Je, CCM Itatawala Milele Au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, CCM Itatawala Milele Au?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Feb 26, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Wakuu wote JF heshima mbele sana, nimekuwa nikisumbuliwa sana na swali moja tunalalamika sana kuhusu matatizo ya uongozi wa CCM kwa taifa letu. Ni miaka 47 sasa CCM imetutawala Tanzania, nikiangalia historia inaonekana wenzetu yaani wazee wa zamani pamoja na uchache wao kielimu na tools, sio siri kwamba walikuwa wanatoa upinzani mzito sana kwa TANU/CCM kuliko sisi vijana wa sasa.

  - Inaonekana kama wenzetu hawakuwa na maneno mengi sana, ila walikuwa na vitendo vizito sana na siku zote walikuwa wakiilaza macho serikali na CCM, tizama kina Anangisye, Mwabulambo, Kambona, Bibi Titi, Kassanga Ntumbo, wazee kama kina Chipaka, Magee, Lugangira yaani huyu pamoja na kumfunga jela alitoroka anyways, Nyirenda na wengineo, I mean mbona inaonekana kama they were more effective kuliko sisi wenye akili sana katika kuipigisha magoti serikali na TANU/CCM? Kila walipomaliza kufanya vitu vyao kuna mabadiliko flani yalikuwa yakifanyika kuitikia vilio vyao kuhusu taifa, infact ni wao ndio walishinikiza Sokoine kupewa power na ile vurugu ya mafisadi, sasa nini kimetokea sasa tena ukitilia maanani kwamba sisi tuna tools nyingi in our hands zaidi ya walizokuwa nazo wao! Hebu soma historia yetu utasikia kila wakati kulikuwa na tafrani somehow somewhere!

  - Tuna vyama vingi vya siasa, tuna uhuru wa kuongea na kuandika, I mean wale hawakuwa na yote haya lakini they were more effective na vitendo vyao bubu kuliko sisi, WHY? Hebu tuambiane nini challenge ya maana iliyowahi kufanyika against CCM na serikali yake toka tuingie vyama vingi Mwaka 1995 to this date katika kuwafahamisha kwamba wananchi tumechoka na upupu mwingi wanaoufanya mpaka kuwashitua ili watusikilize kama wale wenzetu wa zamani?

  - I mean I could be wrong vile vile, lakini this is what I see, we are just not effective enough or convincing to watawala, WHY? Halafu kumbuka kwamba milele ni pale tu mwisho wa maisha yako unapofika na sio anything esle!

  Respect.


  FMEs!
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,695
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Field Marshall ES,

  I disagree with you on those 5 words with red font above. the rest of the post I'm with you!
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0

  - Kasheshe, thanks fafanua japo kidogo ndugu yangu sijakupata1

  Respect.


  FMEs!
   
 4. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hawawezi tawala milele. Wanatamba saizi sababu:
  1. Upeo mdogo wa uelewa wa wananchi. Nagalia elimu ilivyo hovyo. Wanapenda sana iwe hivyo ili waendelee kutawala mbumbumbu. Thats y hata waziri wa natu wake wakiboronga vipi, hawawajibishwi sabab faulire ya elimu ndie mtaji wao.
  2. Propaganda. In 2000, nilibahatika kuangalia Mengi akionyesha ktk ITV yake vita ya Angola. alikuwa ana preach kwamba tukichagua upinzani, maafa yatatokea. Hadi leo watu wengi wanaamini hivyo. Vipindi kama MAFANIKIO YA UTAWALA WA NNE ni cheap propaganda tool wanatumia na kwakuwa watu epeo wao wa kuelewa ni mdogo, wanaamini kwamba mafanikio yapo. Hawajuii kwamba mafanikio hawawi preached jukwani au katika luninga bali yanaokena kwa macho. Si lazima tuamibiwe, tunaona wenyewe.
  3. Mazingira. Hadi leo tuna katiba ya chama kimoja. NEC iko chini ya rais. Uchagizi mdodo unaendeshwa na serikali hiyo hiyo wakati nayo inachiriki nk.
  4. Ukosefu wa uzalendo. Agalia wa bunge wa CCM wanavyoshabikia hoja kata kama nizakijinga ila kama zinamanufaa kwa chama chao, wanaunga mkono. Wanaendesha bunge kwa kulinda chama chao.
  5. Kushindwa kwa upinzani kuungana. Nasemaga, tunaitaji CUF na Chademu tu kuungana ili tuitoe CCM madarakani.
  6.Uchaguzi unakuwaga na mizengwe. Wizi wa kura.
  Sasa kwakujibu swali lako kama CCM itatawala milele au la, nasema hapana. 1991 nikuwa nchi ya jirani, Zambia. Wazambia walikuwa wanafikiri UNIP itatawala milele. Siku mmoja watu waliichoka na wakafanya mapindizi. Siku mmoja watu watasema hapana. Tumechoka ahadi za uongo.
  Tusibiri
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,695
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nina maanisha sidhani kama sisi tuna akili sana kuliko vijana wa Zamani... mimi nadhani walikuwa na akili zaidi yetu.... ni hayo tu mkuu....
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,860
  Likes Received: 22,910
  Trophy Points: 280
  ccm itakufa by time..
  wanachokifanya sasa hivi ni self destruction tu.
  hawawezi tawala milele.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,257
  Likes Received: 3,029
  Trophy Points: 280
  Uwezekano wa ccm kutawala milele upo kama hakutakuwa na mapinduzi ya namna moja ama nyingine.

  Siasa za kipindi cha mwalimu na za sasa hivi ni tofauti sana kwasababu kwasasa nchi ishauzwa na hakuna shinikizo lolote lile kutoka kwa mataifa makubwa ama wafadhili....Mashinikizo ambayo yalikuwa mengi zaidi kutoka kwa mataifa makubwa ya kibepari chini ya mwalimu kwasababu nchi ilikuwa bado haijauzwa.

  Kwasababu nchi imeshauzwa,basi hata uchaguzi usipokuwa wa haki hakuna atakayejali almuradi mikataba inasainiwa kwa terms za bwana wakubwa na vibaraka wao na si za wananchi.

  Na kwasababu wananchi ni waoga kwa visingizio vya amani nk,wengi wamekuwa wakitegemea mafisadi waone huruma na wabadilike,wengine wakitegemea kuwa wale wasiokuwa mafisadi watawatimua mafisadi toka kwenye chama chao kinachotawala....Hayo yote haina maana kuwa chama kitashindwa uchaguzi,cha msingi ni kama uchaguzi huo utakuwa wa haki.

  Hata kama hayo yote yatatokea ama kutotokea,bado kushindwa kwa ccm si rahisi zaidi kwasababu tu ya kuwa na vyama vingine vya upinzani,rather demokrasia ya kweli ndiyo itakayoleta changamoto kwa wananchi kuweza kuwachagua viongozi wanaofaa.

  Wengi wa wananchi wanaongozwa na nidhamu ya woga haswa kuhusiana na upotevu wa amani....Kama hakutatokea mabadiliko ya kweli ndani ya ccm,uwezekano wa wao kuondolewa madarakani kwa sanduku la kura ni mdogo,na kwamaana hiyo kuna uwezekano wakatawala milele unless otherwise kuna mapinduzi ya aina moja ama nyingine....Uwezekano wa kupata mabadiliko ni lazima uanzie within na sio nje tena kama ilivyokuwa huko nyuma,hata wakati wa mwalimu waliokuwa wakipinga hawakuwa na sapoti kubwa sana ya wananchi lakini walikuwa na nguvu kwasababu ya siasa za wakati ule za kibepari dhidi ya siasa za mwalimu....Tofauti kwa sasa ni kwamba sapoti ya wananchi inahitajika kuliko wakati mwingine wowote kwenye historia ya Taifa letu,nadhani kuliko hata wakati wa ukoloni kwasababu wakoloni na vibaraka wao hawakuwa wengi kama mafisadi na vibaraka wao walivyo kwasasa.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,490
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kasheshe,
  Nakukubali. Kuwa na akili si kusoma sana. Kuna wazee kule kijijini kwetu nilipokuwa mdogo hawakuwahi kwenda shule. Lakini walikuwa na busara sana katika mambo ya maisha. Nilijifunza mengi kutoka kwao kuliko nilivyojifunza shuleni.
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,257
  Likes Received: 3,029
  Trophy Points: 280
  Nilidhani FMES aliteleza tu....Hata hivyo sikubalini na wewe wala yeye kwenye pointi hii kuhusu kuwa "Hawa walikuwa na akili zaidi ya wale" kutokana na sababu hizo alizozitoa FMES kuhusiana na yanayotokea kwenye siasa za Taifa letu.

  Kama Taifa halina dira wala mwelekeo,hakuna mwenye akili wala nani atakayeweza kufanyiwa tathmini kwa chochote kile kuhusiana na mwelekeo wowote ule,kwa mantiki hiyo basi,ni bora tuangalie hiyo situation ya kutokuwa na dira wala mwelekeo ilianzia wapi haswa,ndipo utakuja kuona ni kama mbio za vijiti tu wamepokezana na hakuna cha kusema kuna waliokuja wapya ambao hawafanyi vizuri kama wale waliokuwepo before kwasababu it is simply a race to nowhere!Certainly everything is now different,the way we run our politics na mambo mengi tu,tena tuna multiparty sasa and that should also be put into consideration.
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Mushi, tusikimbie vivuli vyetu, tumefanya nini serious cha kuwashitua CCM kwamba we are dead serious? Tizama wazee wa zamani kina Jumbe, Seif na Bakari kidogo wavunje Muungano, maambo yalimalizwa kichini chini lakini fukutu lake wote tulilipata, kina Omar Juma wakapewa umakamu wa Rais wa Jamhuri!

  - Au kutaja majina ya mafisadi ndio a serious one? I mean tukubali ukweli tu kwamba wa zamani walikuwa wametuzidi maarifa kina Abdulrahman Babu, Mhafudh hao walikuwa moto wa kuotea mbali sana, sio kina Mrema waganga njaa!

  - Mushi ulizia kina Anangisye, Chipaka, Bibi Titi, kina Bayona hawa hawakuwa kama sisi blah! blah! tu wao waliitikisa serikali na ikawasikiliza, inasadikiwa hao ndio waliompelekea Mwalimu kuondoka mapema kwenye power!

  Respect.


  FMEs!
   
 11. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  KILA CHENYE MWANZO KINA MWISHO...tatizo mwisho huo utafika lini na kwa faida ya nani!
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Mwisho ni pale bin-adam mmoja unapokufa that is it ndio milele yenyewe, yaani it is over sasa kama unapofika mwisho wa maisha na bado CCM iko kwenye power, ndio milele yenyewe hiyo, yaani umetawaliwa na CCM mpaka miwhso wa dunia, au?

  Respect.


  FMEs!
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,257
  Likes Received: 3,029
  Trophy Points: 280
  Nakubali mkuu kuhusiana na uzalendo wa watu hao,lakini mwalimu alikuwa na hofu kubwa zaidi na wapinzani wake nyakati hizo kwasababu kulikuwa na upinzani mkubwa sana kati ya ubepari na socialism,wapinzani wake wa ndani waliliona hilo na wali exploit situation,hata situations kama za Kambona kupewa ukimbizi nk ni mfano hai,ndio maana nikasema hapo nyuma kuwa tofauti na sasa ni kuwa nchi imeuzwa na ndiyo maana hata nchi wafadhili wanatoa sifa tu licha ya ufisadi wa wazi wazi ambao ushahidi upo hadi nchini mwao.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Exactly ninachosema kwamba wazee wa zamani walikuwa very effective katika kuishinikiza TANU/CCM na serikali, as opposed na sisi wakuu wa sasa.

  Respect.


  FMEs!
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Individualism, selfishness na lack of patriotism ndiyo vinatusumbua vijana wa sasa. Lakini make no mistake some of us wazee wetu walisacrifice in their life time kupambana na hii system to an extent of neglecting/ sub-caring their families. They just perished as unrecognised and unsang heros. As such us the siblings we just selfishly feel/ think it is a turn for others kupigania taifa letu. Just going back to the previously highlighted reasons.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Totally agreed!

  Respect.


  FMEs!
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 135
  Kuna ukweli ndani ya maneno ya FMES. Vijana wa sasa tuna tatizo moja kubwa la kutokuwa na uzalendo kwa nchi yetu. Tunadanganywa na tunajua kuwa tunadangaywa lakini tunaishia kusema ewala, tunaibiwa na tunajua kuwa tunaibiwa na tunaishia kusema eeewala.

  Kila siku huwa nakasirika sana nikisikia jinsi vijana wa tanzania wanavyojitapa kwa kutembelea nchi nyingi majuu, na kutanua majuu ambako kwingine wanaoneana niggers tu, lakini hakuna la maana wanalofanya kuifanya japo robo ya Tanzania iwe kama majuu.

  Naamini kabisa kuwa wazee wetu ambao zamani walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuhamia majuu, waliamua kubaki Tanzania kufanya kazi at least kuifanya Tanzania ipige hatua, kuwafanya watu at least wawe na decent life, lakini tulizubaa na kuacha nchi yetu iingine mikononi mwa wasio stahili, na sasa wenegine wenye uwezo wa kutoa mchango kwa taifa wamebaki kupiga kelele kutoka nje, without any big impact.

  Ni Kolimba pekee aliyejaribu kui-shake system, na Mrema kwa mbali kidogo lakini serikali ilichowafanya kila mtu anajua.

  Vijana tunatakiwa kutoa mchango mkubwa zaidi wa kuifanya Tanzania iwe better, current CCM kuendelea kutawala hali itazidi kuwa mbaya.
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Mkuu agreed, ninachosema ni hvi hawa watoto wetu siku moja watatuuliza tulifanya nini kuwaonyesha watawala wetu kua haturidhiki na wanayotufanyia, eti tutasema nini tulitaja majina ya mafisadi that is all?

  - Tizama kina Kambona, waliona bora hata kukimbia nchi, kina Anangisye wamekaa detention for a very longtime kwa sababu ya kui-denounce political system ya their time, lina Babu walihama nchi na kwenda kuwa wakimbizi huko nje, I mean angalau kina Seif Hamad wanajitahidi kumkosesha tembo usingizi, lakini sisi mineno mingi halafu jioni tuko nao hao hao watawala kwenye dinners na kufungua zahanati, hao kina Anangisye, usingeweza kuwaona na watawala waliowaona kuwa ni mwiba kwa taifa!

  - Halafu mind you enzi zao ilikuwa ni marufuku hata kuonyesha kwamba huitaki serikali au siasa zake, hawa walikuwa wakisumbuliwa na mashushu all the times, lakini hawakuogopa wengine kina Mwabulambo mpaka wakaishia kuchapwa viboko na Mwalimu Ikulu, mkuu hawa they were fighting for us yaani wananchi wa baadaye, kina Mtei wakaacha mpaka kazi za kifahari wakikataa kuburuzwa, wengine kina Jumbe wamewekwa mpaka kwenye house arrest, this were our heros jamani! Kina Professor Rweyemamu, wao wakaona hata kuhama nchi kabisaa!

  - Leo we have everything in our hands, lakini effective hakuna, nilisoma mahali eti wabunge wa sasa bwana sio kama wa zamani, garademiti! show me wamefanya nini cha kutisha for the future ya watoto wetu? Makongamano nonsense kila kukicha yasiyo na faida yoyote wka taifa!

  Respect.


  FMEs!
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,257
  Likes Received: 3,029
  Trophy Points: 280
  Mkuu FMES,naomba pia nisisitize kuwa kuna baadhi ya maneno kwenye posting yangu ambayo yanaleta utofauti zaidi na tafsiri hiyo uliyoitoa hapo juu,kwamba effectiveness yao ya ufanyaji kazi ni ya tofauti na sasa kwasababu nchi ilikuwa haijauzwa,ni tofauti sana na wakati huu ambapo viongozi wengi ni wwenye kujali maslahi binafsi na ni kama sera ya chama kwasababu wanaambiwa wakishapata wawagawie na wananchi.

  Pia nilizungumzia Taifa kutokuwa na dira wala mwelekeo.Hayo yote yanaleta utofauti mkubwa sana,hayo ni tisa,kumi this time ni multi party system tofauti na wakati wa mwalimu,na pia chama tawala kinatumia mbinu za kukabiliana na wapinzani ni za tofauti na wakati ule wa utawala wa chama kimoja,sasa pesa ndio ndio the root to all evils na upinzani wenyewe hauna ubavu wa kupambana na siasa za watu wanaoogopewa hadi na serikali na dola zake ie polisi,hata Kamanda Mwema alisema jeshi hilo halina ubavu wa kuwakamata mafisadi hao,wale ambao ndio walikuzwa na hao wazee wetu na kuaminiwa ndio wanasema maneno kama hayo,ni kama ule mchezo wa zamani wa utotoni unaosema "Simba ni mkali ameua baba,ameuma mama....Haidhuru kimbieni" Hapo kila mtu anatimua mbio tu.

  Kauli kwamba mafisadi wakishughulikiwa nchi itayumba ni dalili za wazi kwamba we're in deep trouble.

  Kama alivyosema Nyambala hapo nyuma,ni kweli wakati huu individualism ndio imetawala na ukiangalia kwanini,jibu ni lile lile kuwa nchi haiko mikononi mwa wananchi,yani kwa kifupi "Imeuzwa"
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 135
  Kila nikikaa na hawa waheshimiwa wabunge wanajua wazi kuwa tatizo liko wapi, na sio kama kweli hawalioni, wanaliona. Lakini ajabu ikifika wakati wa kupiga kura wanapiga kura tofauti kabisa na conscious yao, eti sababu kuwa wanaiogopa CCM, yaana inakwenda kinyume na maslahi ya chama, au maslahi ya watu fulani ndani ya chama. Sasa tumeanza kuona kuwa maslahi ya wawili ndani ya Chama, yanaharibu sifa ya wanachama milioni mbili, lakini still kwa kuwa milioni 2 bado wamelala, bado wawili wanaendelea kupeta tu.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...