Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

Endelea kusubiri watanzania waingie Barabarani...nakuhakikishia utazeeka na vitukuu vyako vitazeeka hilo halitatokea

Watanzania hatujalelewa kwa utamaduni huo

Ninyi msipokubali kubadilika na kujirekebisha hamtakaa mpate dola.......

Unadhani Tume huru inakuja kama upepo..Tume huru inadaiwa..tena kwa strategy madhubuti,....na kwa kupata support ya mfumo......sasa wewe hcho chama chako CHADEMA kinafanya nini kuhusu tume huru?

Muwe mnasikiliza..wengineo sisi tunawaambia
Mkuu mbona hatuelewani vitu vidogo embu wwe niambie hao wananachi wakiingia barabarani system itazuiaje hilo ndo swali???? Maana nyie mnadai system ndio inaamua rais sio wananchi ndo nakuulixa je wananchi wakiingia barabarani kma kenya system watazuia?????

Nijibu hilo sio kusema ntazeeka sijui tume huru haiji kwa upepo we jibu swali kwamba system wanaweza zuia nguvu ya umma ukiamua mabadiliko??
 
Hili nalo ni kosa lingine mnalofanya

kwamba kwa sababu CCM wanamakosa mengi..kwa hiyo mnajustify makosa yenu....Ninyi kama alternative Party mnapaswa kuwa Perfect.

Mnapaswa kuonesha mko tofauti...Kama hamuoneshi tofauti yoyote...sasa mpewe ili mfanye nini? Si bora tuwaache hawa tunaowajua.

Unajua....Haihitaji akili nyingi sana kuliona hili...Watanzania wanataka Changes...hawataki vurugu...lakini CHADEMA mmeshindwa kuzibeba hizo ndoto za watanzania

Na watanzania sio wajinga..Watawaadhibu Big Time.Subiri 2019 Utaniambia..Hitimisho ni 2020....

Tumewapa mapendekezo mengi sana ili muweze kubadilika..Hamtaki...sasa subirini muadhibiwe
Mkuu embu soma hoja nliomjibu huyo jamaa yeye anasema watanxania hawatuamini kisa RICHMOND ndio namuulixa wasituamini kisa richmond afu waiamini ccm kisa escrow epa kagoda meremeta lugumi n.k !!! Je hao watanzania wana upeo mdogo kiasi gani????

Issue hapa sio kwamba watanzania hawatuamini thats a lie issue inakuja kwenye hali ya kisiasa ya tanzania kutawaliwa na chama kimoja na katiba hii inakifanya chama dola kitawale sekta zote sio jeshi sio mahakama fullstop ila other than that watanzania wameshaichoka ccm toka 2010 hilo halina ubishi kinachobakia ni kuwepo uwanja sawa kwa ajili ya mapambano ya siasa zakiushindani !!

Ndio maana nmemuuliza mtoa mada kma anakiri cuf zanzibar ipo tayari kupewa madaraka na inaaminiwa je iwaje miaka yote seif ananyimwa urais na the so called system???

Ili tutoe benefit of doubt kwanni msikubali iwepo fair ground ya kisiasa hapa tanzania ndio mje mseme kweli watanzania wametuchoka kuliko mnapuuzia hoja za wapinzani afu mnadai watanzania wametuchoka!!!! does it make sense

Ndio nashangaa wwe unajiita mpinzani ssi tulikesha kule kwela uchaguzi wa 2015 kura tunaongoza na fomu tunazo tukaishia kupigwa mabomu na kulazwa selo na mshindi akapewa wa ccm then unakuja hapa unapuuzia hoja za wapinzani kuwa chaguzi sio huru ndio maana tunaangushwa !!!!

Kwa kweli freeland unanishangaza sana, hujui gharama tunayoipitia kusimika mabadiliko hapa nchini then nyie mnakejeli madai yetu
 
wajua upinzania ulikuwa na bado wanayonafasi yakuonyesha mfano katika halimashauri na majiji wanayoongoza.... lakini je wanafanya hivyo kuja kuthibitisha au kulalamika kuhusu sisiemu kuwavuruga....??
Dar wapo kujibizana na Makonda huko Arusha kila siku wapo na gambo yani bado kwa kweli
 
Heshima kwako kaka Mayala Paschal,

Hili bandiko limekuja wakati muafaka katika kutathimini mustakabali wa nchi yetu. Jibu langu kwako ni kwamba CHADEMA hawajawa tayari na sioni kwa kipindi kijacho takribani miaka 20 CHADEMA kuwa tayari kushika dola. Napenda kusapoti majibu yangu kwa ushaidi ufuatao.
1. Demokrasia ndani ya chadema ni kaa la moto- Ni mtu mmoja mwenye madaraka ya kuamua nani awe kiongozi na si vinginevyo. Kwa mfano kitendo cha kumpisha mgombea wao wa uraisi mwaka 2015 kilikuwa ni kosa kubwa kwa watu wanoaofikiria kwa makini. Woote tunajua tuhuma alizokuwa nazo mgombea wao , na wao ndo waliokuwa mstari wa mbele kumkataa ghafla kipindi cha uchaguzi wakamsafisha. Hili ni kosa kubwa na ilinionyesha ni jinsi gani hawaatekelezi kile wanacho kihubiri.
2. Kukosekana kwa mabadiliko kwa muda mrefu: Ukilinganisha na chama tawala (CCM), ingawa harakati za kukabidhiana vijiti ndani ya chama zina figisu figusu lakini angalau wamekuwa wakileta watu wenye mtazamo tofauti pindi wanapotakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa katiba.
3. Ubinafsi ndani ya chama: Kuna makada wamekiteka chama na wao ndo wanaoonekana ndio wanafaa kuongoza chama hivyo kupelekea kuwa nyima watu wenginge wenye damu changa. Ukijitokeza na ukaonekana ni threat basi wanakufukuza. So hii itapelekea wao kuchelewa sana kuyafikia malengo yao.
4. Makundi ndani ya chama: Ni rahisi kuona kwamba kwa sasa kunamgawanyiko mkubwa ndani ya chama, wabunge machachari kama John Myika na wengineo wamejikatia tamaa. Hakuna kelele ni kama wamekufa. Naona wameamua kujilia keki yao kwani 2020 ni ndoto kuingia tena bungeni. Hii ni kweli kabisa.

5. UKAWA: Kusambaratika kwa UKAWA nalo ni pigo kubwa kabisa kwani kwa hali ilivyokuwa ingekuwa raisi kwa muunganiko wa vyama kuikabili CCM lakini mpaka 2020 CUF bara itakuwa imekwisha toweka kwenye ramani ya dunia.

Kwa leo inatosha,

wako mtiifu,

Kajuni wa Kajuni.

Hoja yako ni nzuri ila umeitoa ki hisia zako zaidi
Usifikiri watu wote wana hisia kama zako au mtazamo kama wako cdm iko vizuri zaidi unavyofikiria ww na ime.kamilika kila idara mfano mzuri ni wabunge wake wanavyoibua hoja na kitengeneza hutuba mbadala za wizara hata ha hupaoni? swala la ubinafsi ccm ndio limejaa kila kitu ni mtu mmoja ndio mpangaji
Ili uthibitishe haya waruhusu bunge live ujionee mwenyewe na waruhusu siasa kama viongozi wengi ni bashite unafikiri wanaweza kuongoza nchi? Cdm ina vijana wengi wasomi na wenye taaluma mbalimbali mfano ni srekali ya awamu ya 5 vijana wengi wameingia na wanaweza ila ni waoga wananchi wamekuwa waelewa kwa sasa kasoro tume tu
 
Kwanini mkiambiwa ukweli mnachukia
Mkuu, na hawa nyumbuz ndio wanaowapotosha viongozi wao hivyo daima wanaamini wapo sahihi.
Ikumbukwe hapa jf wapo kibao na viongozi wengi chadema jukwaa hili ni "sebuleni" kwao japo kimyakimya!.
Swali kwako mwenyewe: Are you a serious, able, capable, credible and mature enough ANALYST to provide a sound take on this topic? Mkuu Pascal, hilo unalouliza hapa sio swali wala suala sahihi la mada kuu iliyo mezani leo hii nchini. Swali lenyewe ni: je, Tanzania na Watanzania wanao uelewa, uwezo, uadilifu, utimilifu na ukomavu wa kusimamia na kuchukuana na siasa za vyama vingi? Usipoteze muda na CHADEMA au chama chochote cha upinzani kabla hilo swali halijajibiwa. Na bado sijaona hasa kwa nini umevutiwa kuichagua CHADEMA kama lengo (focus) la bandiko. Hao hawana chao; hata waje kama malaika Gabrieli. Huhitaji kufahamishwa kuwa mazingira yaliyopo nchini hayaruhusu anasa ya mjadala "feki" kama huu unaotaka kuutumia kuchokoza "makada" hapa. Labda kama lengo pekee ni utani na "makamanda".

Bila shaka wewe unao uwezo mzuri sana wa kutambua "genius" aliyotumia Mwalimu JKN kuisuka Tanzania na CCM kiasi cha kuacha "wenye ndoto zao" wakiendelea bila kuchoka kuinyatia CCM kwa nyuma kama mafisi wakijiaminisha kuwa mkono unakaribia kumdondoka binadamu waambulie ulaji! Usifikiri waliopania kumfanya JKN "mtakatifu" wamekurupuka tu. He was a "real genius" kwa namna yake; utake usitake. Atakayekuja na mkakati wa kuufumua huo "msuko" alioudarizi Mwl. JKN ndiye atakayetuwezesha kujadili hicho unachokusudia hapa - that is if you, Sir, yourself are genuine and credible.
 
Mkuu embu soma hoja nliomjibu huyo jamaa yeye anasema watanxania hawatuamini kisa RICHMOND ndio namuulixa wasituamini kisa richmond afu waiamini ccm kisa escrow epa kagoda meremeta lugumi n.k !!! Je hao watanzania wana upeo mdogo kiasi gani????

Issue hapa sio kwamba watanzania hawatuamini thats a lie issue inakuja kwenye hali ya kisiasa ya tanzania kutawaliwa na chama kimoja na katiba hii inakifanya chama dola kitawale sekta zote sio jeshi sio mahakama fullstop ila other than that watanzania wameshaichoka ccm toka 2010 hilo halina ubishi kinachobakia ni kuwepo uwanja sawa kwa ajili ya mapambano ya siasa zakiushindani !!

Ndio maana nmemuuliza mtoa mada kma anakiri cuf zanzibar ipo tayari kupewa madaraka na inaaminiwa je iwaje miaka yote seif ananyimwa urais na the so called system???

Ili tutoe benefit of doubt kwanni msikubali iwepo fair ground ya kisiasa hapa tanzania ndio mje mseme kweli watanzania wametuchoka kuliko mnapuuzia hoja za wapinzani afu mnadai watanzania wametuchoka!!!! does it make sense

Ndio nashangaa wwe unajiita mpinzani ssi tulikesha kule kwela uchaguzi wa 2015 kura tunaongoza na fomu tunazo tukaishia kupigwa mabomu na kulazwa selo na mshindi akapewa wa ccm then unakuja hapa unapuuzia hoja za wapinzani kuwa chaguzi sio huru ndio maana tunaangushwa !!!!

Kwa kweli freeland unanishangaza sana, hujui gharama tunayoipitia kusimika mabadiliko hapa nchini then nyie mnakejeli madai yetu

Mkuu...nadhani wewe hiyo kulala selo na kupigwa mabomu ni dogo kuliko la Mawazo aliyeuawa kinyama...

Hoja hapa ni chama chenu CHADEMA kinafanya nini katika hayo

Kwani nani hajui kuwa hakuna urari katika uwanja wa kisiasa nchini? Ninyi mnafanya nini katika kuupigania huo urari?

Ninyi mmeendelea kushiriki chaguzi zote katika mazingira yaleyale ya kikatiba na tume na mkishindwa mnaanza kulia lia ooh..sijui tume and whatsover.....

Sasa hivi uchaguzi umepita badala ya ku strategize jinsi gani tume huru inapatikana mnahangaika na Makonda....Seriously?

Kabla ya 2015..Wananchi walikuwa wanaielewa CHADEMA kiasi...lakini tangu 2015 hadi sasa hamueleweki..Wananchi hawaoni hata faida ya kuchagua watu wa CHADEMA majimboni kwao...kwa sababu you guys are worse off kuliko hata ma CCM....

Nikupe somo mdogo wangu....System inashawishiwa kwa kuwa na watu imara wenye mipango thabiti na wanaoaminika...Niamini mimi siku ambapo chama cha upinzani kitakuwa na mifumo imara...watu imara...mipango madhubuti...trustworthiness....kitaweza kushawishi system kuwa wapewe dola.
 
Pascal umenena vyema lkn nadhani zaidi ya chadema kuonekana immature as you said tatizo ni kwamba hata uundwaji na namna ya kuratibu vyama vingi vya kisiasa nchini ni system inheritance from existing part.
Chadema or any party can be good enough kama vitaacha ku copy namna ya kuratibu shughuli mbalimbali ndani ya vyama vyao. Labda tuseme kabla ya kuwaamini chadema as a leading opposition regime, tuwapime ni kwa namna gani wanajiongoza kama taasisi pamoja na mtaji wa viongozi walionao je are they credibly existing as a products of chadema and not ex-ccm who tries to bet for position after strong competition from ccm
 
Tatizo la CHADEMA ni Mbowe

Kile chama kimekuwa kikubwa sana kuliko uwezo wake

Yes..Amefanya mengi..lakini uwezo wake umefika mwisho...Hawezi kufanya kingine kipya ambacho hajawahi kufanya...Tatizo kubwa zaidi ni yeye anaamua kila kitu

Huwezi kufanya jambo lile lile kila siku...kwa namna ile ile na kutegemea majibu tofauti...

CHADEMA ikitaka kutokufa ikubali kufanya mabadiliko ya ndani ya msingi kabisa na kukihuisha chama .

Chama kikijenge katika msingi imara na thabiti ya kitaasisi.....waweke mifumo inayowawezesha kuweka sera imara...tested policies...na mwisho watengeneze demokrasia ya kweli ndani ya chama.
Mbowe ndie anayeifanya CHADEMA iendelee kua imara...coz hanunuliki
 
Pascal umenena vyema lkn nadhani zaidi ya chadema kuonekana immature as you said tatizo ni kwamba hata uundwaji na namna ya kuratibu vyama vingi vya kisiasa nchini ni system inheritance from existing part.
Chadema or any party can be good enough kama vitaacha ku copy namna ya kuratibu shughuli mbalimbali ndani ya vyama vyao. Labda tuseme kabla ya kuwaamini chadema as a leading opposition regime, tuwapime ni kwa namna gani wanajiongoza kama taasisi pamoja na mtaji wa viongozi walionao je are they credibly existing as a products of chadema and not ex-ccm who tries to bet for position after strong competition from ccm
Ex CCM kwenda chama kingine isiwe tatizo
hata chadema kwenda ccm sio tatizo
Ukweli ni simple tu
CHADEMA hadi kufikia hapa wamejitahidi...cha msingi waendelee kupambana
Mfumo wa nchi hii unakibeba Chama tawala na sio kweli kwamba Chama kingine hakiwezi kutawala
sio karne hii ambayo wasomi wamejaa na watu wana exposure.
 
Kama Chadema ilimuita yule jamaa yako fisadi lakini alipohamia kwao akageuzwa kuwa jembe tena bila ridhaa ya wanachama sitegemei chama hiki kiwe serious kupewa nchi.

Kama kiongozi wake mkuu anatuhumiwa katika ngada ,ukwepaji kodi na uhujumu wa NHC na anakaa kimya sitegemei kama wanaweza kuaminiwa.

Kama chadema inadiriki kuilaumu serikali eti itakosa misaada kwa kuwa inaminya demokrasia ...bado chadema inaamini nchi itakombolewa na wahisani hivyo sio chama chenye fikra mbadala.

Kama chadema kinajiita chama cha demokrasia ilihali mwenyekiti wao ni wa kudumu na upatikanaji wa wabunge wa kuteuliwa au viongozi mbalimbali wa kanda unategemea majina ya mfukoni sioni kama chama hiki kinafaa kuwa mbadala wa CCM.

Kama chadema kina viongozi wanaotegemea ufuasi wa wahalifu ili kuingia madarakani ...hili ni jambo hatari kwa usalama wa nchi.nilimsikia lema kama waziri kivuli wa mambo ya ndani akiwakumbuka marafiki zake wafungwa na mahabusu tena kwenye hotuba yake rasmi.nini kitazuia chama hiki kuendeshwa kwa fedha na matakwa ya wahalifu?Tulishuhudia chadema ikiwatetea wafanyabiashara wanaokwepa kodi,wafanyakazi wazembe na wabadhirifu na watu wa aina hiyo.yaani chadema na wahalifu ni washikaji.

Kama chadema hii inategemea kupata kiki za msibani badala ya kujitoa na kushiriki na wafiwa sitarajii watanzania wenye akili zao timamu waipe kura kuongoza taifa hili takatifu.

Ni chadema hiihii kila kukicha inatukana vyombo vya ulinzi na usalama yaani kuanzia polisi,jwtz na Tiss...sitegemei hawa kupewa nchi hii ya wazalendo.

Kwa ufupi CCM ni Alpha na Omega upinzani uliopo ni chachu tu ya kuisaidia /kui-Check CCM ilete maendeleo kwa nchi.

Umepiga penyewe mkuu....inahtaji uwe empty headed (unintelligent and foolish) kuwachagua hao wahuni from North
 
Tatizo la watu kama Paschal wanafikiri chama hutawala nchi. Hii siyo kweli hata kidogo. Chama hujibanza tu serikalini. Naomba Paschal na wengine wenye mawazo kama yake waniambie, je, CCM ikiondoka madarakani nini kitakosekana kuendesha nchi? Chukulia mfano Majiji na miji inayoongozwa na upinzani, ni nini kinakosekana kuendesha miji na majiji hayo? Mbona mambo ya serikali yanaenda vizuri tu? Hivyo ndivyo itakavyokuwa hata kwa nchi nzima. Maana nchi ni mkusanyiko wa hii mikoa. Chukulia kwa mfano mkoa wa Arusha na Kilimanjaro ambako CCM haina chake. Mbona kuna maendeleo kuliko Dodoma na Singida ambako CCM imetamalaki? Nijuavyo mimi CCM ikiondoka kikaja chama kingine shughuli zote za serikali zitaendelea kama kawaida. Waajiriwa wa serikali ndio huendesha nchi na siyo waajiriwa wa chama. Hospitalini, majeshini, shuleni, vyuoni, mahakamani, mikoani, wilayani, kwenye halmashauri, bandarini, n.k shughuli zitaendellea kama kawaida.

Nyie akina paschal mliobahatika kwenda shule msipotoshe umma kwamba CCM ikitoka nchi itashindwa kujiendesha. Ni uongo kabisa. Sasa naomba Paschal useme ni kitu gani nchi itakosa CCM ikitoka madarakani? Muulize hata Wakili msomi Petro Mselewa atakuelewesha na najua hatakutoza "consultation fee".

Adama Barro kamtoa yahya Jammeh,
Buhari kamtoa jonathan G na walishinda kwa kuviondoa vyama dola.

Pia , Zambia aliingia satta, banda Lupia na E. Lungu wakitoka vyama tofauti. malawi walimtoa banda Joyce akaiing prof P muthalika ,senegal walimtoa Wade abdulaye,kenya wamefanya mabadiliko
Je, huyu mayala mpotoshaji anaweza kutuambia tz inatofauti au ni kubwa/bora kuliko nchi nyingine za africa.

?
CCM inatumia siasa chafu kuvihujumu vyama vya upinzani lakini ina mwisho wake mzuri/mbaya, Yahya jammeh aliondoka kama ajali na ccm inaweza kuondoka kwa demokrasia au ajali.
Mwisho vyombo vya dola.viache kuhujumu watu wenye mawazo tofauti na ccm kwani sote ni watz
 
Topic moja very important kwa mustakabar wa taifa letu. But mimi bado nina maswal kwa mleta mada.
1.creteria zip zinazotumika kuonesha maturity level ya chama cha siasa.
2.kazi ya wanasiasa ni ipikatika muundo wa serikari.
Naomba kwanza mi niishie hapa ntaludi baadae.
 
Mr Mayala kajitahidi kuweka Hoja zake mezani kama Mwanajukwaa Huru Katika Jukwaa Letu Pendwa la Siasa, Were We Dare To talk Openly.
Kwa mantiki ya Andiko lake anapaswa kujibiwa kwa Hoja na si kumwambia ake Kimya kama ndivyo hakuna Sababu ya Kuwa na Jukwaa hili kila mtu angekaa na hoja yake moyoni mwake, na kumwambia akae kimya au hana sababu ya kutueleza anachofikiri ni Dalili za Udiktekta.
Nimesoma na kukuelewa kwa Upana Mayala,
Nishauri yafuatayo Kwa CHADEMA
1.waboreshe mfumo wa mawasiliano ndani ya chama.
2.wawe na semina elekezi kwa Viongozi na wawakilishi wa wananchi (w/viti Mitaa,Madiwani na Wabunge)
3.Migogoro ya Ndani itatuliwe.
4.Ruzuku ipelekwe majimboni ili shughuli za Chama zitekelezeke.
5.Ilani ya Chama itekelezwe kwa Vitendo kwenye Majimbo na Halmashauri wanazoziongoza.
6.Wawaandae Vijana watakaokipokea Chama (Leader Materials) wakuzwe na ikiwezekana waanzishe chuo Cha uongozi ili kuwafua.
7.Waboreshe mifumo ya ulinzi.
8.Wapeleke Vifaa vya uenezi kwenye Maeneo Husika Kadi, Bendera N.k
9.Kuwe na uwazi katika Rasilimali za Chama na ziwanufaishe wote kwa Usawa.
Naamini Wananchi wanahitaji mabadiliko ya Kiuchumi,Kisiasa na Kijamii.
Nafikiri Waanze Majimboni kuwa na Wabunge Wengi kwanza walishike Bunge
 
Chadema bado hawajajiandaa kupewa Nchi........... Kama swala dogo tu Ubunge wa EALA limewashinda wataweza kuongoza nchi??

Asilimia kubwa ya viongozi wa Chadema si wanasiasa ni Wanaharakati...... Toka lini Wanaharakati waliweza kuongoza nchi????
 
Topic moja very important kwa mustakabar wa taifa letu. But mimi bado nina maswal kwa mleta mada.
1.creteria zip zinazotumika kuonesha maturity level ya chama cha siasa.
2.kazi ya wanasiasa ni ipikatika muundo wa serikari.
Naomba kwanza mi niishie hapa ntaludi baadae. QUOTE]
Mayala tuletee scale za maturity kwa vyama vinavyoweza ongoza dola kama maday alivyitaka
 
Mkuu...nadhani wewe hiyo kulala selo na kupigwa mabomu ni dogo kuliko la Mawazo aliyeuawa kinyama...

Hoja hapa ni chama chenu CHADEMA kinafanya nini katika hayo

Kwani nani hajui kuwa hakuna urari katika uwanja wa kisiasa nchini? Ninyi mnafanya nini katika kuupigania huo urari?

Ninyi mmeendelea kushiriki chaguzi zote katika mazingira yaleyale ya kikatiba na tume na mkishindwa mnaanza kulia lia ooh..sijui tume and whatsover.....

Sasa hivi uchaguzi umepita badala ya ku strategize jinsi gani tume huru inapatikana mnahangaika na Makonda....Seriously?

Kabla ya 2015..Wananchi walikuwa wanaielewa CHADEMA kiasi...lakini tangu 2015 hadi sasa hamueleweki..Wananchi hawaoni hata faida ya kuchagua watu wa CHADEMA majimboni kwao...kwa sababu you guys are worse off kuliko hata ma CCM....

Nikupe somo mdogo wangu....System inashawishiwa kwa kuwa na watu imara wenye mipango thabiti na wanaoaminika...Niamini mimi siku ambapo chama cha upinzani kitakuwa na mifumo imara...watu imara...mipango madhubuti...trustworthiness....kitaweza kushawishi system kuwa wapewe dola.
Mkuu kabla ya kujibu hoja zako naomba ujibu zangu nilizouliza........ je wananchi wakiamua kuipa kura upinzani afu wakaingia barabarani kudai ushindi wao je system watazuia???

Nachoataka hapa nipate jibu moja je nani mwenye nguvu kumuweka mtu ikulu system au wannachi nijibu hilo tu

Kwanni nauliza?? Wwe na mtoa mada mnadai system haituamini ndio maana hatupewi ikulu labda nikuulize system inaiaminije ccm wakati miaka 50 imefeli kila kitu...... Y????

Haya pasco anasema chadema bado ila cuf tayari kimekomaa ndio nauliza kma cuf wamekomaa iweje hawapewi dola zaidi kila mwaka wanadhibitiwa???

Anyway conclusion yangu ni whether upinzani utakomaa or not ccm haitowahi kutoka as long as dola haitofautishwi na chama kwa mfumo wa katiba hii ya sasa......... trust me huko TISS au jeshini kuna watu wamekunywa maji ya bendera kuilinda ccm kwa gharama yoyote je hao unafkiri hata chadema ikisimamisha malaika watamuachia eti kwa kuwa wamekomaaa?????

Anyway embu nisaidie hapo mkuu tuwekane sawa
 
Back
Top Bottom