HAPANA...
Cheza na vyote lakini usicheze na hivi vitu viwili
Ardhi
Uumbaji
Hivi ni tunu za kimbingu alizotunukiwa mwanadamu... Fanya vyote lakini usiinajisi ardhi kwa kuimwagia damu isiyo na hatia.. Huu uchafu hausafishiki... Hii dhambi haina msamaha wa kimwili wala wa kiroho..
Usicheze na uumbaji kwakuwa hauna mbadala wala vipuri.. Kama kuna kitu kinapaswa
Kulindwa kwa nguvu zote basi ni uumbaji
Kuogopwa sana basi ni uumbaji
Kuheshimiwa sana basi ni uumbaji
Jina baya la CHAMA CHA MAUAJI limetokana na kutokuheshimu UUMBAJI wala KUULINDA wala KUUOGOPA!
Uumbaji haudhihakiwi kwa namna yoyote ile!

Chama kimefika ukomo wa dhuluma, ghiliba, mateso, wizi na kubwa kuliko yote... Mauaji... Hili doa halifutiki...!... Na kadiri kinavyoua ndivyo ladiri kinavyozidi kuharibu na kujichimbia kaburi kubwa..
Baadhi ya 'serial killers' walianza kwa kuua mashahidi ili wapone na kesi za mauaji zinazowakabili.. Lakini kila walivyoteketeza roho moja waliacha nyayo za ushahidi na kujikuta wanazidi kuua ili kupoteza ushahidi mpya!

Chama kimechafuka, kimenajisika na kinanuka damu za watu wasio na hatia. Hakuna dodoki wala kemikali iwayo yote inaweza kukisafisha, kukitakasa na kurudi kwenye asili yake!

Chama Cha Maharamia
 
Nimeandika na kusoma kesi za serial killers na hakuna serial killer aliyekua anaua mashahidi.

Chama cha siasa chochote kinaongozwa na ideology wengi hua mnasema chama fulani kinajichimbia kaburi kwa matendo yake ila mnasahau ideology hazifi. Utakuta chama kina wafuasi 12M nchi nzima, sasa chama kama hichi kujichimbia kaburi unaloliwaza ni ngumu sana.
 
Kinapindua nini sasa! Uhai? Karma is real
kinapindua kila kilicho mbele yake ambacho kinasigana nacho, hakuna ktu inaitwa karma ccm, wao wanaamini karma itamtafuna wanayemtumia, chama kitabaki palepale na kimeshika hatamu, kwan wao wajinga? kwa nn riz au duli asiende front kupindua uhai? wanatumika makada njaa?
 
Huu ndo Umuhimu wa TLS.

Kusimama imara kwa TLS ya Mwabukusi kumefanya Mahakama kujua nafasi yake Kikatiba na Kusimamia kweli Haki.

Kusimama Imara kwa TLS kumesababisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka mafichoni jana na kutoa tamko kuhusu mwendendo wa masuala ya haki nchini.

Kongole nyingi kwake pia Mzee wetu wa maana kabisa Jaji Joseph Sinde Warioba na Mawakili wa Tundu Antipass Lissu wakiongozwa na Senior Counsel Mzee wangu Mwaisa Mpale Mpoki.

Maamuzi haya kwangu mimi ni ushahidi tosha wa uwepo wa TLS imara inayosimama kwa niaba ya Wananchi.
 
Nimeandika na kusoma kesi za serial killers na hakuna serial killer aliyekua anaua mashahidi.

Chama cha siasa chochote kinaongozwa na ideology wengi hua mnasema chama fulani kinajichimbia kaburi kwa matendo yake ila mnasahau ideology hazifi. Utakuta chama kina wafuasi 12M nchi nzima, sasa chama kama hichi kujichimbia kaburi unaloliwaza ni ngumu sana.
Ilikuwepo kesi moja maarufu South.. Jamaa aligombana na mpenzi wake akamsukuma akaanguka akapigiza kichwa akavuja damu nyingi akafa.. Shuhuda alikuwa rafiki wa mpenzi wake.. Jamaa akaona soo naye haikupita wiki akammaliza..lakini marehemu ya pili mauaji yake yalishuhudiwa na mamaake mzazi.. Chain ilifikia watu sita
 
Kuna debate ya nani anafaa kuitwa serial killer na nani hafai.

Muuaji ataitwa serial killer ikiwa ataua watu kwa kutumia modus oparendi ile ile kwa wahanga wake. Debate nyingine ni je idadi gani itafanya muuaji awe serial killer?

2? 8? 10?

Kwa hii stori uliyosema huyo muuaji siyo serial killer kwakua modus oparendi hazifanani
 
Back
Top Bottom