Je, Bunge lina uwezo wa kisheria kusogeza uchaguzi baada ya miaka mitano ya kikatiba kuisha?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Hivi bunge linaweza kutunga sheria na kubadilisha katiba inayosema kila miaka mitano ni uchaguzi.

Zipo tetesi watawala wanajipanga kuusogeza uchaguzi kisa Korona lakini mamlaka wanayatoa wapi?

Hata nec huo ubavu hawana labda kibali kitolewe na mahakama kuu na hata mahakama kujadili matukio yasiyoweza kuthibitika kama ya mwezi wa Oktoba Korona itakuwaje haiwezi kuyakadiria

Labda, bunge libadili katiba na kujipa mamlaka ya kujiongezea muda wa kuendelea kulamba kodi zetu bila ridhaa ya wapiga kura

Swali la kujiuliza watawala wanaiogopa Korona au wanaiogopa ghadhabu ya mpiga kura maana miaka mitano kwisha na hakuna la maana kwa mpigakura?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa taarifa yako baada ya Magufuli kuingia madarakani, katiba imekuwa sawa na novel, yeye ndio katiba na hakuna wa kuhoji. Atakachotaka yeye kitafanyika, kikwazo pekee kwake sio katiba yetu wala wananchi, labda wazungu wambane.
 
Mnaweweseka tu! Mara hamtapiga kura sasa tena mmeanza kusema uchaguzi utasogezwa mbele. Kasome katiba nani mwenye mamlaka ya kuahirisha uchaguzi acha mapovu mkuu!!
 
Haya tusubiri October sisi tutapiga.

Sio kupiga tu, hata ukiona unachelewa, mchukue mkeo na ndugu zako wiki hii, mkakae kwenye vituo vya kura kabisa ili mpige kura vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Ni kweli bunge lina uwezo kisheria wa kusogeza Uchaguzi Mkuu kutokana na tafsiri ya maneno VITA DHIDI YA ADUI!

Ibara ya 42(4) ya Katiba ya Tanzania 1977 inasema, ''Iwapo Jamhuri ya Muungano inapigana vita dhidi ya adui na Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi, Bunge laweza mara kwa mara kupitisha azimio la kuongeza muda wa miaka mitano uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii isipokuwa kwamba muda wowote utakaoongezwa kila mara hautazidi miezi sita''.

Maneno VITA DHIDI YA ADUI yamebeba ujumbe ambao kwa maoni yangu ni mpana na tafsiri yake ni mjadala wa kisheria!

Dhana ya kusema Uchaguzi Mkuu utaahirishwa kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya Corona ni dhana yenye fikra hasi kwa sababu hatujui hata baada ya mwezi mmoja hali halisi ya maambukizi itakuwa katika kiwango gani!

Tuachane na fikra hasi ambazo hazina manufaa kwa ustawi wa taifa letu!
 
MsemajiUkweli,
Tungekuwa na bunge imara wangalau hivi vifungu vya sheria tungeweza kuona vinavyofanya kazi, lakini kwa sasa hilo bunge ni kama genge la wasaka mlo wanaoweza kutii amri ya mlevi yoyote wa madaraka.
 
Hivi bunge linaweza kutunga sheria na kubadilisha katiba inayosema kila miaka mitano ni uchaguzi.

Zipo tetesi watawala wanajipanga kuusogeza uchaguzi kisa Korona lakini mamlaka wanayatoa wapi?

Hata nec huo ubavu hawana labda kibali kitolewe na mahakama kuu na hata mahakama kujadili matukio yasiyoweza kuthibitika kama ya mwezi wa Oktoba Korona itakuwaje haiwezi kuyakadiria

Labda, bunge libadili katiba na kujipa mamlaka ya kujiongezea muda wa kuendelea kulamba kodi zetu bila ridhaa ya wapiga kura

Swali la kujiuliza watawala wanaiogopa Korona au wanaiogopa ghadhabu ya mpiga kura maana miaka mitano kwisha na hakuna la maana kwa mpigakura?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sitegemei, lakini kama ikitokea janga la corona likachukua muda mrefu adi kufikia wakati wa kampeni na uchaguzi. Je katiba ama sheria za nchi hazikuweka kipengele cha dharura kinachoweza kutumika kusogeza muda?
 
Back
Top Bottom