Je, binadamu ni mwili au roho?

munyinya

Member
Jul 31, 2015
35
10
Leo nimefikiria swali moja; Je, mimi ni mwili au ni roho?

Nimefikiria kinachotokea mpaka mtoto anazaliwa nimeshindwa kupata jibu.

Hebu fikiria kama nilivyofikiri mimi. Utagundua mwili ni kama gari umepewa uendeshe ila kuna baadhi ya vitu huwezi kuvifanya na vinatokea vyenyewe.

Mimi najiuliza tunapozaa watoto inakuwaje waitwe wa kwetu wakati hatujashiriki kuwatengeneza ila miili yetu yenyewe ndo imetengeneza?

Concept yangu ni hii, ikiwezekana wanasayansi wakaweza kutengeneza mwili sawa na wa binadam na wakawa na uwezo wa kuhamisha roho kutoka mwili mmoja kwenda mwingne basi tutakuwa tumekikwepa kifo.
 
Sisi ni mwili na roho,ila suala la kuhamisha roho toka mwili mmoja kwenda mwengine ni jambo la kufikirika yaani haliwezekani.
 
Dah!! Wale wa kufundisha "Mimi ni nani..?" Waje huku maana watoto tunaozaa ati si wakwetu!!!.
 
Leo nimefikiria swali moja; Je, mimi ni mwili au ni roho?

Nimefikiria kinachotokea mpaka mtoto anazaliwa nimeshindwa kupata jibu.

Hebu fikiria kama nilivyofikiri mimi. Utagundua mwili ni kama gari umepewa uendeshe ila kuna baadhi ya vitu huwezi kuvifanya na vinatokea vyenyewe.

Mimi najiuliza tunapozaa watoto inakuwaje waitwe wa kwetu wakati hatujashiriki kuwatengeneza ila miili yetu yenyewe ndo imetengeneza?

Concept yangu ni hii, ikiwezekana wanasayansi wakaweza kutengeneza mwili sawa na wa binadam na wakawa na uwezo wa kuhamisha roho kutoka mwili mmoja kwenda mwingne basi tutakuwa tumekikwepa kifo.
binadamu ni binadamu
 
Binadamu Kama ilivyo kwa viumbe vingine vyote vyenye uhai ni *NAFSI......tofauti ya wanyama na binadamu ni kua binadamu ni nafsi iliyopewa akili ya utambuzi (UTASHI)

Mwili umeumbwa ukapuliziwa roho nafsi iliyoumbwa kwa lengo maalum hukabidhiwa /huunganishwa na mwili husika (km ni mnyama au mdudu au binadamu ) kuja kutekeleza jukumu Iliyopangwiwa hadi pale muumba wake atakapotaka kuichukua roho ya nafsi husika... Na kupelekea kuoza kwa mwili.. Kwa hiyo hapo tumeona kwamba ni utashi tuu ndo unamtofautisha binadamu na viumbe wengine ukitoa hicho yeyote anaweza fanya chochote

AKILI pia ni kiunganishi kati ya ulimwengu wa kimwili (kupitia milango ya fahamu).... na ulimwengu wa kiroho (kupitia ndoto, hisia maono.,) na ndo tunaita jicho la rohoni uwezo wa kichakata ambao Mungu amempa binadamu ili aweze kukabiliana na changamoto za mazingira yake na kutoa maamuzi sahihi

Na ndio maana inaweza kutokea wakati kunatokea mvutano ndani yako unapohitaji kufanya maamuzi upande ukikubali upande ukikataa ina maana ni nafsi Inabishana na akili... Nafsi ni yenye kutamani tuu lakini akili ni muongozo kwa hiyo ukipatwa na hali hiyo ni vyema kuomba kibali kutoka kwa Mungu huenda mojawapo lisiwe na heri.

Katika vitabu vya dini tunaambiwa mungu atazihukumu nafsi kulingana na matendo yake.......wakati huo huo tunaambiwa kua mahayawani (viumbe visivyokuwa na akili kwa maana ya wanyama na wendawazimu) hawatahukimiwa kwa sababu wao hawakupewa akili hivyo basi kutokana na mafundisho haya utagundua kuwa akili ni mali ya nafsi ya uanadamu na ubora wake umefautiana kulingana na athari za kiafya., kimazingira,.lishe., exposure n.k.

Hivyo Basi binadamu atahukumiwa kulingana na ubora wa akili yake na jinsi alivyoitumi...mfano mtoto mdogo au mwendawazimu hatahukumiwa sawa na mtu wa kawaida aliyefanya kosa lile lile.
Kwa hiyo akili yako ndo inatathmini ubinadamu wa nafsi yako.
 
Uhai ni mazingaombwe!

Huenda hapa tulipo tuko ndotoni tu, na yote tunayoyaona ni mazingaombwe tu!

Vyote unavyoviona huenda havipo, na wewe pia haupo!

Unaota tu!
 
Binadamu ni mwili. Unao unganisha Mwili + nafsi + roho.

Mwili - nyama/mifupa na maji
Nafsi - nafsi/ ndio wewe sasa
Roho - uzima/uungu/pumzi/uhai
Mungu alisema elimu ya roho muachieni yeye..hakuna anaejua kuhusu roho
Ndo maana tunaona hapa roho inaitwa mungu Mara pumzi.
Kwahiyo yule mungu tunaemuabudu ni pumzi (breathing)
 
Uhai ni mazingaombwe!

Huenda hapa tulipo tuko ndotoni tu, na yote tunayoyaona ni mazingaombwe tu!

Vyote unavyoviona huenda havipo, na wewe pia haupo!

Unaota tu!
Yah mungu alisema hakika dunia na mapambo yake ni pumbao (not real or hallucinations) dreams.
Siku ya mwisho mtu akifufuliwa ataona alikuwa amelala kwenye usingizi mzito wenye usiku mmoja.
 
Leo nimefikiria swali moja; Je, mimi ni mwili au ni roho?

Nimefikiria kinachotokea mpaka mtoto anazaliwa nimeshindwa kupata jibu.

Hebu fikiria kama nilivyofikiri mimi. Utagundua mwili ni kama gari umepewa uendeshe ila kuna baadhi ya vitu huwezi kuvifanya na vinatokea vyenyewe.

Mimi najiuliza tunapozaa watoto inakuwaje waitwe wa kwetu wakati hatujashiriki kuwatengeneza ila miili yetu yenyewe ndo imetengeneza?

Concept yangu ni hii, ikiwezekana wanasayansi wakaweza kutengeneza mwili sawa na wa binadam na wakawa na uwezo wa kuhamisha roho kutoka mwili mmoja kwenda mwingne basi tutakuwa tumekikwepa kifo.
Binadamu, ni mkusanyiko wa vitu vitatu.
i. e BINADAMU = MWILI + NAFSI + ROHO.

MUNGU alipo kuwa akiumba mwanadamu, kutoka mavumbini hakukumilika, hadi alipo mpulizia pumzi hai.

Roho ikitoka, na ikabaki mwili peke yake inakuwa si binadamu tena, jina litabadilika na kuitwa marehemu,maiti n. K

Roho ikibaki peke yake, unakuwa katik dimension nyingine kabisa na unakuwa hakuna tofauti ni viumbe wengine, na endapo utakuwa accessable duniani, utaitwa Mzimu n.k

Nafsi ikitoka, ikitolewa kwa ujuzi wa nguvu flani, ikashikwa na kufungiwa sehemu, kwa matumizi yao flani, hapo utakuwa MSUKULE, na ili kuulinda mali yao ambayo ni wew, usije ukatafutwa ndipo hapo utangeneza picha ya kifo, uonekane uliwahi kufa, na kukuweka katika dimension nyingine ili watu wa kawaida wasikuone.

MUNGU ameweka huwezo katika binadamu, kuongezeka na kupiga kopi zao, ili uzao uendelee, ametoa mandatory hiyo automatically. Mbinu na huweza wa kimungu, japo wapo wanaojaribu kuelezea kisayansi na kibaolojia, lakini "Energy can neither be created nor destroyed... " Life ni energy na hizi MUNGU kaziweka ndani yetu. Ukiuza mamlaka yako, wapo wataoweza access energy zako na kuamua kukupiga pin usizae, au uzae wachukue.

" watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
"kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa..."
 
Hakuna kitu kama roho. Hebu tafakari mfano huu. Gari linatembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kuna wakati kutokana na hitilafu, linashindwa kufanya kazi milele. Tunaweza kusema limekufa.

Je, gari nalo lina nafsi/roho?

Turudi kwa binadamu. Kwa nini ninasema hakuna kitu roho?

Unaposema binadamu, maana yake ni ukamilifu. Ukamilifu huu ni pamoja na kuwa hai. Ukamilifu wa marehemu ni kutokuwa na uhai.

Sijui ninaeleweka?

Jiwe ni kamilifu. Ukamilifu wake (hali ya kutokuwa hai ambayo ndio ungeita roho) hauna tofauti na ukamilifu wa binadamu.
 
Back
Top Bottom