Je, CCM kuingilia uhuru wa Bunge, imevunja katiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, CCM kuingilia uhuru wa Bunge, imevunja katiba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Aug 20, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  NEC imeingilia uhuru wa Bunge-Slaa

  Wednesday, 19 August 2009
  Na Waandishi wetu - Majira.


  UAMUZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuwakata makali wabunge wake kwa lengo la kupunguza mashambulizi dhidi ya Serikali, umetafsiriwa kuwa ni uvunjaji sheria za nchi na ni kosa la jinai kwani ni kuingilia wajibu wa Bunge.

  Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbrod Slaa, alipozungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Dar es Salaam jana.

  Alisema; "Ibara ya 100 ya Katiba inaeleza kuwa uhuru wa Bunge hauwezi kuingiliwa na chombo chochote, wanapowazuia wabunge asiongelee suala fulani wanaingilia uhuru wa Bunge."

  Kauli hiyo ya Dkt. Slaa imekuja siku moja tangu Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ikiwa imeunda kamati ndogo ya watu watatu kuchunguza kiini cha mashambulizi ya wabunge dhidi ya Serikali, itakayoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ikiwajumusiha Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, Bw. Pius Msekwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Bw. Abdulrahman Kinana.

  Akizungumzia tishio lililokuwa likimkabili Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta, kiasi cha kufikia hatua wajumbe NEC kutaka anyang'anywe kadi ya CCM kwa madai ya kushindwa kusaidia chama chake bungeni, Dkt. Slaa alijibu;

  "Acha Sitta ashughulikiwe mimi sina huruma na hilo, akitaka kuwa huru asijadiliwe kwenye vikao vya chama basi ajiengue kwenye ujumbe wa NEC...Katiba ya nchi haimtaki awe mjumbe wa NEC na CC (Kamati Kuu) ya CCM."

  Alisema walishamtaka aache kuhudhuria vikao vya Kamati ya Uongozi ya CCM inayotokana na wabunge, lakini alishindwa kufanya hivyo.
  Alidai wabunge wamekuwa wakimpelekea hoja zao ili zijadiliwe na Bunge, lakini anazipeleka kwenye Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM na kujadiliwa kwanza.

  Alitolea mfano hoja aliyotaka kuwasilisha bungeni ya watuhumuwa wa ufisadi aliowataja katika mkutano wa Mwembe Yanga kuwa ilikwamishwa na Kamati ya Wabunge wa CCM baada ya kupelekwa huko na Spika pamoja na watu wa Usalama.

  "Kama anataka kushughulikia ufisadi basi ajitose, aache kushughulikia vita hiyo nusu nusu," alisema na kuongeza kuwa kama asingekuwa ndani ya CCM Bunge lingemlinda.

  Alisema kwa sasa CCM inajivunia kipengele kimoja kilichopo kwenye kanuni za Bunge kinachoeleza kuwa kamati za vyama zinatambuliwa ndani ya bunge.

  Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria wa CHADEMA na wakili wa kujitegemea, Bw. Tindu Lissu, alisema ofisi ya Spika inatakiwa kulindwa vinginevyo chombo hicho muhimu kitakuwa kinatelekezwa.

  Kuhusu uamuzi wa NEC kuwakata makali wabunge wa CCM, Bw. Lissu alisema; "Kilichofanyika ni uvunjaji wa sheria."

  Aliongeza kuwa uhuru wa mawazo na majadiliano ndani ya Bunge hautakiwi kuhojiwa na chombo chochote kile hata kama ni mahakama.

  Bw. Lissu alisema wajibu wa Bunge ni kutunga sheria na kuidhibiti Serikali, ndiyo maana lina mamlaka ya kumuondoa Rais, Waziri Mkuu au Waziri yeyote kwenye wadhifa wake, endapo halitaridhika na utendaji kazi wake.

  Alisema ili Bunge liweze kutekeleza wajibu huo, linahitaji uhuru na kama utaondolewa basi Tanzania itakuwa imerudi kwenye mfumo ule unaofanana na wa chama kimoja.

  "Tuna wajibu kama wananchi kutetea hadhi ya Bunge, tukiruhusu wabunge watishwe basi hatutakuwa na Bunge lenye uwezo wa kudhibiti Serikali,"alisema Bw. Lissu. Alisema sheria ya Bunge ya mwaka 1998 imeweka kinga na madaraka ya Bunge.

  Akinukuu sheria hiyo, Bw. Lissu alisema; "Sheria inasema mtu atakayefanya vitendo ambavyo vinapunguza madaraka ya bunge atakuwa ametenda kosa la jinai."

  "NEC ya CCM imetenda kosa la jinai kama kuna mtu wa kwenda kuwafungulia RB kwa Manumba (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jina DCI Robert Manumba) afanye hivyo lakini na yeye hawezi kutusaidia kwa kuwa na yeye ni CCM.

  Alisema kwa mwelekeo wa sasa Bunge litaanza kufanyakazi kwa namna ambayo CCM inataka. Aliongeza kuwa kwa mwenendo wa aina hiyo mijadala kama ya Richmond, Buzwagi na EPA isingeweza kuibuliwa ndani ya Bunge.

  Akizungumzia sakata la mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Bw. Lissu alisema Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, hawezi kusafishwa tuhuma hizo na vikao vya NEC na CC kwa kuwa alijimilikisha mgodi huo mali ya umma akiwa rais, hivyo alikiuka sheria ya maadili ya viongozi.

  "Hilo ni kosa la jinai na mahala pake ni mahakamani na siyo kujadiliwa na NEC au CCM," alisema na kuongeza;
  . "Kutwaa mali ya umma siyo sehemu ya mamlaka ya rais...ni kwa nini alichukua mali ya umma na kuifanya ya kwake?"Alihoji Bw. Lissu.

  Alisema Bw. Mkapa ameshindwa kufikishwa mahakamani kwa kuwa wale wanaosimamia sheria nao wanatakiwa kufikishwa mahakamani.

  Akieleza kuhusu hilo, Dkt. Slaa hawataacha kupiga kelele kulalamikia kitendo cha Bw. Mkapa kujimilikisha mgodi wa Kiwira. "Hatutakaa kimya, tutazuiwa kumuongelea ndani ya Bunge ,lakini mahakama ya mwanasiasa siyo bungeni ni kwa wananchi," alisema.

  Aliongeza kuwa; "Ukiona chama kinawazuia wabunge wasizungumzia kitu chochote basi hicho kinakaribia kufa," alisema.

  Alielezea mshangao wake kuhusiana na Serikali kutaka kuchukua mgodi wa Kiwira na kuwarejea wamiliki wake akiwemo Bw. Mkapa fedha zao.

  Alisema Serikali inaendelea na mchakati huo wakati haijulikani waliokuwa wafanyakazi wa mgodi huo fedha zao kiasi cha dola milioni saba wanazodai kama malimbikizo ya NSSF watazipataje.

  Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alidai kuwa NEC imedhihirisha kuwa CCM ni chama cha mafisadi na wale wote wanaopambana na vita hiyo ni bora wakang'atuka ili kuwamaliza mafisadi hao.

  Akizungumza na gazeti hili, Prof. Lipumba alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete hawezi kupambana na mafisadi waliomo ndani ya chama hicho kwani ndio waliounda kundi la wanamtandao lililomweka madarakani na kuwa lina nguvu ndani ya chama hicho.

  Profesa Lipumba alisema kuwa kama kweli Spika Sitta na wabunge wengine wanataka kupambana kidete na ufisadi lazima watoke CCM kwani inaonekana kete za mafisadi wa CCM ni kali.

   
 2. Sungi

  Sungi Senior Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi sidhani hili la CCM kuzungumza na wabunge wake lina uhusiano wowote na katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. CCM inayotaratibu zake za ndani ya chama ambazo wanachama wa chama hiki wanaongozwa wakati wote.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani jamani mweee!
  Hivi kweli mnaamini kuwa Spika hawezi kuingiliwa utendaji kazi wake na chama tawala?...
  Ebu kwa wale wanaoishi UK nambieni nini hasa source ya Speaker wenu mr. Martin kujiuzuru maanake nilisikia kwamba PM ndiye aliyelianzisha vagi zima na kama sikosei Labour party wali sign a motion of no confidence, matokeo yake mzee akakubali kujiuzuru..
  Sasa picha kama hiyo mnaielewa vipi?
   
 4. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mkandara, Speaker Martin hakuwahi kupigiwa no confidence vote...
  Kilichofanyika hapa ni kwamba baada ya gazeti la daily telegraphy kuja na list ya wabunge na vitu walivyo-claim kama gardening, furniture etc... wabunge walimjia juu kwa sababu akiwa kama mbuge hakuhakisha maadaili ya bunge ya ubunge yanafuatwa... maadali haya ni kama uhuru wa kutoa mawazo... martini alikuwa anazuia kinachoombwa na wabunge kisijulikane hivy wengi hasa wananchi kupitia magazetini na kura za maoni hawakulipenda hilo...
  Hivyo alikugundua kwamba hawamtaki... na akafanya yaliyomema... akajiuzulu...

  Kinachofanyika kwetu ni kwamba speaker anaitwa mhaini na yeye kukaa kimya bila hata kuomba ufafanuzi, na speaker huyohuyo anataka kuwa champion wa uhuru wa mawazo ingawaje uhuru wake huo pia unaingiliwa hivyo sijui atafanyaje kazi ili hali akijua kwamba kuna jopo la watu linakudolea macho kwa utendaji kazi wake...
  Ina maana hafai!!! ni vema aachie ngazi na waje wengine...

  pia ccm kujadili mambo yanayotokea bungeni ni kupungukiwa uwezo wa kufikiri... tangu lini mambo ya barazani/bungeni yakafanywa kuwa ndio agenda za mikutano ya vyama vya siasa... ina maana kwamba kama vyama vya siasa havina agenda, hakuna haja ya kuitisha mikutano...
  Bungeni ni mahala pa kufanya kazi mbili tu.
  1. matatizo yanatajwa... ufumbuzi unatolewa/unapatikana
  2. kutungwa sheria

  full stop na sio kujadili eti speaker anaibana serikali... nafikiri umefika wakati muafaka wa kumfanya speaker asiwe anatokea au kufungamana na chama chochote cha siasa..
  ni haya mkandara!!
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mkandara, mfano unaoutoa wa UK ni potofu na hauna uhusiano wowote na linalotokea Tz - hapa CCM inahoji utendaji na maamuzi ya Bunge kama mhimili mojawapo wa dola. Spika Sitta analaumiwa kwa kuruhusu mijadala Bungeni ya mambo yasiyoipendeza Serikali - kwa maana nyingine NEC ya CCM inataka Bunge lifumbie macho mapungufu katika utendaji kazi wa serikali. Hili haliwezi kutokea popote pale duniani penye utawala wa kistaarabu wa kidemokrasia na unaosheshimu misingi ya sheria na taratibu. Spika wa UK aliandamwa na tuhuma binafsi zilizohusu makosa ya jinai na si kwa sababu ya Bunge la UK kuzikosoa serikali au chama cha Labour Party. Hata hapa hoja ya kutokuwa na imani inaweza kutolewa lakini ndani ya Bunge na si kwenye vikao vya siri vya CCM.

  Je Mkandara, itakuwa haki NEC ya CCM kumwita Jaji Mkuu na kuanza kumkaanga kuhusiana na hukumu zilizotolewa na mahakama zinazowahusu watendaji wa CCM au serikali ?

  Wenzetu wanao hata huo ustaarabu wa kujiuzulu wanapotuhumiwa !
   
 6. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mabishano ya nini?

  Kilichofanyika UK kwenye Bunge la House of Commons ni hiki hapa chini.
  Ukipenda kisome ukichukie kifunike!

  Nimeshasema na ninasema tena CCM acheni propaganda na porojo za kitoto. Mkandara anataka kutushawishi kuwa kilichofanyika UK ni sawa na upuuzi wa CCM waliofanya juzi.
  Waingereza wana akili bwana hawawezi kufanya ujinga kama wa CCM. Wao ndiyo waliotufundisha ustaarabu na utawala wa sheria ingawa sisiem hamtaki kuutumia.

  Baada ya kusoma tafakari kama ni CC au NEC ya Labour Party au Liberal Democratic Party iliyokaa na kumwambia Spika Martin ajiuzulu. Hapa tunaona ni Wabunge wa vyama vyote wakiwa ndani ya Bunge wakimtaka spika aondoke kwa kushindwa kuwajibika kutokana na matumizi mabaya ya pesa za umma na si vinginevyo!!!  Furious MPs tell Speaker Martin: go now or suffer 'death by thousand cuts'


  Unprecedented scenes in Commons after Martin's apology over expenses row fails to quell calls for resignation
  MPs from across the House of Commons rounded on the Speaker, Michael Martin, yesterday over his handling of the row over parliamentary expenses and allowances.
  In unprecedented scenes in the modern era, the Speaker was told to resign and one Conservative MP shouted at him from the bar of the Commons as Martin failed to address cross-party calls to retire.

  Will Woodward on whether Commons Speaker Martin will quit Link to this audio Nick Clegg, leader of the Liberal Democrats, who on Sunday became the first party leader to call for him to resign, tonight warned Martin he faced a humiliating end to his career: "My fear is that if the Speaker digs in, he will suffer death by a thousand cuts." Clegg spoke out after Martin had responded to mounting public anger by apologising directly to the British ­people for parliament's, and his, conduct over MPs' expenses.

  "Please allow me to say to the men and women of the United Kingdom that we have let you down very badly indeed," Martin said in a statement to MPs. "We must all accept the blame and, to the extent that I have contributed to the situation, I am profoundly sorry."
  The Speaker, who tried to take control of the expenses row by calling the party leaders to a meeting within 48 hours, made no mention of his own position. His failure to address his future, as members across the chamber signed a motion calling on him to resign, prompted a wave of MPs to call on him to consider his position.
  Sir Patrick Cormack, one of the longest serving Tory MPs, highlighted Martin's precarious position by likening the atmosphere in the Commons to the Norway debate in 1940. The debate, called after the failure of the British military expedition in Norway at the start of the second world war, prompted the resignation of Neville Chamberlain as prime minister after Leo Amery quoted Oliver Cromwell to say: "In the name of God, go."
  Cormack said: "Could I ask you, sir, to bear in mind that the condition of the house now is rather like the condition of the country at the time of the Norway debate, and could you reflect on that?"
  Labour, Tory and Lib Dem MPs expressed astonishment when the Speaker said MPs would not be able to debate a motion calling on him to resign after Douglas Carswell, the Tory MP for Harwich and Clacton, tabled the no-confidence motion.
   
  Last edited: Aug 20, 2009
 7. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mkandara, lolote linalotokea ulaya, marekani na hata Asia haliwezi kuhalalisha yanayotokea TZ hasa kama yako bayana katika Katiba na sheria zetu.

  Mkuu, iko wazi kabisa katika ibara ya 100 kuhisiana na uhuru wa Bunge.


   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa ni MCHAKATO mzima wa kumpata SPIKA wa BUNGE letu. Katika hili KATIBA ya CCM inaonekana dhahiri iko juu ya KATIBA ya JMT. Kitu ambacho sio sahihi. Wenzetu Kenya wameliona hili na wamelirekebisha kirahisi tu kwa kuwa vyama vya siasa kwao ni mkusanyiko wa kawaida tu ambao hata usajili wake sio mgumu kama huu wetu.
  Tungoje Spika arudi kwenye JUKWAA lake la kujidai tuone atalifanyiaje kazi hili. Vinginevyo mabingwa wa kununua kesi akina Mtikila walisogeze MAHAKAMANI ili tupate ufafanuzi wa kisheria.
   
 9. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakati huo huo Rais pia anaweza kulivunja bunge.
   
 10. l

  libidozy Member

  #10
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli nimeamini elimu si lazima uvunje madarasa!Wewe unawafagilia waingereza eti wana akili yaani yako imedumaa au?!
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu, Mbona mmekuja mbogo wakati mimi nachozungumza sio hoja inayoshinikiza kuhojiwa kwa Speaker Sitta ila uwezekano wa chama tawala kumwezeka kitimoto Speaker kutokana na utendaji kazi wake bungeni akiwa kama Speaker. Hata mimi sikubaliani na kilichotokea Tanzania ila nimejiuliza kama kikao cha CC kina haki ya kufanya hivyo..Ndipo niliposema Kikao cha chama kina haki kikatiba (katiba yao) kumuuliza mtu yeyote na hata ku vote motion of no Confidence.
  Kisha ningeomba mtofautishe katiba mbili hapa kuwa CCM wana katiba yao na kuna katiba ya Kitaifa.
  Kama sikosei pengine itabidi nipitie upya jarida la kesi ya Speaker wa Uingereza. Sikusema Bunge lilipitisha motion of no confidence isipokuwa chama chake na nadhani kuna mtu anaitwa Government Business Manager ndiye aliyeshinikiza motion hiyo. Kuna sehemu niilisoma majina ya wajumbe (Labour party) wali vote na motion ikapita..
  Hivyo sina maana kabisa kwamba kinachofanyika Ulaya ni lazima kifanyike Tanzania kwani inategemea na kesi yenyewe lakini maadam utaratibu wa Utawala ni sawa na nchi hizo ama niseme tumeiga toka kwao sioni tofauti inakuja sehemu zipi.
  Recta, Mkuu unachozungmza wewe ni katiba ya nchi na jinsi inavyoweza kufanya kazi lakini sii within a party. kama nakumbuka vizuri Chadema walimsimaisha mwenyekiti msaidizi wao marehemu Wangwe Uenyekiti na wangeweza kwenda zaidi kumpokonya kadi ya chama kulinagana na katiba yao hata kama inapingana na katiba ya nchi.
  Ni ktk kuchanganya mabo haya ndio maana tunashindwa kuwahukumu kina Lowassa, tunadhani kwamba maadam wao wamechaguliwa na wananchi wa majimbo yao basi chama au serikali haina ruhusa ya kuwanyang'anya Ubunge.

  Kwa hiyo mkuu wangu sizungumzii kosa la Speaker wetu, ambalo halipo isipokuwa ni Ushujaa mtupu kwa mtazamo wangu...kama yule marehemu Wangwe lakini kikatiba vyama vina uwezo mkubwa juu ya wawakilishi wake.. Na nadhani South Afrika pia walimwondoa mzee wao Mbeki ktk mkutano kama huu na Zuma akachukua nafasi wakati vyama vingi ikiwa ni pamoja na bunge la nchi hiyo lilikuwa against mbinu na matokeo ya kumwondoa Mbeki madarakani.
   
  Last edited: Aug 20, 2009
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hebu tujiulize watanzania je ni kweli spika anatekeleza wajibu wake kama inavyostahili bungeni,je ni kweli sio kweli kwamba anapindisha baadhi ya kanuni za bunge ili kulinda maslahi ya chama chake,kwangu mimi ikithibitishwa kwamba ana tekeleza kazi wake kwa mujibu wa kanuni za bunge na mujibu wa sheria kama spika ndipo nitakamoamini kwamba yaliyotekea kwenye kikao cha ccm cha cc sio propaganda za kupindisha vuguvugu la kimapinduzi linaloendelea zidi ya mafisadi
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,541
  Likes Received: 81,975
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Recta, kwa mantiki hayo basi CCM kwa kutaka kuingilia na kuhoji utendaji wa Spika wanavunja katiba ya nchi.
   
 14. Sungi

  Sungi Senior Member

  #14
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sio kwa sababu tulitawaliwa na Waingereza basi kila wanachofanya wao basi nasi tunakifanya ... soma Kanuni za Bunge hapa. Hebu tuchambue mambo kisomi sasa sio kwa "personal emotions".
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu tuwe makini ktk hili hapa kwani tusije kumjengea ngao kubwa speaker Sitta..
  Ebu nikupe mfano nje ya mada hii kidogo.. tuseme Chadema ndio wameshinda na kumchagua Spika wa bunge ambaye
  Hivi kweli mnataka kusema Sitta angekuwa mbunge na spika wa Chadema na akafanya kinyume cha chama kwa kukataa kabisa mada zinazohusiana na Mafisadi kusimamishwa kinyume cha wabunge wa Chadema....basi Uongozi wa Chadema ungekuwa hauna haki kumsimamisha Uongozi Spika huyo kwa sababu analindwa na katiba ya nchi?..Meaning hivi leo Spika Sitta angekuwa anafanya kama Mafisadi wanavyotaka tungekuwa hatuna sheria ya kumwajibisha!..
  Mkuu soma kipengele cha pili kinatanguliwa na maneno haya:- Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika..
   
 16. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Bado tuna watumwa ndugu yangu. Wakiona mzungu wao wanafikiri ni akili, kaazi kweli kweli
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu shukran sana lakini kikao cha CCM sio kikao cha Bunge..
  Hakuna mahala popote ktk katiba kunapoweka sheria kuzuia chama kimoja kumnyang'anya kadi mwanachama wake kwa makosa ndani ya katiba ya chama. Kila chama kina katiba yake na ukivunja katiba hiyo chama kinaweza kabisa kukunyang'anya kadi hata kama ukiwa rais wa nchi acha mbali Spika..Hivyo JK anaweza kuvuliwa kadi kwa makosa ndani ya chama with motion of no confidance..Na ndivyo inavyo apply kwa Spika.

  Sasa ukitokea upande huu wa mtazamo utaona mantiki ya hoja yangu kwamba kuwepo kwa Spika kunatokana na uwalikishi wa chama..
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu ebu nambieni hapa ingekuwa vipi.. Spika sitta amejiunga na Mafisadi na amekataa hoja zozote zinahusiana na Mafisadi kuzungumzwa Bungeni.. Kisha ktk mkutano mkuu wa chama chama wapambe wa JK wakasimama na kusema Spika anakiuka kanuni za chama kuwalinda Mafisadi.. Je, bado ingekuwa ni kosa la mkutano huo kumweka kitimoto Sitta maanake navyofahamu mimi uamuzi wowote wa Sitta iwe for or agaist Mafisadi bado kungeigawa CCM vile vile..Bado tungekuwa upande wa Spika?.
   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mkandara ndiyo maana Chadema wakasema na wamesema na wana nia ya muswada Bungeni kwamba Speaker awe mwenyewe asiwe wa Chama . Hapa CCM sijui kama watakubali maana wana amini kwamba wao ni wengi so kila siku watatoa speaker wao.
   
 20. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180

  Mkandara:

  Watu hatusomi katiba na kuzielewa. Mkutano wa NEC hauna makosa yoyote kikatiba kwa sababu moja kubwa.

  Mbunge anachaguliwa akiwa ni mwanachama wa chama cha kisiasa. Hivyo akifukuzwa au akiacha uanachama wa chama chake basi anakuwa amepoteza ubunge wake.

  Na katiba ya CCM inasema kuwa kazi moja ya NEC ni kungalia kuwa viongozi wa CCM wanafuata na kutimiza agenda za chama. Hivyo kama watu walikuwa wana malalamiko kuhusu Sitta, NEC ni sehemu mwafaka kusikilizwa malalamiko hayo. Na baada ya kusikiliza NEC inaweza kutoa hatua za kichama.

  Na kama hatua ya NEC itakuwa ni kumfuta mbunge au kiongozi uanachama, basi automatically sheria nyingine za katiba ya nchi zitafuatia. Kama vile kupoteza madaraka.

  Kwa mfano Mrema aliporudisha kadi yake ya CCM, alipoteza ubunge.

  Hivyo msikae hapa mnapiga kelele wakati hizo ni taratibu za CCM. Kolimba, Kitine waliitwa kwenye vikao vya NEC. Hivyo hii sio mara ya kwanza.
   
Loading...