Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
Mkandara:
Watu hatusomi katiba na kuzielewa. Mkutano wa NEC hauna makosa yoyote kikatiba kwa sababu moja kubwa.
Mbunge anachaguliwa akiwa ni mwanachama wa chama cha kisiasa. Hivyo akifukuzwa au akiacha uanachama wa chama chake basi anakuwa amepoteza ubunge wake.
Na katiba ya CCM inasema kuwa kazi moja ya NEC ni kungalia kuwa viongozi wa CCM wanafuata na kutimiza agenda za chama. Hivyo kama watu walikuwa wana malalamiko kuhusu Sitta, NEC ni sehemu mwafaka kusikilizwa malalamiko hayo. Na baada ya kusikiliza NEC inaweza kutoa hatua za kichama.
Na kama hatua ya NEC itakuwa ni kumfuta mbunge au kiongozi uanachama, basi automatically sheria nyingine za katiba ya nchi zitafuatia. Kama vile kupoteza madaraka.
Kwa mfano Mrema aliporudisha kadi yake ya CCM, alipoteza ubunge.
Hivyo msikae hapa mnapiga kelele wakati hizo ni taratibu za CCM. Kolimba, Kitine waliitwa kwenye vikao vya NEC. Hivyo hii sio mara ya kwanza.
Mzee kujadili mwenendo wa Bunge na kutaka kuzima hoja zinazo itafuna Nchi ndiyo issue hapa mengine haya ni yao wenyewe CCM.Ila kulikemea Bunge na hata kumkata speaker kuwaumiza wapinzani na hoja zao ni kazi ya NEC ya CCM ?