Je, CCM Itatawala Milele Au?

Je, CCM Itatawala Milele Au?

Status
Not open for further replies.
Safi FMES; naona maoni yako yanaweza kupigiliwa msumari kama huu

Kama tunataka kuikoa nchi yetu haraka iwezekanavyo, tusimuonee aibu yeyote yule ambaye anakuwa kikwazo. Awe CHADEMA, CUF, CCM etc., ni nchi yetu iliyowekwa mhanga hivi sasa.

Tunavyoendelea kuiachia nchi kwenye mikono ya manyang'au ndio itakavyokuwa vigumu zaidi kuikomboa. Lakini kama tukiendelea tu kuwapigia makofi watu wabovu kwa vile tu ni wa chama unachokishabikia, tusije tukajilaumu nchi ikibaki mikononi mwa JK na timu yake milele.
 
Hawawezi tawala milele. Wanatamba saizi sababu:

1. Upeo mdogo wa uelewa wa wananchi. Nagalia elimu ilivyo hovyo. Wanapenda sana iwe hivyo ili waendelee kutawala mbumbumbu. Thats y hata waziri wa natu wake wakiboronga vipi, hawawajibishwi sabab faulire ya elimu ndie mtaji wao.
2. Propaganda. In 2000, nilibahatika kuangalia Mengi akionyesha ktk ITV yake vita ya Angola. alikuwa ana preach kwamba tukichagua upinzani, maafa yatatokea. Hadi leo watu wengi wanaamini hivyo. Vipindi kama MAFANIKIO YA UTAWALA WA NNE ni cheap propaganda tool wanatumia na kwakuwa watu epeo wao wa kuelewa ni mdogo, wanaamini kwamba mafanikio yapo. Hawajuii kwamba mafanikio hawawi preached jukwani au katika luninga bali yanaokena kwa macho. Si lazima tuamibiwe, tunaona wenyewe.
3. Mazingira. Hadi leo tuna katiba ya chama kimoja. NEC iko chini ya rais. Uchagizi mdodo unaendeshwa na serikali hiyo hiyo wakati nayo inachiriki nk.
4. Ukosefu wa uzalendo. Agalia wa bunge wa CCM wanavyoshabikia hoja kata kama nizakijinga ila kama zinamanufaa kwa chama chao, wanaunga mkono. Wanaendesha bunge kwa kulinda chama chao.
5. Kushindwa kwa upinzani kuungana. Nasemaga, tunaitaji CUF na Chademu tu kuungana ili tuitoe CCM madarakani.
6.Uchaguzi unakuwaga na mizengwe. Wizi wa kura.
Sasa kwakujibu swali lako kama CCM itatawala milele au la, nasema hapana. 1991 nikuwa nchi ya jirani, Zambia. Wazambia walikuwa wanafikiri UNIP itatawala milele. Siku mmoja watu waliichoka na wakafanya mapindizi. Siku mmoja watu watasema hapana. Tumechoka ahadi za uongo.
Tusibiri

Mkuu swali la FMES gumu sana, naona unalijibu kisiasa kwanza nikujibu kwa kinamba kama hoja zako zilivyokaa kinamba!

1. Si kweli tena futa kabisa kuwa watanzania hawana akili! hayo ni maneno ya walioshindwa kazi. Niambie akina Mkwawa, Rumanyika, Mirambo, Kimweri, Mputa , Mangi sina, Mandara walisoma vyuo gani na wafuasi wao walikuwa na elimu gani? still akina Mkwawa walipigana na wakoloni, mpaka watu wakaja na ideology za majimaji kuonyesha tu watu wanavyojali! Si kweli kabisa swala la elimu, maana walio na elimu ndio hawanyeshi lolote, hakuna wa kuwaongoza tu, na hawawezi kuamka peke yao lazima wawe na mchungaji. Kuna watu walijibatiza majina ya ukombozi wakabeba dhamana ambayo; FMES anauliza kwa kuonyesha wameshindwa, na sisi tumo humo tumeshindwa pia. Mimi na wewe sio mbumbumbu mkuu!

2. Mengi kweli analaumiwa na atalaumiwa kwa kuonyesha vita ya Burundi na Rwanda mwaka, lakini kishindo cha Mrema mbona kilifuta yote hayo?? tukubali hajatokea kama Mrema mpaka leo!

3. KATIBA kuwa ya chama kimoja ni jukumu la vyama vya upinzani kuibadilisha mbona CUF Zanzibar wamefika pazuri mkuu? sema vyama vimelala !!

4. Haswaaa hilo ndio jibu!

5.Jibu tena, japo wana sera tofauti , so kuungana kuiondoa CCM hakutaleta tija baadae maana watagombana tu

6. Uchaguzi hauna mizengwe, wakala wa vyama vyote huwa wanakuwepo kwenye vituo vya kura kuhakikisha mabox kabla ya kura na kuhesabu kura!! mbona wako kimya?
 
- Wakuu wote JF heshima mbele sana, nimekuwa nikisumbuliwa sana na swali moja tunalalamika sana kuhusu matatizo ya uongozi wa CCM kwa taifa letu. Ni miaka 47 sasa CCM imetutawala Tanzania, nikiangalia historia inaonekana wenzetu yaani wazee wa zamani pamoja na uchache wao kielimu na tools, sio siri kwamba walikuwa wanatoa upinzani mzito sana kwa TANU/CCM kuliko sisi vijana wa sasa.

- Inaonekana kama wenzetu hawakuwa na maneno mengi sana, ila walikuwa na vitendo vizito sana na siku zote walikuwa wakiilaza macho serikali na CCM, tizama kina Anangisye, Mwabulambo, Kambona, Bibi Titi, Kassanga Ntumbo, wazee kama kina Chipaka, Magee, Lugangira yaani huyu pamoja na kumfunga jela alitoroka anyways, Nyirenda na wengineo, I mean mbona inaonekana kama they were more effective kuliko sisi wenye akili sana katika kuipigisha magoti serikali na TANU/CCM? Kila walipomaliza kufanya vitu vyao kuna mabadiliko flani yalikuwa yakifanyika kuitikia vilio vyao kuhusu taifa, infact ni wao ndio walishinikiza Sokoine kupewa power na ile vurugu ya mafisadi, sasa nini kimetokea sasa tena ukitilia maanani kwamba sisi tuna tools nyingi in our hands zaidi ya walizokuwa nazo wao! Hebu soma historia yetu utasikia kila wakati kulikuwa na tafrani somehow somewhere!

- Tuna vyama vingi vya siasa, tuna uhuru wa kuongea na kuandika, I mean wale hawakuwa na yote haya lakini they were more effective na vitendo vyao bubu kuliko sisi, WHY? Hebu tuambiane nini challenge ya maana iliyowahi kufanyika against CCM na serikali yake toka tuingie vyama vingi Mwaka 1995 to this date katika kuwafahamisha kwamba wananchi tumechoka na upupu mwingi wanaoufanya mpaka kuwashitua ili watusikilize kama wale wenzetu wa zamani?

- I mean I could be wrong vile vile, lakini this is what I see, we are just not effective enough or convincing to watawala, WHY? Halafu kumbuka kwamba milele ni pale tu mwisho wa maisha yako unapofika na sio anything esle!

Respect.

FMEs!
Sasa wewe kama unatetea Mramba unashangaa nini?
 
Na wewe ngoja ujibiwe kwa namba.
1.Mifano yako ya akina Mkwawa haijatulia. Inaonekana ni kati ya wale watu wanaoamini kuwa kusoma ndio kuwa na akili. Hiyo futa kabisa kichwani mwako. Ni ukweli usiopingika kuwa wapiga kura wengi hawana akili. Huwezi mtu ukawa na akili timamu ukapewa kanga au kofia ukatoa kura yako. Huko ni kukosa akili. Pilau ya siku moja kama unaakili timamu haina thamani ya kura. Hao machifu uliowataja wangekuwa na akili kama za wapiga kura wengi wasingepambama. Walikuwepo wasiokuwa na akili kama Mangngo wa Msovero. Shanga tu zilitosha kutoa nchi ndio kama hao wapigakura walio wengi.
2. Hata kama hajatokea kama Mrema demage ilishafanyika na hapo ndio tunarudi wa kwa wapiga kura kuwa ni mbumbumbu wasiotumia vichwa vyao kufikiri vinginevyo wangeelewa kuwa hizo ni propaganda tu.
3. unaelewa utaratibu wa kubadilisha Katiba wewe? Bunge! Nani anashikilia Bunge? Ebu tueleze CUF wemefika pazuri wapi? Halafu kwani CUF kama ndio wataalam kwani Bara hawapo?
4. Kama unajua kuwa ukosefu wa uzalendo ndio jibu sasa inakuwaje unalalamikia vyama vya upinzani?
5. Watagombana kwa sababu ya sera? Mbona CCm mwenyekiti wao alisema sera hazitekelezeki na wengine wakasema zinatekelezeka bado walikaa pamoja? Haya maswala ya sera ni mismiati tu ya wanasiasa. Sera ni moja tu, Usitawi wa jamii ya Watanzania
6. Eti uchaguzi hauna mizengwe! ptuh! Temea mate chini na uache kututukana hapa. Tuanzie mwaka 1995 hivi kwa nini Dar uchaguzi ulirudiwa? Huko Zanzibar ni lini CCm ilishinda? Wabunge wangapi waliondoshwa kwenye ubunge baada ya matokeo kutenguliwa? Sasa kama hivyo vyote si mizengwe kwako mizengwe ni ipi?
 
- nimekuwa nikisumbuliwa sana na swali moja tunalalamika sana kuhusu matatizo ya uongozi wa CCM kwa taifa letu.- I could be wrong vile vile, lakini this is what I see, we are just not effective enough or convincing to watawala.

Respect.

FMEs!
Mkuu FME's ...
kumbe hili la CCM kutawala milele ndio umeliona sasa na kuliuzia swali!?.
Kumbe umekuwa ukisumbuliwa sana?.
Kumbe 'tunalalamika sana kuhusu matatizo ya uongozi wa CCM kwa taifa letu'!.
'we are just not effective enough or convincing to watawala' kumbe tunatakiwa kuwa effective enough kuwa convince watawala wetu!.
Maadam pia umekubali, ' you could be wrong', then,
You are wrong Mzee FMEs.

Kwenye post zangu huko nyuma nimeshasema sana tena sana tuu kuwa CCM itatawala milele, as long as Watanzania tukiendelea kulala, kama tunavyolalaga.

Nilisema kuna baadhi ya maeneo CCM inachaguliwa sio kwasababu watu hawaipendi, bali kwasababu CCM is the one and only party they have known tangu wamezaliwa. There is simply no altenative.

Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho, Watanzania wameanza kuamka, itafikia muda muafaka wote wataamka, and by then, altenative itakuwepo na CCM itaangukia pua.

Issue inabaki ni lini, its only a matter of time, with the right people and the right strategies and the genuine sacrifices, The Almighty atawakomboa Watanzania toka utumwani CCM.

Waisraeli waliishi miaka 400 utumwani Misri na kusafiri kwa miaka 40 jangwani, ili waifikie ile nchi ya ahadi, na wengi hawakuingia akiwemo kiongozi wao Musa, muda wote huo, bado haujaitwa milele. Milele ni kwenye uzima wa milele tuu, mengine yote yanamwisho.

Nakuahidi FME's, utalishuhudia anguko la CCM kabla ya milele yako, japo siujui umri wako, mimi ni muumini wa eternal life, na life after life. Death is only a change of state, spirit never die, hivyo for sure 100% utalishuhudia anguko la CCM!.
 
Kamwe CCM haiwezi kutawala milele ila kwa sasa bado tunawapima wa kuwapa uongozi, iwa CHADEMA, CUF, kiufupi ni kwamba tumeichoka CCM na sisi kama watu hatuna njia nyingine ila bado tunaipima hawa wengine, ni kwamba hata Mungu naye ana mpinzani wake sembuse CCM
 
Wakati wa mwalimu vipaumbele vya taifa vilikuwa clearly defined na watu walikuwa accountable.

Kule hakukuwa na kumuonea mtu haya. Naamini uhuru wa kuongea ulikuwepo lakini ukiwa na manufaa kwa taifa pasipo kuwa na chembe ya ubinafsi, ukabila na hata udini.

Kwasasa mtu anashindwa kuchukua hatua kwa kuwa kuna mtu au kikundi cha watu kimefaidika na uozo uliopo. Dhamira haikusukumi kuchukua hatua.

Asante FMES kwa huu mjadala.
 
Mkuu FME's ...
kumbe hili la CCM kutawala milele ndio umeliona sasa na kuliuzia swali!?.
Kumbe umekuwa ukisumbuliwa sana?.
Kumbe 'tunalalamika sana kuhusu matatizo ya uongozi wa CCM kwa taifa letu'!.
'we are just not effective enough or convincing to watawala' kumbe tunatakiwa kuwa effective enough kuwa convince watawala wetu!.
Maadam pia umekubali, ' you could be wrong', then,
You are wrong Mzee FMEs.

Kwenye post zangu huko nyuma nimeshasema sana tena sana tuu kuwa CCM itatawala milele, as long as Watanzania tukiendelea kulala, kama tunavyolalaga.

Nilisema kuna baadhi ya maeneo CCM inachaguliwa sio kwasababu watu hawaipendi, bali kwasababu CCM is the one and only party they have known tangu wamezaliwa. There is simply no altenative.

Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho, Watanzania wameanza kuamka, itafikia muda muafaka wote wataamka, and by then, altenative itakuwepo na CCM itaangukia pua.

Issue inabaki ni lini, its only a matter of time, with the right people and the right strategies and the genuine sacrifices, The Almighty atawakomboa Watanzania toka utumwani CCM.

Waisraeli waliishi miaka 400 utumwani Misri na kusafiri kwa miaka 40 jangwani, ili waifikie ile nchi ya ahadi, na wengi hawakuingia akiwemo kiongozi wao Musa, muda wote huo, bado haujaitwa milele. Milele ni kwenye uzima wa milele tuu, mengine yote yanamwisho.

Nakuahidi FME's, utalishuhudia anguko la CCM kabla ya milele yako, japo siujui umri wako, mimi ni muumini wa eternal life, na life after life. Death is only a change of state, spirit never die, hivyo for sure 100% utalishuhudia anguko la CCM!.
Pasco,
Wewe unasimamia wapi hasa? kuna sehemu umesema kuwa hata huko nyuma (uliwahi kuwa shekhe Yahya lol) na kutabiri kuwa CCm itatawala milele. Lakini aya zilizofuata umegeuka nyuzi 360 nakugundua kuwa hakuna tawala itakayo dumu milele. Na huo ndio ukweli wenye na umesapoti na mifano hali. Kama iliangu dola ya Kirumi ndio iwe CCM. Umenena vema sana. Wanachofanya ni kuchelewasha tu anguko lao lakini lipo linakuja.

Wakati wa mwalimu vipaumbele vya taifa vilikuwa clearly defined na watu walikuwa accountable.

Kule hakukuwa na kumuonea mtu haya. Naamini uhuru wa kuongea ulikuwepo lakini ukiwa na manufaa kwa taifa pasipo kuwa na chembe ya ubinafsi, ukabila na hata udini.

Kwasasa mtu anashindwa kuchukua hatua kwa kuwa kuna mtu au kikundi cha watu kimefaidika na uozo uliopo. Dhamira haikusukumi kuchukua hatua.

Asante FMES kwa huu mjadala.
Hili ndilo neno la Selous. Mwenye masikio ya kusika na asikie.
 
Na wewe ngoja ujibiwe kwa namba.
1.Mifano yako ya akina Mkwawa haijatulia. Inaonekana ni kati ya wale watu wanaoamini kuwa kusoma ndio kuwa na akili. Hiyo futa kabisa kichwani mwako. Ni ukweli usiopingika kuwa wapiga kura wengi hawana akili. Huwezi mtu ukawa na akili timamu ukapewa kanga au kofia ukatoa kura yako. Huko ni kukosa akili. Pilau ya siku moja kama unaakili timamu haina thamani ya kura. Hao machifu uliowataja wangekuwa na akili kama za wapiga kura wengi wasingepambama. Walikuwepo wasiokuwa na akili kama Mangngo wa Msovero. Shanga tu zilitosha kutoa nchi ndio kama hao wapigakura walio wengi.
2. Hata kama hajatokea kama Mrema demage ilishafanyika na hapo ndio tunarudi wa kwa wapiga kura kuwa ni mbumbumbu wasiotumia vichwa vyao kufikiri vinginevyo wangeelewa kuwa hizo ni propaganda tu.
3. unaelewa utaratibu wa kubadilisha Katiba wewe? Bunge! Nani anashikilia Bunge? Ebu tueleze CUF wemefika pazuri wapi? Halafu kwani CUF kama ndio wataalam kwani Bara hawapo?
4. Kama unajua kuwa ukosefu wa uzalendo ndio jibu sasa inakuwaje unalalamikia vyama vya upinzani?
5. Watagombana kwa sababu ya sera? Mbona CCm mwenyekiti wao alisema sera hazitekelezeki na wengine wakasema zinatekelezeka bado walikaa pamoja? Haya maswala ya sera ni mismiati tu ya wanasiasa. Sera ni moja tu, Usitawi wa jamii ya Watanzania
6. Eti uchaguzi hauna mizengwe! ptuh! Temea mate chini na uache kututukana hapa. Tuanzie mwaka 1995 hivi kwa nini Dar uchaguzi ulirudiwa? Huko Zanzibar ni lini CCm ilishinda? Wabunge wangapi waliondoshwa kwenye ubunge baada ya matokeo kutenguliwa? Sasa kama hivyo vyote si mizengwe kwako mizengwe ni ipi?

Mkuu umejibu vyema, you have actually confirmed kuwa CCM watatawala milele!

kuwa sisi ni
1. Mbumbumbu
2. Hatuna Uzalendo
3. Katiba haiwezi kubadilika
4. Uchaguzi una mizengwe

why bother then with other political parties? kwa nini tusiseme tuendelee na CCM kwa sababu tuna hivyo vilema? maana tungeokoa fedha za ruzuku tukajenge shule na kununua madawati

Haukunielewa kuwa majibu yangu yoote yalionyesha tatizo lipo na lina weza kutibika, tuondoe excuse. Mkuu umekuja na kusema matatizo yapo na hayatatatulika!

so FMES is correct CCM will rule forever sawa mkuu Monsignor?
 
- Exactly ninachosema kwamba wazee wa zamani walikuwa very effective katika kuishinikiza TANU/CCM na serikali, as opposed na sisi wakuu wa sasa.

Respect.

FMEs!

Kulikuwa na wazee majasiri sana enzi za TANU ambao mfano wake hakuna tena, walimuheshimu Mwalimu lakini hawakumuogopa ; wakina Rajab Diwani, Masudi Mtandika. Wenyeviti wa TANU/CCM pia walikuwa na msimamo na walikuwa hawaogopi kusema kile walichoamini; walikuwepo wakina Enos Mwangoka toka Mbeya, Budodi toka Mwanza , Kaaya toka Arusha na wengine wengi ambao walitetea maslahi ya wananchi na si matumbo yao kama wenyeviti wa Mikoa wa CCM wanavyojidhallilisha mbele ya MAFISADI kwa kuhongwa ili wakawatete dhidi ya madhambi yao kwenye vikao vya chama!!
 
Then Siasa za Tanzania ni very fragmentation hata JK wakati anaingia madarakani alisema ataboresha mfumo uliopo kwenye siasa lakini mpaka leo mambo yale yale, Hivyo jua kuwa tatizo jingine ni katiba naye na kuwa na CHAMA DUME kwenye mfumo dhaifu Sana kwenye siasa, una GIANT CCM na vyama vidogo sana dhaifu na kushindana nalo. Kuna haja ya kutazama Tume ya Nyalali na tume nyingine mapendekezo yake walisema mengi sana, UKIWA NA VYAMA DHAIFU VYA UPINZANI HIVYO HUZAA AU KUFANYA SERIKALI DHAIFU> Hivyo ukiona mtu anasema kuwa Tanzania ni dhaifu kwa upinzani basi jua na serikali dhaifu, ndio maana unaona matatizo sana katika EPA, Richmond, na madudu mengine mengi na Bunge
 
Kama taifa tumeshapoteza mwelekeo. Lakini serikali (CCM) iko bize kutusadikisha kwamba njia tunayopita ndio yenyewe.

Natoa mfano hapa chini kuonyesha kiwango cha uelewa wetu.

Hivi kuna mmoja wenu kawahi jiuliza juu ya msemo huu "Malaria haikubaliki Tanzania"; halafu kuna picha ya Tz iliyozungushiwa chandarua katika tangazo hilo.

Kama uelewa wetu ndio huu kwamba suluhisho la tatizo sugu la malaria ni chandarua, itakuwa miujiza kuja na mikakati ya kuipa CCM changamoto.

Importing mosquito nets implies creating jobs for the exporter country; outflux of foreign currency; and indeed improving quality of life of people of the exporter country.

Ni upumbavu mtupu.
 
- Wakuu wote JF heshima mbele sana, nimekuwa nikisumbuliwa sana na swali moja tunalalamika sana kuhusu matatizo ya uongozi wa CCM kwa taifa letu. Ni miaka 47 sasa CCM imetutawala Tanzania, nikiangalia historia inaonekana wenzetu yaani wazee wa zamani pamoja na uchache wao kielimu na tools, sio siri kwamba walikuwa wanatoa upinzani mzito sana kwa TANU/CCM kuliko sisi vijana wa sasa.

- Inaonekana kama wenzetu hawakuwa na maneno mengi sana, ila walikuwa na vitendo vizito sana na siku zote walikuwa wakiilaza macho serikali na CCM, tizama kina Anangisye, Mwabulambo, Kambona, Bibi Titi, Kassanga Ntumbo, wazee kama kina Chipaka, Magee, Lugangira yaani huyu pamoja na kumfunga jela alitoroka anyways, Nyirenda na wengineo, I mean mbona inaonekana kama they were more effective kuliko sisi wenye akili sana katika kuipigisha magoti serikali na TANU/CCM? Kila walipomaliza kufanya vitu vyao kuna mabadiliko flani yalikuwa yakifanyika kuitikia vilio vyao kuhusu taifa, infact ni wao ndio walishinikiza Sokoine kupewa power na ile vurugu ya mafisadi, sasa nini kimetokea sasa tena ukitilia maanani kwamba sisi tuna tools nyingi in our hands zaidi ya walizokuwa nazo wao! Hebu soma historia yetu utasikia kila wakati kulikuwa na tafrani somehow somewhere!

- Tuna vyama vingi vya siasa, tuna uhuru wa kuongea na kuandika, I mean wale hawakuwa na yote haya lakini they were more effective na vitendo vyao bubu kuliko sisi, WHY? Hebu tuambiane nini challenge ya maana iliyowahi kufanyika against CCM na serikali yake toka tuingie vyama vingi Mwaka 1995 to this date katika kuwafahamisha kwamba wananchi tumechoka na upupu mwingi wanaoufanya mpaka kuwashitua ili watusikilize kama wale wenzetu wa zamani?

- I mean I could be wrong vile vile, lakini this is what I see, we are just not effective enough or convincing to watawala, WHY? Halafu kumbuka kwamba milele ni pale tu mwisho wa maisha yako unapofika na sio anything esle!

Respect.

FMEs!
Ukiendele kujiuliza na kuuliza swalikama hilo bila kufanya chochote CCM itatawala milele.
 
-Tatizo kubwa ni kukosa mwamko na utashi wa uwajibikaji

-pia kuna vyombo vya muhimu kama baraza huru la vijana.Mabadilikoau mapinduzi yote muhimu duniani hufanywa na vijana.Nadhani vyama vya upinzani,wanaharakati mbalibmali walikubali kuwa turned down na ruling party katika hii ishu ya baraza huru la vijana

-kukosa uzalendo,kudumaa kimawazo na kuwa tegemezi kwa vijana ndiko kulikotufanya tufike hapa

-Still tunahitaji uhamasishaji,kutoa elimu ya uraia,wanaharakati kuongeza nguvu ktk mapambano kwa vitendo nk

-Mpaka sasa hivi nakiri kabisa CCM haijawahi pata serious challenge ingawa tunazo potentials zote za kuwapa changamaoto nzito.kinachohitajika ni kuunganisha nguvu na kuwa na misimamo

Hebu fikiria itakuaje pale ambapo tutapata mtu wa kusimmia kigezo kimnoja kitakachowaleta pamoja wanaharakati walioko upinzani,na walioko ndani ya CCM,Wanafunzi wa vyuo vikuu,wanahabari,wanasheria,wafanyakazi na wakulima pamoja against CCM? Ground kama za kutaka katiba mpya zinaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kuwaleta wanaharakati wote pamoja against government,kutakua na vuguvugu ambalo kwa kweli inaweza kuwa ndiyo mwanzo mpya wa upinzani wqenye nguvu na group hiyo hiyo inaweza kuanzisha au kuunganisha vyama vyote vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu
 
"For evil to flourish, it only requires good men to do nothing." Edmund Burke
 
-kama CCM watacheza rafu zote na kukandamiza haki zetu na sisi kubaki hivi hivi na haya tunayofanya tu si watazidi kutawala?kimsingi sisi ndio tunawapa hiyo fursa
 
Nakumbuka kama leo kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema kuwa Mmungu akitaka asitake CCM itatawala mpaka ulimwengu umalizike kama utamalizika.(kwa sasa anatajwa kugombea Urais kule Zanzibar)
 
Nakumbuka kama leo kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema kuwa Mmungu akitaka asitake CCM itatawala mpaka ulimwengu umalizike kama utamalizika.(kwa sasa anatajwa kugombea Urais kule Zanzibar)

Nadhani huyo ni mshirikina,ana dini? Anyway,hata katiba inatambua haki za wapagani
 
Pasco,
Wewe unasimamia wapi hasa? kuna sehemu umesema kuwa hata huko nyuma (uliwahi kuwa shekhe Yahya lol) na kutabiri kuwa CCm itatawala milele. Lakini aya zilizofuata umegeuka nyuzi 360 nakugundua kuwa hakuna tawala itakayo dumu milele. Na huo ndio ukweli wenye na umesapoti na mifano hali. Kama iliangu dola ya Kirumi ndio iwe CCM. Umenena vema sana. Wanachofanya ni kuchelewasha tu anguko lao lakini lipo linakuja.
Monsignor, niliyasema hayo baada ya kuhudhuria uchaguzi wa Busanda na nikayasema tena baada ya kuhudhuria uchaguzi wa Biharamulo.

Kila niliposema CCM itatawala milele, lilikuwa ni angalizo, kama Watanzania wataendelea kulala, sasa nina uhakika wanaanza kuamka.

Hata mimi binafsi nina vita kubwa sana ndani yangu, ninakabiliwa na kuamua, kati ya kuelekeza nguvu zangu kuwaamsha waliolala na baada ya hapo, kukubali matokeo ikiwemo maisha ya msoto kwa sana, ama nijikalie mbali na dirty games za politics na kuendelea kumtumikia kafiri nipate mradi wangu, bora mkono uende kinywani.

Inahitajika sacrifice ya upendo wa mshumaa kumulikia wengine, huku wenyewe ukiteketea, ama ujasiri kama wa Masiya, kwa kuteswa kwake sisi tunaponywa. Lazima tuwapate watu wengi zaidi ya Dr. Slaha wenye patriotisim na nchi hii kutupeleka kwenye ukombozi wa kweli.

For sure, CCM haitatawala milele yote!.
Monsignor msalimie Monsignora
 
- Wakuu wengi mliochangia ahsante sana, ila wengi mnaonekana kutonielewa kwenye hoja yangu ya msingi ya kichwa cha hii mada, ninasema hivi have we done enough kuwashinikiza watawala wetu kubadilika for the good of our nation na sisi wenyewe yaani the people? Kubadilisha mienendo yao ambayo inaimaliza taifa, na nikaongeza hivi mbona wazee wetu walikuwa na nguvu sana katika hili la kuwashinikiza viongozi wetu wa enzi hizo na waliwasikiliza, sisi mbona hawatusikilizi?

- Sasa jamani ninashangaa na majibu mengi ambayo hayana anything to do na ninachouliza, kama huna cha maana ni bora unyamaze ebo! hii mada ni about responsibility yako na yangu kwa taifa letu, sasa usilaumu wengine kwamba ni wajinga wewe mwenye akili umefanya nini kuwashinikiza watawala wetu kuwa they need to change, nimekupa mifano ya kina Anangisye, Mwabulambo, Jumbe, Seif Bakari, Seif Hamad, Bibi Titi, The Chipakas, Kambona, na wengineo wengi kwamba hawa watu stood up to the powers na wakasikilizwa, in the process wamefungwa, wameswekwa rumande, wamewekwa under house arrest, wamenyimwa kazi, wamekimbia nchi!

- Jamani ninarudia tena eti sisi tumefanya nini cha kuwashitusha watawala wetu wa sasa kwamba we are dead serious na demading a change, au ni Mtikila kuwapeleka serikali mahakamani na ishu ya wagombea binafsi, na Dr. Slaa na majina ya mafisadi basi, ndio tunategemea wabadilike au kutusikia?

- Je watawala wetu wa sasa wakisema hatuko serious ndio maana hawabadiliki watakuwa wanakosea? Can we for once take the responsibility in our hands badala ya kulaumu tu wengine! Tukubali kwamba either sisi ni waoga tunaotegemea wengine watufanyie au malalamiko yetu sio ya wananchi wengi wa Tanzania, I mean something is a miss haiwezekani tunalia this bad lakini watawala hawatusikilizi wala kutingishika, something is not right wakuu tujiangalie na tutafakari!

- And yes! I said it tujiangalie tena something is not right!

Respect.

FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom